FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Mmh, kwani hiyo 250m ya mauzo ya nyumba, kwamba yote ni faida tu? Hiyo nyumba ilijengwa kwa gharam 0?!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtu mwenyewe Kibatala, hapa ana mgao 50% , Muulize AY na mwanaFADaaadekii, hapa Mtaalamu anapita na kika upenyo wa kupata pesa
KivipiHii michezo inachezwa na watu wa benki
Apewe hati yake akalale asigeuze hilo tatizo kuwa mtajiBenki ya biashara ya Akiba (ACB) imeburuzwa mahakamani na mteja wake, Aisha Abubakar Hassan baada ya hati yake ya nyumba aliyoiweka dhamana ya mkopo kupotea.
Kwa mujibu wa hati ya madai aliyofungua Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mfanyabiashara huyo wa vipodozi alichukua mkopo wa Sh30 milioni katika benki hiyo Novemba 4, 2021 kwa ajili ya kupanua biashara hiyo.
Ili kupata mkopo huo uliotakiwa kurejeshwa ndani ya miezi 18 kwa riba ya asilimia 1.5 kila mwezi, Aisha aliweka dhamana ya hati ya nyumba iliyoko kitalu namba 2136, bloku H, Tegeta, wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam.
Anadai kuwa alipomaliza mkopo huo Benki hiyo haikurejesha hati yake.
Baada ya kufuatilia mara kadhaa na kumwandikia barua mbili meneja wa tawi la benki hiyo bila mafanikio, kupitia wakili wake alitoa taarifa ya kusudio la kuchukua hatua za kisheria, ndipo baadaye benki hiyo ikamjibu kuwa hati hiyo imepotea.
Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na meneja wa mikopo, Charles Kamoto na mwanasheria wa benki hiyo, Niwaeli Mziray, benki hiyo ilisema imeomba nakala kutoka masjala ya ardhi ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo akiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala amefungua shauri hilo, akiiomba mahakama iiamuru benki hiyo imrejeshee hati ya nyumba yake.
Pia anaitaka benki hiyo imlipe jumla ya Sh355 milioni, kati ya hizo Sh250 milioni zikiwa ni fidia ya hasara ya kukosa biashara kutokana na benki kutokumpatia hati ya nyumba hiyo na hivyo kushindwa kuiuza kwa mteja aliyekuwa tayari kumlipa kiasi hicho.
Vilevile anaiomba mahakama hiyo iiamuru benki hiyo imlipe fidia ya Sh100 milioni kwa hasara ya kukosa kipato alichokuwa akikitarajia kutokana na biashara yake hiyo aliyokusudia kuipanua kwa kuongeza bidhaa.
Malipo mengine ni Sh5 milioni ikiwa ni hasara ya malipo ya awali aliyokuwa amelipa kwa mmiliki wa chumba cha biashara (fremu), katika Mtaa wa Mchikichini na Congo, Kariakoo, Dar es Salaam.
Pia anaiomba mahakama hiyo iiamuru benki hiyo imlipe fidia ya hasara ya jumla kwa kadiri itakavyotathmini, kwa kuendelea kushikilia hati yake wakati alishamaliza kurejesha mkopo na riba.
Vilevile anaomba riba ya asilimia 21 ya jumla ya malipo hayo yote ya fidia aliyoyataja, na riba ya asilimia ya kiwango cha mahakama kuanzia tarehe ya hukumu mpaka tarehe ya kumaliza malipo hayo na gharama za kesi.
Katika hati ya madai namba 199 ya mwaka 2023, mfanyabiashara huyo anayeagiza vipozi hivyo kutoka Uingereza, Uturuki na Marekani, na kuviuza katika duka lake lililoko Namanga, Oysterbay, anadai kwamba aliamua kuchukua mkopo kwenye taasisi nyingine ili kumaliza kulipa deni lililokuwa limesalia.
Anadai alifanya hivyo kwa matarajio kwamba akimaliza deni hilo atapewa hati yake ya nyumba ambayo alishaingia makubaliano na mteja kuinunua kwa Sh250 milioni, ambazo kati yake angetumia Sh200 milioni kupanua biashara yake kwa kuagiza bidhaa hizo.
Mfanyabiashara huyo anadai kuwa bidhaa hizo alitarajia kuziuza kwa bei ya rejareja na jumla kwa wateja wa ndani na nje katika kipindi cha sikukuu za mwisho na mwanzo wa mwaka 2023.
Hata hivyo anadai benki hiyo haikuweza kumrejeshea hati yake hiyo, jambo lililofanya biashara ya kuuza nyumba hiyo kukwama na pia kushindwa kurejesha mkopo aliouchukua katika taasisi nyingine kumaliza deni hilo, hivyo deni la mkopo huo kuendelea kukua na hasa riba.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Obadia Bwegoge imepangwa kutajwa Machi 23, kwa ajili ya kupanga utaratibu wa usikilizwaji wake.
Source: Gazeti la Mwananachi, Ijumaa March 3, 2023.
Uwezekano ndani ya benki kuna mtu ameichomoa ilipokuwa mchezo uchezwe wakishinda wanagawanaKivipi
Kwa nini unasema hivyo mkuu? Umewahi kupata usumbufu wa kuzungushwa na taasisi fulani? Kama ni kweli kuwa walipoteza hati yake halafu wakaanza kumzungusha, hadi baada ya kutishiwa kushtakiwa ndo wakamuandikia barua kuwa hati imepotea, sio fair kabisa mkuu. Kupotea kwa hati sio jambo la ajabu sana, ila walitakiwa ku handle vizuri swala zima. Cha kwanza, walitakiwa kumuita na kukaa nae mara tu bada ya kugundua kuwa wamepoteza hati yake, kisha kumwambia hatua ambazo wamechukua na wanaendelea kuzichukua kufanyia kazi suala lake.Dah, pesa inasakwa kwa kila njia,mwamba anaisakanya kinguvu[emoji23]
Inahusiana nini na anachokidai mkuu?alafu unaweza kuta ni mwamba huyo ni four two c tu..
Exactly..!!Sawa,wampatie hati yake basi
Ova
Ni uzembe kiukweli. Hivi taasisi kama hiyo tutaiamini vipi na pesa zetu? red flag kubwa sana aisee.Hati inapoteaje ikiwa bank?
Kwa nini unasema kuwa madai yake mengi hayana uhalisia?Madai yake mengi yanaonekana hayana uhalisia sema tu ni ushauri wa Kibatala,hata ingekuwa mimi ningetoa hoja hizohasa ningekazia kuhusu mteja kushindwa kununua nyumba....
Kwaida benki kupoteza hati?Haya mambo ni ya kawaida sana ila hiyu dada anatafuta pa kupigia hela. Kwa hiyo amepanga na Kibatala kuwakomoa Bank. .
Sio rahisi kihivyo aisee. Ni ka process fulani. Wanaweka process ngumu ili kuto encourage watu kupoteza hati kizembe zembe.Replacement si ni fasta tu kwa taasisi kama bank?