Tetesi: MKT wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Kuanza Ziara ya Ulaya na US Kupitia Dubai 28/08/2016? !.

Anapiga mapushapu ya nini kama hajaribiwi, umewahi sikia wapi mtu mstarabua akapiga mipushapu mbele ya kadamunasi Lol!
Mkuu huo ustaarabu unaotaka wewe yeye hana na ameshatangaza kweupe kila mtu amemsikia kuwa yeye HAJARIBIWI sasa Mjaribu ili ukione kilicho mtoa Kanga Manyoya
 
Inawezekana Pasco siku hizi ushageuka kuwa muongo ila kwakuwa ni tetesi sitakuhukumu; labda niseme hili moja tu kwamba atakayetoka barabarani siku hiyo ni kwa hasara yake na familia yake. Upinzani wetu huu wa uchumia tumbo sio wa kuupa uhai wako au kiungo cha mwili wako; yet siasa ni mchezo mchafu ukiamua kuucheza lazima ujue utachafuka na kwa maana hiyo sijui kelele ni za nini kama uongozi unawamwagia tope, si hata wao wangekuwa madarakani wangeleta michezo michafu kuliko hata hiyo wanayoilalamikia? Hebu tuwape kijimda walioko madarakani wafanye klle walichoahidi wakishindwa si kila mtu atajua tu wameshindwa? na hapo si watageukia upinzani kwa point bila mashinikizo? wakati wote muda/wakati ni mwalimu mzuri
 
Tuambie basi hicho kibali cha kusafiri nchi za nje Mbowe alikiomba lini kwa Mungu wa Ikulu na lini kibali hicho kilitolewa!?
Kamanda hao waliotoa kibali ndio waliopenyeza habari hizo,na ndio maana serikali inajiamini kwa tambo zoote inajua wapi pa kuanzia
 
@WanaJamvi,

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe hana mpango wowote wa kufanya safari nje ya nchi siku za hivi karibuni

Katika Hotuba yake ya Leo kwa vyombo vya habari hapa Arusha ameeleza kuwa atakua mstari wa mbele kwenye mapambano kama ilivyo siku zote.
 
Kwa nini mtapigwa safari hii tena badly?

1. Mahakama kuu imetupilia mbali kesi yenu ya kudai haki ya kuandamana. Hivyo zuio la IJP ni sahihi hadi sasa.

2. Mahakama imewashauri kisheria kuwa, rufaa ikatwe na kuelekezwa kwa bosi wa IJP Mangu ambaye ni Lameck Mchemba Mwigulu ambaye ameishindilia juzi akiwa mtwara kuwa zuio hilo bado ni valid.

Sasa, mna grounds zipi za kulianzisha 1st Sep, 2016?

Mtapigwa tu, maana hakuna namna.
 
Hivi una kichaa?Huu ndio uthibitisho kuwa hatosafiri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…