Mkopo wa MGODI wa Vodacom waweza kuwa changamoto kwa maskini

Sitaki kusikia huo ushuzi niliwah kukopa songesha hlf nikasahu ikapita miaka rukuki walivyo wajinga nikawa nikiweka hela hawakati kumbe wangese wamepeleta taarifa zangu credit info aaaah nikawa nafuatilia mamilion yng bank asee nilisota kinoma
 
Hivi wewe umeelewa kilichoandikwa na ulichoandika?? Au bhange?
 
Hivi wewe umeelewa kilichoandikwa na ulichoandika?? Au bhange?
Nadhani nina uelewa mzuri tu. Halafu si kuelewa nilichoandika hii ni mikopo ambayo tunaichukua kwenye simu zetu kila siku, kwa hiyo nina ufahamu mzuri wa ninachokisema.
 
Ingawaje Vodacom na mitandao mingine biashara yao ni mawasiliano, lakini naona kwa kiasi kikubwa waneingia katika biashara ya fedha. Napendekeza kuwa kiwe kitengo rasmi cha kujitegemea na mahesabu yao yawe yanachapishwa kwenye vyombo vya habari kama benki zingine. Riba ya kukopa na makato ya miamala ni makubwa mno hivyo ni wakati muafaka BOT waingilie kati.
 
Chief, vodacom hawafanyi biashara ya pesa hawana leseni hizo. Leseni yao ni ya mawasiliano. Walichonacho wao ni platform. Wanaofanya hizo biashara ni mabenki au taasisi za kifedha. Wameingia tu makubaliano na makampuni ya simu. Kwa hiyo wanawalipa gharama za kutumia platform zao.
 
Really? Kwa hiyo MPESA, Airtel Money etc. ni biashara za mabenki? Mfano, MPESA ni biashara ya benki ipi na kama ni ya benki kwa nini kusiwe na MPESA ya Voda, Airtel etc kwani ni benki moja inatumia platform za makampuni tofauti ya simu?
 
Mimi sijaona shida hapo tatizo labda hesabu tu.. ukiwa umeambiwa unakopeshwa elfu 81 na labda liba ni tsh 16000.. maana yake unapaswa kulipa elfu 97,000... sasa wanachofanya hao mgodi wao riba yao wanakata kabisa hivyo utapewa elfu 65000 then ukija kirudisha unarudisha elfu 81,000 ukijumlisha na hela waliyokata jumla ni elfu 97 ileile..

Labdankinachochanganya hapo ni namna ya utaratibu wao wa kuchukua riba yao mapema.
 
Hii mbona kali ila ni wajanja asee mi ndio nimegutuka leo ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„ kwenye 114,000 walinkopaga 90k kam kumbukumbu zko vzr ila uzuri sikuwalipa nilichukua hela nikalala mbele.
 
Really? Kwa hiyo MPESA, Airtel Money etc. ni biashara za mabenki? Mfano, MPESA ni biashara ya benki ipi na kama ni ya benki kwa nini kusiwe na MPESA ya Voda, Airtel etc kwani ni benki moja inatumia platform za makampuni tofauti ya simu?
Nilijibu swali lako haraka bila umakini. Hizi mobile money zote ni biashara za mitandao ya simu. Ila mikopo ndio biashara za mabenki. MPAWA, mgodi and the likes.
 
MPESA, TIGOPESA na AIRTELMONEY si biashara za benki. Hizi ni biashara za makampuni ya simu. Ila mikopo ndio bishara za benki. SijUI Mgodi, mpawa, tigi nivushe hizi ndio biashara za benki.
It's an eye opener to me. Mfano Nivushe ni benki gani ina operate. Na kama ni benk kwa nini kusiwe na Nivushe kwenye kila mtandao?
 
It's an eye opener to me. Mfano Nivushe ni benki gani ina operate. Na kama ni benk kwa nini kusiwe na Nivushe kwenye kila mtandao?
Mkopo wa nivushe ni wa Azania Bank, kuhusu hoja yako kuwa kwanini wasiweke kila mtandao jibu ni kwamba kila kampuni ya simu inaingia mkataba na benki wanayoitaka na wanayokubalina maslahi maana sheria haiwabani kwamba ni lazima waingie mkataba na benki fulani.
 
It's an eye opener to me. Mfano Nivushe ni benki gani ina operate. Na kama ni benk kwa nini kusiwe na Nivushe kwenye kila mtandao?
Tigo nivushe wanaoperate azania benk. Mpawa benk ya NCBA. Songesha TCB Bank. Mgodi Diamond Trust Bank. Bustisha ya tigo same Azania bank.

Hapo nafikiri ni ubunifu na biashara. Voda ana benk tatu anafanya nazo kazi kwenye product tofauti za mikopo.
 
Hii mbona kali ila ni wajanja asee mi ndio nimegutuka leo ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„ kwenye 114,000 walinkopaga 90k kam kumbukumbu zko vzr ila uzuri sikuwalipa nilichukua hela nikalala mbele.
Bosi hii itakuchafua. Ikitokea siku unataka mkopo mkubwa benki let say wa kazini hiyo laki unayodaiwa itafanya ukose huo mkopo. Ingwa wetu wetu huwa tunachukulia oya oya tu.
 
Najaribu kukuelewa, ila nashindwa, em fafanua kwa undani zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ