Mkopo wa MGODI wa Vodacom waweza kuwa changamoto kwa maskini

Kuna kipindi nlikua nahitaji kuongez nguvu ya shilingi laki moja (100000) ili kukamilisha kilimo, jamaa ote wakaniruka hakuna aliejihusisha na mim kabisa, awamu ioiyofata nkachukua laki nne (400000) kimya kimya bila ku experience masimango ktoka kwa mtu yeyote, nkalipia shamba na pesa ya walimaji ikabaki.

Nlichojifunza, mgodi ni msaada kwangu, na ndo taasisi pekee sitaki kugombana nayo kwa namna yoyote vile,

Npo tyari niwalipe kidogo kidogo yaani effortlessly then nachukua parefu na kufanya jambo la kiuzalishaji
 
Najaribu kukuelewa, ila nashindwa, em fafanua kwa undani zaidi.
Kwa kifupi kinachofanyika ni kwamba riba ya mkopo wanachukua kabisa kabla ya kukupa mkopo wakati utaratibu uliozoeleka ni kuwa riba inalipwa kipindi unalipa deni.
Mfano rahisi; umekuja kwangu unataka mkopo wa laki moja nikakuambia riba yake ni elfu thelathini ukakubali. Maana yake unatakiwa kunilipa laki na thelathini. Mimi nakupa elfu sabini nakata kabisa riba yangu, ukilipa deni unalipa laki moja pekee kwa sababu riba nilishakata mwanzo.
 
Nadhani nina uelewa mzuri tu. Halafu si kuelewa nilichoandika hii ni mikopo ambayo tunaichukua kwenye simu zetu kila siku, kwa hiyo nina ufahamu mzuri wa ninachokisema.
Hakika Mkuu, niliku'challenge tu...

Pamoja Sana !!
 
hamieni Burundi daadeki zenu kila kona kausha damu na badoooooooooooooooooo mitano tena kwa Hangaya
 
Mie nataka mkopo wa 100k na sio 70k. Ndo maana nashindwa kuelewa kabisa.

Huu ni utapeli.
 
Mpawa, Songesha, Mgodi na Timiza kwa airtel ni wa kuepuka haswa. Labda iwe ndio last resort, yani huna pakwenda.

Kuna saccoss, vikundi vya mitaani na Bank...nenda huko.
Kweli aiseee,bora kwenda kwa hawa wa mtaani maana hawa huhangaiki kuitoa

Maana hawa wa mtaani laki 1 unarudisha 120,000
 
A banker is a fellow who lends you his umbrella when the sun is shining, but wants it back the minute it begins to rain.

By the way Vodacom ni mediator tu nyuma yao kuna Taasisi za Benki
 
Sitaki kusikia huo ushuzi niliwah kukopa songesha hlf nikasahu ikapita miaka rukuki walivyo wajinga nikawa nikiweka hela hawakati kumbe wangese wamepeleta taarifa zangu credit info aaaah nikawa nafuatilia mamilion yng bank asee nilisota kinoma
Ulifanyaje asee mana ndo kinacĥonikuta sasa ivi nna deni wali write off ndo natakiwa nilipe.. ila nikitaka kulipa naambiwa sina deni lolote
 
Mtu asipoelewa haya maelezo achana naye! Mtu analalamika kakatwa 17k , kakatwa from where wakati yeye hakuwa na pesa! Hiyo 17 uliyokatwa ni kama walijikata wao so wanaisubiri kutoka kwa mkopaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…