GE2025 Mkoa wa Morogoro: Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2025 kama yanavyotujia

GE2025 Mkoa wa Morogoro: Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2025 kama yanavyotujia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Wakuu,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Morogoro. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mkoa wa Morogoro una una jumla ya majimbo ya uchaguzi (11) ambayo ni
  1. Jimbo la Kilosa​

  2. Jimbo la Mikumi​

  3. Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki​

  4. Jimbo la Morogoro Kusini​

  5. Jimbo la Morogoro Mjini​

  6. Jimbo la Mlimba​

  7. Jimbo la Kilombero​

  8. Jimbo la Ulanga​

  9. Jimbo la Malinyi​

  10. Jimbo la Mvomero​

  11. Jimbo la Gairo​


Kupata matukio ya nyuma kabla ya siku ya Uchaguzi soma > PreGE2025 - Morogoro: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Updates (Walioshinda Ubunge Mkoa wa Morogoro)

CCM imeshinda majimbo 11 ya uchaguzi.

Majimbo yote ni kama Ifuatavyo;
  1. Jimbo la Kilosa - Prof. Palamagamba John Kabudi
  2. Jimbo la Mikumi - Dennis Lazaro Londo
  3. Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki - Hamisi Shabani Tale Tale
  4. Jimbo la Morogoro Kusini - Zuberi Yahaya Mfaume
  5. Jimbo la Morogoro Mjini - Abdul Aziz Mohamed Abood
  6. Jimbo la Mlimba - Kellen Rose Rwakatare
  7. Jimbo la Kilombero - Abubakar Damian Asenga
  8. Jimbo la Ulanga - Salim Alaudin Hasham
  9. Jimbo la Malinyi - Mecktrids Fratern Mdaku
  10. Jimbo la Mvomero - Sarah Msafiri Ally
  11. Jimbo la Gairo - Ahmed Mabkhut Shabiby
 
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kilombero, mkoani Morogoro kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Abubakar Asenga amekuwa mgombea wa kwanza kupiga kura nchini, baada ya kupiga kura mapema leo, Jumatano Oktoba 29.2025 katika kituo cha shule ya msingi Madukani kata ya Ifaraka majira ya saa 01:03 asubuhi

Asenga ambaye anagombea kutetea kiti hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo anachuana na wenzake Saba kutoka vyama tofauti katika kinyang'anyiro hicho

Screenshot 2025-10-29 074817.png
 
Nipo ifakara. Mpaka sasa mwitikio ni mdogo sana. Vituo vingi wapiga kura hamna. Nimetembelea kituo cha shule ya msingi jongo watu hamna. Shule ya secondary techfort hali ni hiyohiyo. Shungu sekondary kidogo kulikuwa na watu kama 10.
Ofisi ya mtendaji wa kata nako hali sio nzuri.
Labda hali ibadilike baadae. Kama hali ikibaki hivyo itakuwa ni aibu kwa kweli.
 
Ikiwa zoezi la upigaji kura linaendelea kote nchini, Jambo TV imefika katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro, ili kujionea mwenendo wa zoezi hilo muhimu la kidemokrasia.

Wananchi waliohojiwa na Jambo TV wameeleza kuwa zoezi linaendelea kwa utulivu na amani, huku wakieleza kuridhishwa na maandalizi yaliyofanyika. Aidha, wametoa wito kwa wananchi wengine waliojiandikisha lakini bado hawajapiga kura, kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika mchakato huo ili kutimiza haki yao ya kikatiba.


Source Jambo TV
 
Back
Top Bottom