Mkoa wa Kagera unakuwaje masikini wa kutupwa na una kila kitu?

Sababu ni zile zile tu zinazofahamika.. na almost mikoa mingi ya Tanzania iko ivyo..na sababu zinafanana everywhere
  • Inequality or social injustice
  • Lack of education
  • Poor basic infrastructure
  • Selfishness
  • Much know
  • Poor Government support
much know[emoji879]
 
Maendeleo binfsi huletwa na juhudi ya mtu mwenyewe na sio wanasiasa hasa wa bongo
 
Komenti ya Hawa akiongea na nyoka Eden
 

Remittance wameanza kupata hata kabla ya Uhuru
 
Umasikini unaozungumziwa Kagera ni porojo,propaganda ambazo huwezi kuzichambua kisayansi ,labda unazungumza sana na watani wetu. Mimi nikiangalia vigezo vya umasikini Kagera inavivuka. Mathalaani ukiangalia swala la Elimu tupo viwango vya juu.Makazi tupo juu labda kipato Cha Kila mwananchi kinakumbana na vikwazo vingi ambavyo kuvielezea hapa sio rahisi.Fikeni Kagera uone Hali kihuhalisia kuliko kukaa Mara na Kigoma kuleta mambo ya utani na kuandika kejeli zisizo halisi.
 
Umemaliza kila kitu kwa mlengo chanya bila kuweka dhoruba tunazopitia bila ya kupewa msaada na serikali
 
Siku moja Serikali iandae sheria ya kuruhusu wahaya wauze mazao yao ya kilimo nje ya nchi bila kuingiliwa na mtu yeyote halafu ikusanye takwimu tuone huo umaskini. Umaskini wa Kagera ni wa kutengeneza.
 
Ziwa Victoria upande wa Kagera wameshindwa kutumia vizuri fukwe zao kuweka hotel au beach nzuri za kuvutia wageni na watalii ingawa wana maeneo mazuri.

Uvuvi unafanyika kiwango cha kawaida, Bukoba inatakiwa wapambane wawe na kiwanda cha kuchakata samaki. Wavuvi wengine wanatoka sehemu za Mwanza wanasogea mpaka Bukoba kuvua samaki na dagaa.

Usafiri wa abiria kutoka Bukoba Port kwenda visiwani wanatumia boti ndogo za mbao na nyingine sio salama kulingana na idadi ya abiria. Kwenye meli za mizigo kati ya Uganda na Bukoba zilikuwa zinaleta sabuni na mafuta kutoka kiwanda cha mukwano. Matajiri na diaspora wakiwekeza mji utapanuka kibiashara, kuna wahindi walikuwa Port Bell Uganda na Boti za Earth Wise lengo lao ilikuwa ni kufanya trip za Uganda - Bukoba wakakwama.
 
Afadhali wewe umeongea kwa hoja. Watu hawajui kwamba Biharamulo na Ngara pia ni sehemu ya Kagera. Pia wengi wao wanatumia kigezo cha stand na soko kuhalalisha umaskini wa Kagera. Wachache waliotembelea vijiji vya Muleba, Kyerwa, Karagwe na Misenyi.
 
Kwenye hili uko sahihi lakini wahaya wanaogopa kuhujumiwa na Serikali. Wengi wangependa kuwekeza lakini kahawa tu imehujumiwa mpaka watu wakafyeka mashamba
 
Kuna kiwanda Cha samaki kemondo na pia Bukoba mjini.
 
Watanzania hamtaki watu wanaojiamini. Hilo linatukwaza sana. Ona report ya CAG. Wizi mwingi lkn hakuna mtu wa kujiamini hata kuhoji
Tunaibiwa na tunanyamaza kama makuku tu. Kwani kujua English wamemkosea nani.
 
Mkoa wa Kagera... Umejaa ushirikina, ubinafsi na wazee tu... Biashara hazifanyiki, Wageni wanarogwa na kupigwa vita... Wamebaki wao tu wahaya unadhan mkoa utachangamka...? Ndiyo maana RC Chalamila anawatukana kilasiku waache ubinafsi na ushirikina ili wapate maendeleo...
 
Bugabo kwao na akina Dio πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…