1. Tatizo la wakopaji wa TANZANIA wamekwisha kuwa addicted na mikopo
2. Anakopa mkopo benki wa muda mrefu tena ni mfanyakazi na haachi nafasi ya dharura kwenye mshahara wake na baada ya muda anakwenda kwenye vikundi kule nako anaelemewa anakimbilia kwa wale watu binafsi ambao hata viwango vyao vya riba havipo dunia hii na hushikilia mpaka kadi za benki.
3. Akifika kwenye taasisi ya kukopesha yeye maswali yake ni mawili tuu NITAPATA KIASI GANI na NATAPATA LINI
4.Yale masharti yaliyopo kwenye mkataba wa mkopo kama riba kwa mwezi, ada ya mkopo, bima na processing fees haulizi wala hana muda huo na afisa mkopo hawezi kumwambia
5. Taasisi nyingi za kibepari zinazokopesha zinatumia deminishing method katika riba tuu na sio principal hivyo ukienda maamuma wakikuambia reducing method unaingia kichwa kichwa kumbe, wameweka mtego wanajua katika miaka yote 6 huwezi kuvumilia iishe bila kurudi kwao kuomba fedha tena..ndipo unaingia kwenye mtego uitwao TOP UP. Hapo tayari wanakuwa wameshavuna riba yao yoote inabaki pricipal wanakuweka tena kifungo kingine tena unakuta masharti ya riba yalishabadilika wee huna habari
6. Hapo bado hujamkatia afisa mikopo ili akufanyie fasta ukalipe furushi la madeni mengine unayodaiwa....hapo unaununua umaskini unajiona hivi hivi. Fanya tafiti kabla ya kukopa usisukumwe na shida zako..utajuta utakuwa unawafanyia kazi tuu hela yoote wanachukua