Mkoa wa Kagera unakuwaje masikini wa kutupwa na una kila kitu?

Mkoa wa Kagera unakuwaje masikini wa kutupwa na una kila kitu?

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
1,726
Reaction score
3,391
Mkoa wa Kagera ni mfano halisi wa ujinga wa mtu mweusi. Mkoa unaardhi nzuri na mvua ya kutosha. Ndiyo maana wanaweza kulima mazao kama kahawa na ndizi, na miwa, mazao ya nahohitaji hali nzuri ya hewa. Mkoa umepakana na nchi mbili, Rwanda na Uganda, labda na Burundi pia.

So kibiashara umekaa eneo zuri sana. Ungeweza kuwa hata gateway ya kwenda mashariki ya DRC. Mkoa una ziwa kubwa. Watu wake wanabidii ya kutafuta elimu.

Sasa mkoa kama huu unakuwaje masikini wa kutupwa?

Naomba kujua mambo yanayosababisha mkoa wa Kagera kuwa masikini?
 
Mkoa wa Kagera ni mfano halisi wa ujinga wa mtu mweusi. Mkoa unaardhi nzuri na mvua ya kutosha. Ndiyo maana wanaweza kulima mazao kama kahawa na ndizi, na miwa, mazao ya nahohitaji hali nzuri ya hewa. Mkoa umepakana na nchi mbili, Rwanda na Uganda, labda na Burundi pia. So kibiashara umekaa eneo zuri sana. Ungeweza kuwa hata gateway ya kwenda mashariki ya DRC. Mkoa una ziwa kubwa. Watu wake wanabidii ya kutafuta elimu. Sasa mkoa kama huu unakuwaje masikini wa kutupwa?
Naomba kujua mambo yanayosababisha mkoa wa Kagera kuwa masikini?
Hauna mamlaka au political power, unagawiwa kiduchu kutoka dar es salaam.
 
Sababu ni zile zile tu zinazofahamika.. na almost mikoa mingi ya Tanzania iko ivyo..na sababu zinafanana everywhere
  • Inequality or social injustice
  • Lack of education
  • Poor basic infrastructure
  • Selfishness
  • Much know
  • Poor Government support
 
Mkoa wa Kagera ni mfano halisi wa ujinga wa mtu mweusi. Mkoa unaardhi nzuri na mvua ya kutosha. Ndiyo maana wanaweza kulima mazao kama kahawa na ndizi, na miwa, mazao ya nahohitaji hali nzuri ya hewa. Mkoa umepakana na nchi mbili, Rwanda na Uganda, labda na Burundi pia. So kibiashara umekaa eneo zuri sana. Ungeweza kuwa hata gateway ya kwenda mashariki ya DRC. Mkoa una ziwa kubwa. Watu wake wanabidii ya kutafuta elimu. Sasa mkoa kama huu unakuwaje masikini wa kutupwa?
Naomba kujua mambo yanayosababisha mkoa wa Kagera kuwa masikini?
Una watu Wana mdomo sana badala ya kufanya kazi.
 
Huo Mkoa Wana diaspora wengi sana, lakini remmittance zote zinaishia Dsm,Mwanza na Arusha, wanaogopa kujenga kwao, ushirikina mwingi, ma nyaruju.

Nilitarajia Mkuu wa Mkoa aanze kampeni ya Kila familia kupanda parachichi, hakuna, michikichi, hakuna, labda aongee na SIDO wajenge mashine kubwa za kukamua chikichi, hakuna, yeye anatukanana na wanasiasa tu.

Natarajia tarehe ijayo SSH amuhoji kuhusu parachichi na chikichi
 
Mtausema sana huu mkoa. Watanzania mna roho ya kwanini.
Mkoa unatoa wasomi sana lkn mliweuwekea passmark za juu sana. Wahaya walikimbilia mikoa mingine kutafuta elimu. Kuna wahaya Wana majina mpaka ya Kimasai. Wakati wagogo wakirudisha namba za mitihani wao wameshinda hata Kama hawakuandika chochote. Kagera ilikuwa na shule nyingi miaka ya sabini kuliko mikoa mingi lkn walijaa makabila mengine tena wenye passmark kdg. Kisa NYERERE HAKUWAPENDA NA ALISEMA HAKUNA MHAYA KUWA RAIS. Mambo mengi yaliyofanywa tangu nyuma ndiyo yanaonekana leo. Na mpaka sasa bado mnawachukia hawa wahaya. Kama mnakubali kuwa wameelimika na elimu.ni ufunguo wa maisha, kwanini hawa wahaya wasifunguliwe maisha?
 
Tabia za watu wa Kagera, wajuaji sana, wanajua hadi eti Kiingereza/kizungu kuliko british wenyewe..!! Wahaya ni shida, wabishi kuliko watu wa kigoma, but kiuhalisi kumbe hawajui mambo vizuri, sbb anaejua mambo vizuri hujikamua katika lindi la umaskini.
 
Mkoa wa Kagera ni mfano halisi wa ujinga wa mtu mweusi. Mkoa unaardhi nzuri na mvua ya kutosha. Ndiyo maana wanaweza kulima mazao kama kahawa na ndizi, na miwa, mazao ya nahohitaji hali nzuri ya hewa. Mkoa umepakana na nchi mbili, Rwanda na Uganda, labda na Burundi pia. So kibiashara umekaa eneo zuri sana. Ungeweza kuwa hata gateway ya kwenda mashariki ya DRC. Mkoa una ziwa kubwa. Watu wake wanabidii ya kutafuta elimu. Sasa mkoa kama huu unakuwaje masikini wa kutupwa?
Naomba kujua mambo yanayosababisha mkoa wa Kagera kuwa masikini?
Burundi hawana purchasing power kubwa pamoja na kwamba ni mamilioni ya watu. Kagera almost haina cha kuuza Burundi.
Rwanda haina cha kununua kinachozalishwa Kagera zaidi ya kutumika kama transit ya bidhaa.
Mwanza inachukua vitu vingi zaidi ya hizi nchi mbili.

Uganda na Kagera wanafanana kila kitu, Kagera inafanana Uganda kuliko mkoa wowote Tanzania. Ni sawa uitake Songea inunue mahindi ya Rukwa.

Serikali inapiga marufuku kuuzwa mazao nje ya nchi, kahawa inauzwa bei ndogo sana haimshawishi mkulima kuweka juhudi. Vanilla ndio hiyo bei inapanda na kushuka zaidi ya 50% kwa msimu. Bei ya vanilla Uganda huwa ni almost twice ya Kagera, bei ya kahawa Uganda miaka yote inakuwa juu ila jichanganye ukamatwe unaitorosha uone. Border tunayo-share na Uganda ni ndogo na sehemu nyingine hazina makazi hivyo ni rahisi kuilinda tofauti na border mfano na Kenya utailinda uimalize ile? Kwahiyo kufanya smuggling kule ni rahisi.

Kagera iko more than 1000km kutoka bandarini, ni gharama kubwa kusafirisha bidhaa na mazao mengi kutoka kule hayafiki sokoni au yakifika inabidi yafidie higher transport cost na hivyo hayapo competetive kwenye soko. Ukifunga ndizi kuzileta Dar zinaweza iva kabla hujafika.

Na mwisho ni priorities za central government. Sipendelei Federation kwa Afrika maana zinasumbua umoja ila Tanzania hii central government yetu kuna mikoa haina vipaumbele. Bora Kagera tutasingizia iko mbali, Lindi je? Mtwara wanavuna korosho hata serikali kuweka kiwanda kikubwa cha kubangua hawawezi mpaka korosho iende unprocessed kwenye magunia.
 
Tabia za watu wa Kagera, wajuaji sana, wanajua hadi eti Kiingereza/kizungu kuliko british wenyewe..!! Wahaya ni shida, wabishi kuliko watu wa kigoma, but kiuhalisi kumbe hawajui mambo vizuri, sbb anaejua mambo vizuri hujikamua katika lindi la umaskini.
Hakuna mhaya maskini acha habari zenu za hovyo.Wahaya ni sehemu ndogo ya mkoa wa kagera kama hiyo habari ulikuwa hujui.

Mkoa wa kagera una makabila yafuatayo:Wanyambo(wenyeji wa Karagwe),wasubi(wenyeji wa Biharamulo) wahangaza(wenyeji wa Ngara).

Nitajie sehemu yoyote ukiondoa hii miji na mkoa wa Kilimanjaro ambao watu wake kijijini wa na makazi bora kama sio kwa wahaya tu.

Nimekaa karibu sehemu zote hapa Tanzania ila ukitoka tu mjini huko kijijini ni hatari tupu
 
tatizo nguvu kazi haipo kagera. Vijana wote wenye nguvu wapo katoro, geita, kahama na mwanza wanaendesha bodaboda
Haya dada zao ndo kama hivyo unategemea nini?

Wamebaki wazee mamwinyi wenye ardhi ya nyarubanja hawataki iguswe. Kingine wageni wanabaguliwa eti ni wanyamahanga hata ukifungua duka kama sio muhaya hupati wateja sasa ndo mambo gani haya?
 
Mtausema sana huu mkoa. Watanzania mna roho ya kwanini.
Mkoa unatoa wasomi sana lkn mliweuwekea passmark za juu sana. Wahaya walikimbilia mikoa mingine kutafuta elimu. Kuna wahaya Wana majina mpaka ya Kimasai...
Hata Mbeya na Kilimanjaro hayo yalifanyika lakini hukuti umasikini kama unaotajwa Kagera kuwa nao.
 
Hivi bado soko kuu Bukoba siku ya jumapili linafungwa mchana?😁

Bukoba ikifika saa mbili kamji kanakuwa kimyaaa

Mpaka wa Mutukula ni waganda ndio wanaunogesha

Kagera Kuna ardhi nzuri sana, kwa mfano misenji ni 🔥tatizo uvivu

Kuna biashara ukianzisha na usipokuwa wa kwao utapata tabu

Stendi ya Bukoba ni aibuu mvua ikinyesha

Mzunguko wa pesa ni mdogo sana Kagera, tuliwahi kuishi Karagwe kwa miezi minne, umaskini tuliokutana NAO ni mkubwa sana.

Q bar sijui bado ipo?

Halmashauri Haina root za hiace....

Wenyeji kuuza ardhi ni wagumu sana

Niliwahi kwenda Bugabo nusura niliwe
 
Kimsingi huo umasikini mnaousemea mkoa wa Kagera ni wa kufikirika. Mkifika kule mkaona mijengo ilivyo na hali ya watu ilivyo ndo mtakasirika zaidi
Hakuna anayekasirika hapa. Tunataka kujifunza kitu juu ya hii paradox ya umasikini Kagera.
 
Back
Top Bottom