Mkopo NMB: Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Mkopo NMB: Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Status
Not open for further replies.
Mkopo NMB : Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Umaskini hauishi kamwe.

umekopa au umekopesha maana hapo kuku kazaa mbuzi.
yani nchi yetu inashindwa kitu kimoja kutambua mchango wa mwananchi kujenga nchi.hizi benki sio rafiki na sema sio rafiki hata ukiweka hesabu ya kikokotoo hapo hiyo asilimia yake ni kichekesho.
 
Haya ndio mambo ambayo serikaliya wanyonge ilipaswa kushughulika nayo maana yana athir moja kwa moja maisha ya raia wengi.
Sasa sijui katuroga nani mpaka tunashabikia ujinga tu.
 
Hayo mabank yaliambiwa yapunguze riba zao lakini kimya mpaka kesho..
 
Mkopo NMB : Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Umaskini hauishi kamwe.
Kama ni kweli unayosema, ulikopa bila kusoma vigezo na masharti? hukupiga hesabu kwamba utatakiwa kurudisha kiasi gani badae? kama ndivyo, basi UMASKINI umeukaribisha mwenyewe, na wajinga ndio waliwao.
 
Kabla sijaweka formula. Nikikuambia uchukue leo 500000tsh na nikikuambia nikupe hiohio 500000tsh baada ya miaka miwili. Utachukua ipi?
Mkuu unataka uingize siasa kwenye hesabu...wewe weka formula ndugu
 
1. Tatizo la wakopaji wa TANZANIA wamekwisha kuwa addicted na mikopo

2. Anakopa mkopo benki wa muda mrefu tena ni mfanyakazi na haachi nafasi ya dharura kwenye mshahara wake na baada ya muda anakwenda kwenye vikundi kule nako anaelemewa anakimbilia kwa wale watu binafsi ambao hata viwango vyao vya riba havipo dunia hii na hushikilia mpaka kadi za benki.

3. Akifika kwenye taasisi ya kukopesha yeye maswali yake ni mawili tuu NITAPATA KIASI GANI na NATAPATA LINI

4.Yale masharti yaliyopo kwenye mkataba wa mkopo kama riba kwa mwezi, ada ya mkopo, bima na processing fees haulizi wala hana muda huo na afisa mkopo hawezi kumwambia

5. Taasisi nyingi za kibepari zinazokopesha zinatumia deminishing method katika riba tuu na sio principal hivyo ukienda maamuma wakikuambia reducing method unaingia kichwa kichwa kumbe, wameweka mtego wanajua katika miaka yote 6 huwezi kuvumilia iishe bila kurudi kwao kuomba fedha tena..ndipo unaingia kwenye mtego uitwao TOP UP. Hapo tayari wanakuwa wameshavuna riba yao yoote inabaki pricipal wanakuweka tena kifungo kingine tena unakuta masharti ya riba yalishabadilika wee huna habari

6. Hapo bado hujamkatia afisa mikopo ili akufanyie fasta ukalipe furushi la madeni mengine unayodaiwa....hapo unaununua umaskini unajiona hivi hivi. Fanya tafiti kabla ya kukopa usisukumwe na shida zako..utajuta utakuwa unawafanyia kazi tuu hela yoote wanachukua
Mkuu naweza kuja inbox ukanieleza jambo?
 
Aya makato yabenk unapojiwekea muda mref kwa kujifariji kua utarejesha kdg kdg na hutasikia maumivu ndo unavyozid kuumia apo ungeamua kujilipua tu marejesho ya laki 3 na 50 ungejikuta unarejesha ata kwa miaka mi3 tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom