Mkopo NMB: Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Status
Not open for further replies.
Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya
Wewe hesabu ilikupita kushoto darasani popote ukiiona kimbia Sana utokomee..... Amekwambia anakatwa 250,000 kila mwezi sasa Kwa miezi 12 anakuwa amekatwa 21*250,000=3,000,000 hivyo ndani ya Miaka sita anakuwa amekatwa 18million
 
Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya
[emoji16][emoji16][emoji16]mwenyewe umeona umepatiaaa kumbe unajichora.
Kwani marejesho ni kwa kila mwaka ndo 250,000 au kila mwezi ndo 250,000
Kwa MIAKA 6?
 
Nyie ndio mnazinenepesha Benki zetu, ubarikiwe.
 
Kagenge kangu kakijaa jaa ntaenda nikope mkopo mkubwa nifanye mambo kwa muda wote huo wa miaka 6 mwee, ntakuwa na Msupa marketi ntaizungusha weee, ntaizunguusha wee , ntaizungushaa wee, et nmeskia mkoa jiran ukiingia shamba hata kwa laki 5 kulima ndondo waeza pata kadilio la Tsh1.8milllion miez 6 je mara 50% ya huo mhela afu wao uwanalipa mdogo mdogo, "Make Your Gold Multiply" rejea kitabu The Richest Man in Babylon, mabenki wanafanya hvyo kwako kwa pesa za watu nawe fanya hivyo kwa pesa zako au ukipenda nunua gari mkuu😀😀, nilianza na mafungu kumi ya nyanya sasa yamefika 30 naamin ipo sku ntadaka mnoti kama huo, kila la heri ndugu, Tchao Muuza ,Nyanya
 
Mkopo NMB : Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Umaskini hauishi kamwe.
Umasikini hauwezi kuisha ikiwa tutaukaribisha sisi wenyewe. Imagine umekopa hio 9 mil then ukaenda kununua ka Vitz au IST yako ili uvimbe mtaani lazima uumie kwa makato hayo from low salary scale mfano tu hio mil 9 ukanunua boda boda 3 na change ukaiweka kwa contigency unakuta hio laki 2 na nusu kwa mwezi sio Janga. Tu jiulize tunakopa Pesa kwa ajili ya kufanya nini? maana wakopeshaji nao wanataka pesa.

Kumi la pili linaelekea kuzuri sana
 
Mkuu unataka uingize siasa kwenye hesabu...wewe weka formula ndugu
Na wewe jibu ilo swali kwanza ili iwe rahisi kukufundisha io concept ukaielewa boss.

Formular zipo kibao boss ila nikiweka formular hapa bila kukupa background concept ni kaz bure
 
Mmhhh mbona km Unaibiw Crdb Mkopo M12.7 makato 259 miaka 7 inarudishwa My 21 ss ww iwe hvyo kapige hesabu vzr
====
Sijaona tofauti sana hapo. wewe umekopa milioni 12.7 unalipa 259,000/x 7 (yrs) x 12 (months)=21,756,000/= kweli wajinga ndio waliwao. Endeleeni kukopa bank.
 
Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya
Mkopo hulipwa kila mwezi so fanya hivi... 6x12x250,000 . siku nyingine ukufaham wewe mburura usikurupuke kujibu hasa kama inahusu namba.
 
Msipende kukopa kwa muda mrefu ndipo mnaona pesa nyingi sana. Ungekopa kwa mwaka mmoja ungerudisha kwa mwezi pesa nyingi lakini overal interest ingekuwa ni ndogo.
 
Mkopo NMB : Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Umaskini hauishi kamwe.

Pole sana hiyo ndiyo maana ya kurudisha na riba. Kabla ya kukopa hukusoma masharti na kupiga mahesabu?

Kutosoma mashariti ya mkataba na kupiga mahesabu kumewafilisi watu wengi sana.
 
Hili ndo tatizo letu wabongo,

Kampe muuza chipsi 5M aboreshe biashara zake kama hajakurudishia 400,000 kwa mwezi na hea yako bado ipo.
 
Na wewe jibu ilo swali kwanza ili iwe rahisi kukufundisha io concept ukaielewa boss.

Formular zipo kibao boss ila nikiweka formular hapa bila kukupa background concept ni kaz bure
Ndo mana nimekwambia acha siasa boss...kwa hiyo jibu langu litabadilisha iyo formula....weka formula....formula za hesabu huwa hazibadiliki we niwekee tu formula
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…