Mkopaji aishtaki Akiba Commercial Bank (ACB) kwa upotevu wa hati ya nyumba

Mkopaji aishtaki Akiba Commercial Bank (ACB) kwa upotevu wa hati ya nyumba

Akilipwa hiyo pesa...nimekaa pale..
Alafu nilitaka kushangaa dada kamalizaje deni hilo kirahisi hivyo, kumbe alikopa sehem nyingine....
kiufupi, dada kafirisika
Kwa nini bongo mtu akifuatilia haki yake anaonekana wa ajabu? Yaani bongo ukondoo unaonekana ndo kawaida. Daaahhh.
 
mbuzi kafia kwa muuza bucha.
Kwa kweli.
Ila kusema ukweli taasisi nyingi za bongo haziheshimu kabisa wateja wake. Na ni kwa sababu wanajua kuwa wabongo sisi wengi wetu ni makondoo, hatuna cha kuwafanya. Ukisoma hiyi habari, baada ya kuwa wamepoteza hiyo hati badala ya kumuita bidada na kukaa nae kumueleza ukweli na kumwambia hatua wanazochukua, kumuomba msamaha na kumuomba ushirikiano, wao waliamua kumzungusha weeee, hadi mteja kuwaandikia barua mara mbili, wao hawana habari. Hadi walipotishiwa kushitakiwa ndo wakakurupuka kumuandikia barua na kumwambia kuwa wamepoteza hati yake. Its not fair kabisa kwa kweli. Acha wanyooshwe tuu.
 
Halafu mteja wa nyumba unamrudisha wewe?

Umesoma hoja zake? Unaelewa maana ya damage?
Kaka, Watazania wengi wetu ni makondoo, mtu akifuatilia haki yake mguu kwa mguu kama hivi ndo anaonekana wa ajabu. Ila hizi taasisi nyingi za bongo zinasumbua sana wateja wake, kwa sababu wanajua sisi ni makondoo.
 
Kaka, Watazania wengi wetu ni makondoo, mtu akifuatilia haki yake mguu kwa mguu kama hivi ndo anaonekana wa ajabu. Ila hizi taasisi nyingi za bongo zinasumbua sana wateja wake, kwa sababu wanajua sisi ni makondoo.
Mwaka 2016 nililipia kifurushi Dstv kupitia tigo pesa ili nione match zote za world cup, guess what.. ile pesa ilikatwa kwenye akaunti lakini haikwenda Dstv.

Niligundua kuwa hazikwenda baada ya kuwasiliana na Dstv na wao kunitaka niwasiliane na tigo. Nilipiga simu sana tena sana tigo customer care, wanakili pesa kweli imekatwa na wanadai kulikua na hitilafu kwenye mifumo yao.

Kufupisha story ile pesa hadi navyoandika hapa sikuwahi kurudishiwa maana baadae ilibidi nilipe kwa mtandao mwingine huku nikiwasiliana nao, hadi kwenye maduka yao nilifika hakuna msaada zaidi ya itarudishwa baada ya saa 72. Naunga mkono hoja watoa huduma wengi wanapuuzia wateja na kuwadharau.

Ngoja hawa wanyooshwe mahakamani.

NB: audio ya mazungumzo kati yangu na wao ninayo.
 
Mwaka 2016 nililipia kifurushi Dstv kupitia tigo pesa ili nione match zote za world cup, guess what.. ile pesa ilikatwa kwenye akaunti lakini haikwenda Dstv.

Niligundua kuwa hazikwenda baada ya kuwasiliana na Dstv na wao kunitaka niwasiliane na tigo. Nilipiga simu sana tena sana tigo customer care, wanakili pesa kweli imekatwa na wanadai kulikua na hitilafu kwenye mifumo yao.

Kufupisha story ile pesa hadi navyoandika hapa sikuwahi kurudishiwa maana baadae ilibidi nilipe kwa mtandao mwingine huku nikiwasiliana nao, hadi kwenye maduka yao nilifika hakuna msaada zaidi ya itarudishwa baada ya saa 72. Naunga mkono hoja watoa huduma wengi wanapuuzia wateja na kuwadharau.

Ngoja hawa wanyooshwe mahakamani.

NB: audio ya mazungumzo kati yangu na wao ninayo.
Sisi ni makondoo mkuu, ndio maana taasisi nyingi zinatupotezea tu, kwa sababu wanajua hatutachukua hatua yoyote. Hebu angalia uwezekano wa kuonana na wakili mzuri kama Kibatala au anaefanana na huyo, umuelezee ishu yako na kumpatia vielelezo ulivyonavyo uone kama ni kesi ambayo inaweza kupelekwa mahakamani, andaa tu hela ya consultation ya mara ya kwanza, malipo mengine mnaelewana na kuingia makubaliano yatakatwa kwenye malipo ya ushindi wa keshi asilimia kadhaa kama mtashinda kesi, na kama mtashindwa pia mnakubaliana utampoza vipi.
 
Benki ya biashara ya Akiba (ACB) imeburuzwa mahakamani na mteja wake, Aisha Abubakar Hassan baada ya hati yake ya nyumba aliyoiweka dhamana ya mkopo kupotea.

Kwa mujibu wa hati ya madai aliyofungua Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mfanyabiashara huyo wa vipodozi alichukua mkopo wa Sh30 milioni katika benki hiyo Novemba 4, 2021 kwa ajili ya kupanua biashara hiyo.

Ili kupata mkopo huo uliotakiwa kurejeshwa ndani ya miezi 18 kwa riba ya asilimia 1.5 kila mwezi, Aisha aliweka dhamana ya hati ya nyumba iliyoko kitalu namba 2136, bloku H, Tegeta, wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam.
Anadai kuwa alipomaliza mkopo huo Benki hiyo haikurejesha hati yake.

Baada ya kufuatilia mara kadhaa na kumwandikia barua mbili meneja wa tawi la benki hiyo bila mafanikio, kupitia wakili wake alitoa taarifa ya kusudio la kuchukua hatua za kisheria, ndipo baadaye benki hiyo ikamjibu kuwa hati hiyo imepotea.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na meneja wa mikopo, Charles Kamoto na mwanasheria wa benki hiyo, Niwaeli Mziray, benki hiyo ilisema imeomba nakala kutoka masjala ya ardhi ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, mfanyabiashara huyo akiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala amefungua shauri hilo, akiiomba mahakama iiamuru benki hiyo imrejeshee hati ya nyumba yake.

Pia anaitaka benki hiyo imlipe jumla ya Sh355 milioni, kati ya hizo Sh250 milioni zikiwa ni fidia ya hasara ya kukosa biashara kutokana na benki kutokumpatia hati ya nyumba hiyo na hivyo kushindwa kuiuza kwa mteja aliyekuwa tayari kumlipa kiasi hicho.

Vilevile anaiomba mahakama hiyo iiamuru benki hiyo imlipe fidia ya Sh100 milioni kwa hasara ya kukosa kipato alichokuwa akikitarajia kutokana na biashara yake hiyo aliyokusudia kuipanua kwa kuongeza bidhaa.
Malipo mengine ni Sh5 milioni ikiwa ni hasara ya malipo ya awali aliyokuwa amelipa kwa mmiliki wa chumba cha biashara (fremu), katika Mtaa wa Mchikichini na Congo, Kariakoo, Dar es Salaam.

Pia anaiomba mahakama hiyo iiamuru benki hiyo imlipe fidia ya hasara ya jumla kwa kadiri itakavyotathmini, kwa kuendelea kushikilia hati yake wakati alishamaliza kurejesha mkopo na riba.

Vilevile anaomba riba ya asilimia 21 ya jumla ya malipo hayo yote ya fidia aliyoyataja, na riba ya asilimia ya kiwango cha mahakama kuanzia tarehe ya hukumu mpaka tarehe ya kumaliza malipo hayo na gharama za kesi.

Katika hati ya madai namba 199 ya mwaka 2023, mfanyabiashara huyo anayeagiza vipozi hivyo kutoka Uingereza, Uturuki na Marekani, na kuviuza katika duka lake lililoko Namanga, Oysterbay, anadai kwamba aliamua kuchukua mkopo kwenye taasisi nyingine ili kumaliza kulipa deni lililokuwa limesalia.

Anadai alifanya hivyo kwa matarajio kwamba akimaliza deni hilo atapewa hati yake ya nyumba ambayo alishaingia makubaliano na mteja kuinunua kwa Sh250 milioni, ambazo kati yake angetumia Sh200 milioni kupanua biashara yake kwa kuagiza bidhaa hizo.

Mfanyabiashara huyo anadai kuwa bidhaa hizo alitarajia kuziuza kwa bei ya rejareja na jumla kwa wateja wa ndani na nje katika kipindi cha sikukuu za mwisho na mwanzo wa mwaka 2023.

Hata hivyo anadai benki hiyo haikuweza kumrejeshea hati yake hiyo, jambo lililofanya biashara ya kuuza nyumba hiyo kukwama na pia kushindwa kurejesha mkopo aliouchukua katika taasisi nyingine kumaliza deni hilo, hivyo deni la mkopo huo kuendelea kukua na hasa riba.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Obadia Bwegoge imepangwa kutajwa Machi 23, kwa ajili ya kupanga utaratibu wa usikilizwaji wake.

Source: Gazeti la Mwananachi, Ijumaa March 3, 2023.

Kibatala? He he
 
Back
Top Bottom