Mkoa wa Kagera ni Mkoa masikini zaidi nchini Tanzania; tutaugeuza kituo cha biashara EAC

Kuna haja 50% ya mapato ya kila mkoa yabaki kuunufaisha mkoa husika...

Watu wa kagera sio masikini kiasi hicho, tatizo wanachokichangia kwenye kapu la taifa hakiwafaidishi

Ni kama wakulima wa tumbaku kule tabora...wanachangia kiwango kikubwa kwenye kapu la taifa kwa kilimo cha tumbaku ila mwisho wa siku hata barabara za changarawe hawana na serikali yao imewabandika jina la masikini wa kutupa...

Inasikitisha.
 
Hujaeleza bayana ni kwa namna gani Kagera unaweza kyfanywa kama kituo cha biashara Afrika ya Mashariki.
Utakuwa wa kwanza kupata majibu ya hoja ama mswali yako kutoka kwa mleta mada!!! Maani siku hizi hana utamaduni huo.
 
Ameweka gazeti lake na kutokomea kusikojulikana kimya kimya
 
Mkoa huu una mito mingi mikubwa ya asili na uoto mzuri sana na ardhi yenye rutuba nzuri hususani wilaya ya Kyerwa na Karagwe
Wizara ya kilimo ikitumia vizuri fursa hii hakika kagera inaweza kuongeza pato la taifa kupitia kilimo
nani kakuambia wizara inalima? Wenyeji hawajaona hiyo mito, kwanini wasiitumie. Mi nilichoona huko ni uvivu hakuna kitu kingine. Hayo maeneo wangepata watu km wa kaskazini wape miaka 5 tu uone mabadiliko. Hao watu ni wajuaji wa midomoni, ila ni wavivu wa kufanya kazi. Kagera ni mkoa unaopata mvua nyingi kwa mwaka na uko karibu kabisa na mstari wa ikweta uliopitia hapo Entebe-Uganda kuna ardhi nzuri sana.
 
Economic metrics zinaweza kusema hivyo lakini umaskini wa mikoa yetu hautofautiani ukitoa mikoa michache sana. Kutumia kipimo cha pato la mkoa over population ni yale yale ambayo hata mzee Mkapa aliyakataa.

Mfano mmasai mwenye ng'ombe 5000 kwa vipimo vya uchumi ni maskini! Hivyo zipo njia sahihi za asili kuainisha hali ya uchumi ya mtu mmoja mmoja.

Kuhusu Kagera kwavile ni mkoa ninaotokea, binafsi naona ni mkoa wa kimkakati ambao serikali haijawahi kuwa na lengo la ku tap hizo advantages ambazo mh Zitto amezitaja baadhi.

Mkoa umepakana na nchi nyingi kuliko mkoa wowote sio Tanzania tu bali Afrika mashariki, ni mkoa wenye mvua wakati wote na ardhi kubwa yenye rutuba nzuri.

Ule mkoa ungetumika kama hub ya elimu ya vyuo vya kati hadi university ingekuwa center kwa hata nchi za jirani. Lakini pia kibiashara kama miundombinu ya uwanja wa ndege na reli ikiwa sawa wafanyabiashara wa nchi jirani wangetumia Bukoba kama center badala ya Mwanza.

Kilimo cha kahawa ni kama kimekufa inabidi kipewe nguvu upya maana ndio ilikuwa kimbilio la wananchi wengi maskini.
 
Inabidi Mh.Zitto ajipambanue na utaalam wake wa uchumi bila kufanya hivvyo atapuuzwa tu.
 
Vyuo vimefunguliwa vitatu ili kuleta chachu ila alipokuja ndugu yenu akavifunga.
 
Jamaa usitafute political advantage kwa kutumia mkoa wa Kagera, mengi humo umeandika pumba ungeanza kutatua matatizo ya ndugu zako wanaoishi nyumba za nyasi. Eti Kagera haizalishi chakula, ni lini serikali imepeleka chakula cha msaada huko?? Bwege tafuta sifa kwingine sio Kagera.
 
Jamaa anatumia GDP per capita ya mwaka 2019/2020 ambayo hata population iliyotumika haikuwa halisi, kama Kagera ni maskini hivo mbona mapato ya halmashauri inafanya vizur kuliko mikoa mingi kwani hayo mapato yanatoka wapi?? Pato la taifa ni kwa sababu hakuna uwekezaji mkubwa kama viwanda vikubwa au madini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…