Mkopo wa MGODI wa Vodacom waweza kuwa changamoto kwa maskini

Mkopo wa MGODI wa Vodacom waweza kuwa changamoto kwa maskini

Wana Jamvi kuna Mkopo wengi wetu tulikuwa hatujui kuwa ni tatizo na ni kwa sababu ya kutokaa na kufikiria mara mbili. Nimefanya tafiti za riba kupitia watu 4 wanao chukua mikopo ya mtandao nikabaini mengi na mfano moja wapo ni huu, lazima kila mtu akae afikirie mara 2 kabla ya kuchukua mkopo wa mtandaoni.

Kwenye menu ya mpesa ya vodacom *150*00# ukichagua namba 5 ambayo ni Loans...halafu 3 ambayo ni MGODI... Hawa hutoza riba ya 50% ndani ya mwezi 1 kwa ujanja mkubwa sana ambao huwezi kushtuka na sio rahisi.

Mfano Mkopo wa sh 81,000 unaambiwa wanakata pesa zao ili ubaki na sh 64,000 wala hawasemi wanakata sh ngapi au ni % ngap kwa hizo wanazoita pesa zao. Ila wewe mkopaji utabaini wamekata sh 17,000 kwa mkopo huo wa sh 81,000, sasa badala ya kukueleza kwamba utalipa deni la sh 64,000 maana wameshachukua chao wao watakwambia unadaiwa sh 81,000 maana yake wanaendelea kukudai tena sh 17,000 walio kata hapo mwanzo. Sasa ukijumlisha sh 17,000 walio kata ili wakupe mkopo na hii ambayo imeingizwa tena ili ulipe mkopo ulio ainishwa kwa mara ya kwanza kama mkopo kamili utabaini unawalipa sh 34,000 kwa mkopo halisi ulio upokea wa sh 64,000. Kumbuka hata hiyo sh 64,000 ulio upokea bado kutoa utakatwa nyingine kama makato ya kutolea.

Taasisi za mikopo waliangalie hili swala. Kwanza wamsaidie mkopaji kisheria kama wanavyo tunga sheria pamoja na soko huria ya riba ili ukali wa makato kwa njia ya mtandao uzingatiwe kwenye kupunguza riba. Vinginevyo ni umaskini tu na ninchangamoto kwa maskini maana unaulipa ndani ya mwezi mmoja kwa riba ya 50%
Kuna kipindi nlikua nahitaji kuongez nguvu ya shilingi laki moja (100000) ili kukamilisha kilimo, jamaa ote wakaniruka hakuna aliejihusisha na mim kabisa, awamu ioiyofata nkachukua laki nne (400000) kimya kimya bila ku experience masimango ktoka kwa mtu yeyote, nkalipia shamba na pesa ya walimaji ikabaki.

Nlichojifunza, mgodi ni msaada kwangu, na ndo taasisi pekee sitaki kugombana nayo kwa namna yoyote vile,

Npo tyari niwalipe kidogo kidogo yaani effortlessly then nachukua parefu na kufanya jambo la kiuzalishaji
 
Najaribu kukuelewa, ila nashindwa, em fafanua kwa undani zaidi.
Kwa kifupi kinachofanyika ni kwamba riba ya mkopo wanachukua kabisa kabla ya kukupa mkopo wakati utaratibu uliozoeleka ni kuwa riba inalipwa kipindi unalipa deni.
Mfano rahisi; umekuja kwangu unataka mkopo wa laki moja nikakuambia riba yake ni elfu thelathini ukakubali. Maana yake unatakiwa kunilipa laki na thelathini. Mimi nakupa elfu sabini nakata kabisa riba yangu, ukilipa deni unalipa laki moja pekee kwa sababu riba nilishakata mwanzo.
 
Nadhani nina uelewa mzuri tu. Halafu si kuelewa nilichoandika hii ni mikopo ambayo tunaichukua kwenye simu zetu kila siku, kwa hiyo nina ufahamu mzuri wa ninachokisema.
Hakika Mkuu, niliku'challenge tu...

Pamoja Sana !!
 
hamieni Burundi daadeki zenu kila kona kausha damu na badoooooooooooooooooo mitano tena kwa Hangaya
 
Kwa kifupi kinachofanyika ni kwamba riba ya mkopo wanachukua kabisa kabla ya kukupa mkopo wakati utaratibu uliozoeleka ni kuwa riba inalipwa kipindi unalipa deni.
Mfano rahisi; umekuja kwangu unataka mkopo wa laki moja nikakuambia riba yake ni elfu thelathini ukakubali. Maana yake unatakiwa kunilipa laki na thelathini. Mimi nakupa elfu sabini nakata kabisa riba yangu, ukilipa deni unalipa laki moja pekee kwa sababu riba nilishakata mwanzo.
Mie nataka mkopo wa 100k na sio 70k. Ndo maana nashindwa kuelewa kabisa.

Huu ni utapeli.
 
Mpawa, Songesha, Mgodi na Timiza kwa airtel ni wa kuepuka haswa. Labda iwe ndio last resort, yani huna pakwenda.

Kuna saccoss, vikundi vya mitaani na Bank...nenda huko.
Kweli aiseee,bora kwenda kwa hawa wa mtaani maana hawa huhangaiki kuitoa

Maana hawa wa mtaani laki 1 unarudisha 120,000
 
A banker is a fellow who lends you his umbrella when the sun is shining, but wants it back the minute it begins to rain.

By the way Vodacom ni mediator tu nyuma yao kuna Taasisi za Benki
 
Sitaki kusikia huo ushuzi niliwah kukopa songesha hlf nikasahu ikapita miaka rukuki walivyo wajinga nikawa nikiweka hela hawakati kumbe wangese wamepeleta taarifa zangu credit info aaaah nikawa nafuatilia mamilion yng bank asee nilisota kinoma
Ulifanyaje asee mana ndo kinacĥonikuta sasa ivi nna deni wali write off ndo natakiwa nilipe.. ila nikitaka kulipa naambiwa sina deni lolote
 
We jamaa kuna sehemu huelewi hapo. Umesema alikopa 81,000 wakakata riba 17,000. Wamempa 64,000. Kwa hiyo jamaa yako amepoke 64,000 kwenye simu yake.

Kwa kifupi jamaa yako alikuwa hana hela akapata mkopo wa 64,000 kwenye simu. Sasa akirudisha 64,000 kampuni itakuwa imepata faida gani. Yaani apate 64,000 arudishe 64,000. Kampuni hamna ilichopata hapo.

Ili kampuni ipate inakuwa imempa 64,000 halafu sasa inamdai 81,000. Maana yake kapoke 64,000 kwenye simu ila wakati wa kurudisha anakuwa amerudisha 81,000. Hapo kammpuni inakuwa imepata 17,000 faida.

Hapo hakuna 17,000 mara mbili ni wewe tu haukuangalia vizuri. 17,000 inalipwa mara moja tu.
Mtu asipoelewa haya maelezo achana naye! Mtu analalamika kakatwa 17k , kakatwa from where wakati yeye hakuwa na pesa! Hiyo 17 uliyokatwa ni kama walijikata wao so wanaisubiri kutoka kwa mkopaji!
 
Back
Top Bottom