Mkopaji aishtaki Akiba Commercial Bank (ACB) kwa upotevu wa hati ya nyumba

Apewe hati yake akalale asigeuze hilo tatizo kuwa mtaji
 
Dah, pesa inasakwa kwa kila njia,mwamba anaisakanya kinguvu[emoji23]
Kwa nini unasema hivyo mkuu? Umewahi kupata usumbufu wa kuzungushwa na taasisi fulani? Kama ni kweli kuwa walipoteza hati yake halafu wakaanza kumzungusha, hadi baada ya kutishiwa kushtakiwa ndo wakamuandikia barua kuwa hati imepotea, sio fair kabisa mkuu. Kupotea kwa hati sio jambo la ajabu sana, ila walitakiwa ku handle vizuri swala zima. Cha kwanza, walitakiwa kumuita na kukaa nae mara tu bada ya kugundua kuwa wamepoteza hati yake, kisha kumwambia hatua ambazo wamechukua na wanaendelea kuzichukua kufanyia kazi suala lake.
Itakua hujawahi kusumbuliwa mkuu, taasisi nyingi za bongo zina tabia ya "kuchukulia poa mambo" au kama kupotezea ishu za aina hii zinazomsumbua mteja. Ndio maana bongo hela yako inaweza kukatwa kimiujiza na benki, na ukifuatilia unaambiwa ni makosa, halafu hiyo hela kurudishwa inaweza chukua hata mwaka unafuatilia tuu, na they get away with that mara nyingi kwa sababu wabongo sis wengi wetu ni "makondoo" (samahani kwa kutumia neno hili). Yaani hatujui haki zetu. Ndio maana mtu akifuatilia haki yake kama hivi anaonekana kama analazimisha mambo.
 
Madai yake mengi yanaonekana hayana uhalisia sema tu ni ushauri wa Kibatala,hata ingekuwa mimi ningetoa hoja hizohasa ningekazia kuhusu mteja kushindwa kununua nyumba....
Kwa nini unasema kuwa madai yake mengi hayana uhalisia?
 
Haya mambo ni ya kawaida sana ila hiyu dada anatafuta pa kupigia hela. Kwa hiyo amepanga na Kibatala kuwakomoa Bank. .
Kwaida benki kupoteza hati?
Kawaida benki kutomwambia ukweli mteja wake kuwa wamepoteza hati yake na kumzungusha tu?
Wabongo wengi wetu ni makondoo sana. Mtu akifuatilia haki yake anaonekana complicator au mtafuta kiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…