Tetesi: MKT wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Kuanza Ziara ya Ulaya na US Kupitia Dubai 28/08/2016? !.

Tetesi: MKT wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Kuanza Ziara ya Ulaya na US Kupitia Dubai 28/08/2016? !.

Wazushi ndivyo walivyo, nadhani unakumbuka barua fake kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati ya maadili kwenda kwa Mbowe na Lissu iliyoandikwa na Buku 7.
Mpaka kitaeleweka tu dhidi ya huyu dikteta uchwara mwendo kasi.

Alutta continua! continua!

Kamanda hao waliotoa kibali ndio waliopenyeza habari hizo,na ndio maana serikali inajiamini kwa tambo zoote inajua wapi pa kuanzia
 
Wanabodi,

Naomba kuanza uzi huu kwa ku declare my interest kuwa Mimi Pasco wa JF, naunga mkono maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima na siku ya siku, nitajitokeza kushiriki na nitatoa wito wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, tujitokeze kwa wingi! .

Niko kwenye kijiwe fulani hapa mjini kati, jijini Dar es Salaam, nikainasa ndogondogo kuwa wakati chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, kiko kwenye maandalizi ya maandamano na mikutano nchi nzima kuhamasisha UKUTA, siku ya Tarehe 1 September 2016, habari ambazo hazijathibitishwa, zimeeleza kuwa, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe, yuko kwenye maandalizi ya mwisho mwisho kuanza ziara binafsi ya Ulaya na Marekani kupitia Dubai. Ziara hiyo umeelezwa kuwa pia itahusisha matibabu, uchunguzi wa afya na mapumziko mafupi mjini Dubai. Mtoaji wa taarifa hiyo isiyothibitishwa, imesema ziara hiyo ni binafsi, ya kifamilia na ya kibiashara.

Mtoa habari huyu alijitambulisha rasmi kama mkereketwa wa Chadema, na kutaja majina yake, lakini kufuatia habari hizi bado hazijathibitishwa rasmi na uongozi wa Chadema, naomba nisilitaje jina la mtoa habari wangu chini ya kinga ya kihabari iitwayo "the confidentiality of the source " mpaka habari hizi zitakapothibitishwa au kukanushwa.

Kufuatia source wa habari hii sio a trusted source ndio maana habari hii ina lebo ya tetesi, ikiishatibitishwa, neno tetesi litaondolewa! . Sii mara moja wala mbili kwa tetesi mbali mbali kushuka jf na baadae zikathibitishwa au kukanushwa! .

Hii sii mara ya kwanza kwa kiongozi Mkuu wa Chadema kuanzisha maandamano lakini siku ya siku haongozi harakati hizo na badala yake huwa safarini kikazi au kibinafsi hivyo kuwaachia wengine waliopo.

Lengo la kuileta habari hii humu jf hata kabla haijathibitishwa ili ile jf spirit ya "be the first to know! ".

Ikitokea ikathibitika habari hii sii ya kweli bali ni uzushi tuu, nitamuomba mode, asiufute uzi huu bali aufunge tuu kusubiria hiyo tarehe 1 September tuthibitishe this time around, Mwenyekiti atakuwepo kuongoza maandamano.

Lengo la kuomba uzi usifutwe bali ufungwe tuu, ni kufuatia posibility ya Chadema kuikanusha taarifa hii kuwa sii kweli lakini siku ya siku ikaelezwa Mwenyekiti amepata safari ya dharura.

Pasco.
Update 1.
Wanabodi
Post 110 nimepata uthibitisho toka kwa trusted source from Chadema Mkuu Ben Saanane.


Hivyo kwa ujumbe huu toka Ben Saanane, inawezekana tetesi hizi ni uzushi, wakati tukisubiria official response from Chadema office bearer na kusubiria kama Mwenyekiti atakuwepo mwenyewe physically hivyo, Tarehe 1 September .

Pasco
Pasco hauna tofauti na Dida wa 100.5 anzisha kazi kipindi chako cha kuchamba vinginevyo watadhani unavaa Madela.
 
Pasco ile habari yako ya kigogo mkubwa kutumbuliwa wiki kadhaa nyuma ilikufa kibudu... Naisubiria hii sasa ili niendelee kumjua Pasco wa JF, be 1st to know
 
Pasko katika ubora wake. Everyone has a price. Wengine ni vile tu bei zao hazijafika. But everyone has a price. Trust me.
 
Hii ndo tabia ya Mbowe hata kipindi cha Uchaguzi aliuza chama kwa Lowasa na wakati wa matokeo ya Uchaguzi alikimbilia marekani. Kinachomkimbiza nini? Kwanini asiairishe hadi tarege 1 sept ipite asije akasema hayakufanikiwa kwasababu hakuwepo
 
Achaa kiki zakishamba wakat kaenda ulaya amekuaga mbowe tunae hapa oficn sasa wala hana ratiba yakuondoka, skia nkuambie kama huna nakara yakuandika nakuomba kaakmya kbisaa usitudhalilishe kijana, nadhan umenisoma This last warning!
 
Back
Top Bottom