Mkoa wa Kagera unakuwaje masikini wa kutupwa na una kila kitu?

Mkoa wa Kagera unakuwaje masikini wa kutupwa na una kila kitu?

Eti soko la Bukoba ni baya Mara stand Mbaya... Nyie mikoa yenu stand na masoko mlijijengea wenyewe? Huku Kijichi tumejenhewa soko na world Bank lkn tunalikimbia. Stand pia tumejengewa Kijichi lkn hatuhitaji. Bukoba mnawatukana na kuwabeza mnataka wajijengee stand. Wajijengee soko? Nadhani hata hiyo barabara ya lami imejengwa kwasababu ya Uganda
Pesa ya soko na stand imetengwa tangu enzi za Kikwete mpaka leo ubishani wenu wa kibaguzi lijengwe wapi na kwanani mpaka leo Kagasheki na Meya Kalumna ukiongea uwe na uhakika hata madiwani wa Bukoba ni wabaguzi hawataki mtumishi ambae sio muhaya ukiitwa ujieleze kwa kihaya Wahaya mnatafunwa na ubaguzi wenu wataalam wanashindwa kifanya kazi kwenu mambo ya Soko kujengwa na WB uzushi tuu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Mkoa wa Kagera ni mfano halisi wa ujinga wa mtu mweusi. Mkoa unaardhi nzuri na mvua ya kutosha. Ndiyo maana wanaweza kulima mazao kama kahawa na ndizi, na miwa, mazao ya nahohitaji hali nzuri ya hewa. Mkoa umepakana na nchi mbili, Rwanda na Uganda, labda na Burundi pia.

So kibiashara umekaa eneo zuri sana. Ungeweza kuwa hata gateway ya kwenda mashariki ya DRC. Mkoa una ziwa kubwa. Watu wake wanabidii ya kutafuta elimu.

Sasa mkoa kama huu unakuwaje masikini wa kutupwa?

Naomba kujua mambo yanayosababisha mkoa wa Kagera kuwa masikini?
TUMIA AKILI TANZANIA KAMA NCHI INA KILA KITU LAKINI WATU WAKE NI MASIKINI ITAKUWA KAGERA?
 
Hivi bado soko kuu Bukoba siku ya jumapili linafungwa mchana?😁

Bukoba ikifika saa mbili kamji kanakuwa kimyaaa

Mpaka wa Mutukula ni waganda ndio wanaunogesha

Kagera Kuna ardhi nzuri sana, kwa mfano misenji ni 🔥tatizo uvivu

Kuna biashara ukianzisha na usipokuwa wa kwao utapata tabu

Stendi ya Bukoba ni aibuu mvua ikinyesha

Mzunguko wa pesa ni mdogo sana Kagera, tuliwahi kuishi Karagwe kwa miezi minne, umaskini tuliokutana NAO ni mkubwa sana.

Q bar sijui bado ipo?

Halmashauri Haina root za hiace....

Wenyeji kuuza ardhi ni wagumu sana

Niliwahi kwenda Bugabo nusura niliwe
Bugabo wanakulaga watu hahahaa,

Wanasema jumapili ni siku ya kwenda kusali na kuona wazee vijijini, hii ya kusali inatokana na influence ya wakoloni walipoleta dini ya kikristo.

Kuna maeneo kama Katoro, kule Wana sifa ya kushutakiana mpaka mahakama zote ziishe.

Ila Mutukula naona upande wa Tanzania Kuna maduka yanajengwa mengi sana, sijui kama yatajaa. Wanajenga wale jamaa wa Prince Hotel.

Cha kuchekesha, asilimia fulani ya wafanyabiashara upande wa Mutukula ya Uganda ni watanzania, wanafungua maduka, jioni wanatudi Tz kulala.

Sehemu inayofanya biashara na Mutukula ni kahama na shinyanga, wanapeleka mchele sana. Bukoba hawana Cha kupeleka Uganda, kwa kuwa walichonacho na waganda wananchi. Kwa Sasa naona wasukuma wanaingia kagera kuanza kulima katika mabonde yenye maji, wanalima mpunga, lakini kwa hofu sana, ukiwasikuliza masimulizi yao, yamejaa tahadhari ya kudhulumiwa ardhi na wazawa.

Kwa upande mwingine, Kagera inaweza kupeleka nyanya Uganda au passion fruits huko, zina soko sana, minziro walianza kulima na kupeleka Uganda, sijui msukumo wao Kama bado upo.

Burundi wanapenda sana unga wa muhogo, labda Biharamulo ndio wataweza kuuza kwa kuwa ardhi yao inaruhusu muhogo kustawi.

Q-Bar ni maarufu sana,ila imekuwa danguro, zamani ilivuta watu kwa sababu waganda walikuwa wanacheza nusu uchi.

Pale Ngara, Kuna bar inaitwa New Happy, ya bwana Tuombe, marehemu, walikuwa na wahudumu warundi, mashalaaaa.

Uganda wanapeleka ndizi nje ya nchi, serikali itume timu ya wataalamu wakajifunze the whole process.

Kwa kumalizia tu, kama umeenda kwenye duka la muhaya una elfu kumi, unanunua bidhaa ya 2000, atakwambia Sina chenji, hajihangaishi hata kwenda duka la jirani kuomba chenji
 
Tatizo letu watu weusi hatuna desturi ya kukubali na kuambizana ukweli. Tukielezwa tusiyopenda kuyasikia tunanuna.

Nikiwa kama mhaya nakubali kweli kabisa mkoa wetu una matatizo na watu wake. Mimi mvivu kuandika humu. Ningeandika.
 
Mkoa wa Kagera ni mfano halisi wa ujinga wa mtu mweusi. Mkoa unaardhi nzuri na mvua ya kutosha. Ndiyo maana wanaweza kulima mazao kama kahawa na ndizi, na miwa, mazao ya nahohitaji hali nzuri ya hewa. Mkoa umepakana na nchi mbili, Rwanda na Uganda, labda na Burundi pia.

So kibiashara umekaa eneo zuri sana. Ungeweza kuwa hata gateway ya kwenda mashariki ya DRC. Mkoa una ziwa kubwa. Watu wake wanabidii ya kutafuta elimu.

Sasa mkoa kama huu unakuwaje masikini wa kutupwa?

Naomba kujua mambo yanayosababisha mkoa wa Kagera kuwa masikini?
Wanatakiwa wawe na utangamano na wananchi wenzao wanaotoka mikoa mingine wasiwabague then maendeleo yatakuja haraka sana !! Nimesikia lakini sina uhakika kama ni kweli kwamba wenyeji wa huko wana kaubaguzi baguzi kwa wahamiaji kutoka mikoa mingine !!
 
Inauma Tanzania kuzidiwa na Ukraine kulima
Mito imejaa Nchini, maziwa yapo kibao tena ni maziwa makuu na mvua zipo za kutosha lakini maji ya mvua yanaishia baharini au kule yasikohitajika !! Tumeshindwa kufanya kilimo cha umwagiliaji japo katika nusu ya Nchi tu !! Ukiuliza kwanini inakuwa hivyo utaambiwa Hakuna pesa !! Sasa swali ni kwamba Nchi itapata wapi pesa kama hakuna mipango imara na ya uhakika ya kupatia pesa ???!!! Miaka yote tangu nikiwa mtoto nilikuwa nasikia slogan ya Kilimo ni Uti wa mgongo wa Nchi yetu !! Je bandugu kulikoni ?! Kama Ukraine 🇺🇦 wameweza sisi tushindwe kwanini ??!! Kupanga ni kuchagua tukidhamiria na kujinyima haya mambo ya kula Bata TUTAWEZA TU !!
 
Pls usilinganishe mimba na Kitambi muhaya Kilimanjaro umefika au hata kupita?? Kagera hata stand ya mabasi hakuna chuo Kikuu hata kimoja hakuna unabishana kwa kututajia makabila so what?? Yamesaidiaje mkoa kutoka kwenye umaskini uliotopea ??

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Hamna shukrani nyie watu.Ndio tunajua haya yote yanatokea baada ya watu kuwa na tumaini kwamba kuna siku wahaya watakomboa hili taifa kutoka kwenye umaskini na hii imepelekea muwe na hasira juu yetu kwa maana mnaona taifa lenu maskini na sisi bado tunaishi.

Sawa ukombozi utafanyika kuweni na subra.Kingine mimi hako ka Kilimanjaro nilikapaisha tu.There is nothing special in that place.

Huu ndio ukweli wetu sasa,before the Germans showed up,we had the greatest civilisation(having best schools,practising religion,conducting a well organised trade with people from Buganda kingdom,practising agriculture with advanced technology,having a bible and other books in haya language,just to make a list shorter) and these were the reasons why we managed to negotiate with them.

Sasa nyie mmepata ustarabu kidogo tu kutoka kwetu leo mnatulabel hovyo hivi.Hivi ni kabila lipi limejenga stendi,soko,n.k kwenye maeneo yao?.Kama unataka kuliona hilo waeleze serikali kuu waache kuchukua mapato yetu na tuwe watu huru.Then kesho ukiona hayo hayafanyiki njoo na maneno yenu ya hivi.

Anyway,pambaneni na sisi lakini usisahau ya kuwa mkombozi wa ulimwengu huu ni mhaya.Ikawe siku njema kwako kaka.
 
Mkoa wa Kagera ni mfano halisi wa ujinga wa mtu mweusi. Mkoa unaardhi nzuri na mvua ya kutosha. Ndiyo maana wanaweza kulima mazao kama kahawa na ndizi, na miwa, mazao ya nahohitaji hali nzuri ya hewa. Mkoa umepakana na nchi mbili, Rwanda na Uganda, labda na Burundi pia.

So kibiashara umekaa eneo zuri sana. Ungeweza kuwa hata gateway ya kwenda mashariki ya DRC. Mkoa una ziwa kubwa. Watu wake wanabidii ya kutafuta elimu.

Sasa mkoa kama huu unakuwaje masikini wa kutupwa?

Naomba kujua mambo yanayosababisha mkoa wa Kagera kuwa masikini?
Kuwa na kila kitu kipi? Kuna nchi zina badili jangwa kuwa eneo la kilimo,
 
Dar es salam Arusha na Mwanza ndo kipau mbele cha serikali mkoa migine inafanana tu. Tofauti yao ni ndogo.
Mwanza sio kipaumbele , ingekuwa kipaumbele ingekuwa jiji bora kabisa duniani kielimu, miundombinu na afya, na hakuna mtu angeenda Dar kutafuta elimu, Dodoma, Dar na Arusha ndio vipaumbele licha ya Mwanza kukua kwa kasi zaidi baada ya Dar es salaam.
 
Umasikini ni Nini ? Labda tuanzia hapo.....

Miaka kadhaa hapo nyuma Household ilikuwa na Makazi yenye natural Air Condition (Clay Building) ina natural carpet kwa afya yao (Nyasi) na ina efficient Laundry (mtoni kila once a week ambapo kuna recycling of water) Vyoo vilikuwa natural havipotezi maji kuliko sasa ambapo watu tuna-shit where we are eating...., Mtu huyu alikuwa na uhakika wa milo mitatu na kila mtu kwenye store yake ana access ya kinywaji mwaka mzima kila anapotaka.... (na siongelei maji ambayo nayo alipata naongelea kinywaji - Yaani kilevi cha kula Bata) mtu huyu alikuwa anapata leisure ya kumwaga, ngoma za hapa na pale - in short huyu mtu yeye na tabasamu ilikuwa ni kama chanda na pete.....

In comparison chukua mkoa wowote ambao unasema ni so called Tajiri wa kuongoza hapa Tanzania au nichukue mfano wa Dar...., kuna watu wanakaa kwenye slums (sio wachache a good number) majority hawana uhakika wa milo mitatu let alone akiamka asubuhi kujua kama atapata pesa ya kumlisha jioni (stress of the mind), Wote mobility ni hatari yaani katika maisha yao wanatumia takribani miaka mitatu mpaka minne wakiwa kwenye traffic / usafiri kutoka point A mpaka B;..... badala ya kuzalisha au kula bata na ndugu zao..., wanaishi kwenye dumpster na hata maji wanayokunywa ukifuatilia leave a lot to be desired......... In short for an onlooker they are in a rat race.....

Kwahio narudia tena naomba definition ya Umasikini na utagundua kwamba Tanzania nzima Umasikini kwa wengi umeongezeka na watu kujiliwaza na toys za hapa na pale - mbaya zaidi ni umasikini wa fikra na kuwa na distorted view ya utajiri ambayo imekuwa promoted na consumerism, marketing na excessive wants with less access for important needs for the majority
 
Umaskin wa kagera unatokana na geographic position yake.
Mfano:
Kilimo hakina soko, ardhi ya Uganda inazalisha kuzidi kagera
Mwanza lazima meli usafiri gharama otherwise uzunguke kwa muda mrefu
 
Umasikini ni Nini ? Labda tuanzia hapo.....

Miaka kadhaa hapo nyuma Household ilikuwa na Makazi yenye natural Air Condition (Clay Building) ina natural carpet kwa afya yao (Nyasi) na ina efficient Laundry (mtoni kila once a week ambapo kuna recycling of water) Vyoo vilikuwa natural havipotezi maji kuliko sasa ambapo watu tuna-shit where we are eating...., Mtu huyu alikuwa na uhakika wa milo mitatu na kila mtu kwenye store yake ana access ya kinywaji mwaka mzima kila anapotaka.... (na siongelei maji ambayo nayo alipata naongelea kinywaji - cha kupata bata) mtu huyu alikuwa anapata leisure ya kumwaga, ngoma za hapa na pale - in short huyu mtu yeye na tabasamu ilikuwa ni kama chanda na pete.....

In comparison chukua mkoa wowote ambao unasema ni so called Tajiri wa kuongoza hapa Tanzania au nichukue mfano wa Dar...., kuna watu wanakaa kwenye slums (sio wachache a good number) majority hawana uhakika wa milo mitatu let alone akiamka asubuhi kujua kama atapata pesa ya kumlisha jioni (stress of the mind), Wote mobility ni hatari yaani katika maisha yao wanatumia takribani miaka mitatu mpaka minne wakiwa kwenye traffic / usafiri kutoka point A mpaka B;..... badala ya kuzalisha au kula bata na ndugu zao..., wanaishi kwenye dumpster na hata maji wanayokunywa ukifuatilia leave a lot to be desired......... In short for an onlooker they are in a rat race.....

Kwahio narudia tena naomba definition ya Umasikini na utagundua kwamba Tanzania nzima Umasikini kwa wengi umeongezeka na watu kujiliwaza na toys za hapa na pale - mbaya zaidi ni umasikini wa fikra na kuwa na distorted view ya utajiri ambayo imekuwa promoted na consumerism marketing na excess wants with less access for important needs for the majority
Umemaliza!!!
Kuna watu wanaona wamasai masikini ila ukiwauliza kwenu lini familia imekula nyama na maziwa hawakumbuki
Zaidi ya dagaa
 
Hakuna mkoa uliochukiwa na kupigwa vita kama Kilimanjaro. Nyerere alifanya uharibifu wa kimbari huko lakini watu walikimbilia Kenya kusoma na kufanya biashara. KNCU chama cha ushirikina wa kahawa kilionekana tishio kikafungwa pamoja na vyama vingine mwaka 1977 lakini Nyerere aligundua anafanya makosa akavifungua.

Watu wa Kagera kama mnataka maendeleo pendeni kwenu na jengeni mazoea ya kufika nyumbani mara kwa mara kama wachagga. Wachagga wana msemo wao: East, West, North, South, home is best!
Mtausema sana huu mkoa. Watanzania mna roho ya kwanini.
Mkoa unatoa wasomi sana lkn mliweuwekea passmark za juu sana. Wahaya walikimbilia mikoa mingine kutafuta elimu. Kuna wahaya Wana majina mpaka ya Kimasai. Wakati wagogo wakirudisha namba za mitihani wao wameshinda hata Kama hawakuandika chochote. Kagera ilikuwa na shule nyingi miaka ya sabini kuliko mikoa mingi lkn walijaa makabila mengine tena wenye passmark kdg. Kisa NYERERE HAKUWAPENDA NA ALISEMA HAKUNA MHAYA KUWA RAIS. Mambo mengi yaliyofanywa tangu nyuma ndiyo yanaonekana leo. Na mpaka sasa bado mnawachukia hawa wahaya. Kama mnakubali kuwa wameelimika na elimu.ni ufunguo wa maisha, kwanini hawa wahaya wasifunguliwe maisha?

Burundi hawana purchasing power kubwa pamoja na kwamba ni mamilioni ya watu. Kagera almost haina cha kuuza Burundi.
Rwanda haina cha kununua kinachozalishwa Kagera zaidi ya kutumika kama transit ya bidhaa.
Mwanza inachukua vitu vingi zaidi ya hizi nchi mbili.

Uganda na Kagera wanafanana kila kitu, Kagera inafanana Uganda kuliko mkoa wowote Tanzania. Ni sawa uitake Songea inunue mahindi ya Rukwa.

Serikali inapiga marufuku kuuzwa mazao nje ya nchi, kahawa inauzwa bei ndogo sana haimshawishi mkulima kuweka juhudi. Vanilla ndio hiyo bei inapanda na kushuka zaidi ya 50% kwa msimu. Bei ya vanilla Uganda huwa ni almost twice ya Kagera, bei ya kahawa Uganda miaka yote inakuwa juu ila jichanganye ukamatwe unaitorosha uone. Border tunayo-share na Uganda ni ndogo na sehemu nyingine hazina makazi hivyo ni rahisi kuilinda tofauti na border mfano na Kenya utailinda uimalize ile? Kwahiyo kufanya smuggling kule ni rahisi.

Kagera iko more than 1000km kutoka bandarini, ni gharama kubwa kusafirisha bidhaa na mazao mengi kutoka kule hayafiki sokoni au yakifika inabidi yafidie higher transport cost na hivyo hayapo competetive kwenye soko. Ukifunga ndizi kuzileta Dar zinaweza iva kabla hujafika.

Na mwisho ni priorities za central government. Sipendelei Federation kwa Afrika maana zinasumbua umoja ila Tanzania hii central government yetu kuna mikoa haina vipaumbele. Bora Kagera tutasingizia iko mbali, Lindi je? Mtwara wanavuna korosho hata serikali kuweka kiwanda kikubwa cha kubangua hawawezi mpaka korosho iende unprocessed kwenye magunia.

Hakuna mhaya maskini acha habari zenu za hovyo.Wahaya ni sehemu ndogo ya mkoa wa kagera kama hiyo habari ulikuwa hujui.

Mkoa wa kagera una makabila yafuatayo:Wanyambo(wenyeji wa Karagwe),wasubi(wenyeji wa Biharamulo) wahangaza(wenyeji wa Ngara).

Nitajie sehemu yoyote ukiondoa hii miji na mkoa wa Kilimanjaro ambao watu wake kijijini wa na makazi bora kama sio kwa wahaya tu.

Nimekaa karibu sehemu zote hapa Tanzania ila ukitoka tu mjini huko kijijini ni hatari tupu

Kimsingi huo umasikini mnaousemea mkoa wa Kagera ni wa kufikirika. Mkifika kule mkaona mijengo ilivyo na hali ya watu ilivyo ndo mtakasirika zaidi
 
Mkuu kanda ya ziwa yote ni masikini watupu. Kidogo mwanza kuna masikini waliochangamka. Ila uko kagera, geita sijui wapi shinyanga yani uchawi unawarudisha nyuma hawa watu.

Alafu wanapenda novida ni balaa
 
Mkoa wa Kagera ni mfano halisi wa ujinga wa mtu mweusi. Mkoa unaardhi nzuri na mvua ya kutosha. Ndiyo maana wanaweza kulima mazao kama kahawa na ndizi, na miwa, mazao ya nahohitaji hali nzuri ya hewa. Mkoa umepakana na nchi mbili, Rwanda na Uganda, labda na Burundi pia.

So kibiashara umekaa eneo zuri sana. Ungeweza kuwa hata gateway ya kwenda mashariki ya DRC. Mkoa una ziwa kubwa. Watu wake wanabidii ya kutafuta elimu.

Sasa mkoa kama huu unakuwaje masikini wa kutupwa?

Naomba kujua mambo yanayosababisha mkoa wa Kagera kuwa masikini?
Hao ndio wahaya kutwa jf kushindana na wachaga haha
 
Back
Top Bottom