Mkude Simba SC imetosha, tafuta changamoto sehemu nyingine

Mkude Simba SC imetosha, tafuta changamoto sehemu nyingine

ToniXrated

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
1,134
Reaction score
2,993
Amani iwe kwenu.

Nimekuwa nikifuatilia sana mwenendo wa viungo wakabaji wa timu ya Simba SC kwa muda mrefu sasa. Nimeona mabadiliko makubwa kwa Mzamiru Yasin na Sadio Kanoute, viwango vyao vinakua siku baada ya siku ila inapokuja kwa mchezaji Jonas Gerald Mkude suala hili limekuwa ni tofauti. Mkude habadiliki kiuchezaji hata kidogo.

Ni mvivu kukaba na hupendelea kukaba kwa macho tu, kitendo ambacho kinampa mzigo wa ziada Mzamiru Yasin kwenda kusahihisha makosa ya Mkude.

Hakimbii uwanjani, ikumbukwe hakuna sehemu inahitaji mchezaji akimbie sana kama sehemu ya kiungo mkabaji. Kwa Mkude hali ni tofauti, sehemu ya kukimbia yeye ana jog (kimbia taratibu).

Mkude hana msaada katika timu linapokuja suala la kushambulia. Timu inasogea mbele kushambulia ila Mkude utamuona ametulia kwenye dimba kati kati ya kiwanja na hata akipewa pasi wakati timu inafanya shambulizi la kushtukiza, utamkuta anapiga pasi za upande au pasi za nyuma.

Mchezo huu wa derby dhidi ya Yanga amempa tabu sana Mzamiru katika kukaba tofauti na pale ambapo Mzamiru anapocheza na Putin Sadio Kanoute.

Mkude ni wakati sasa wa kuivua jezi ya Simba na kwenda kutafuta changamoto kwa timu za madaraja ya chini ambazo hazina uhitaji kubwa katika suala la uchezaji kama ilivyo kwa timu ya Simba.

Tunakushukuru kwa mchango wako katika kuitumikia timu na tunakutakia safari njema katika maisha yako mapya ya soka.
 
Dabi ya name hi jamaa anatafutiwa dabi ya. Kumi mwezako aandike history
 
Mkude haendi kokote! Bado yupo yipo sana pale msimba,i. Tumeshawazoea. Hivyo kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.
 
Sawa mkude mda umemtupa mkono ila mzamiru kwa mkude bado sana mzamiru kupiga pasi shida kukimbia shida sio ajabu mzamiru kupokonya mpira halafu akapoteza mda huo huo kwa kupiga pasi fyongo hyo hali ni tofauti na mkude ndo maana mzamiru anaitwa kuingo punda mkude anamapungufu yake ila sio kwa mzamiru maana wapo tofauti sana kiuchezaji
 
Ni mpuuzi tu ndiye anayeweza mfananisha mkude na mzamiru!!, Huyu mzamiru ambaye hata pass kupiga ni taabu?
 
Malalamiko FC A.K.A MBUMBUMBU FC au MAKOLOKOLO FC
emoji38.png
 
Mkude ana mechi zake, Sehemu ya kiungo ya Yanga imekamilika Kwa Leo Mkude mna mwonea. Ndio maaana kocha wa Simba katikati alipa acha akawa anapiga mipira mirefu(diagonal) Kwa Okra.

Alijua eneo la kati ya uwanja Yanga Wana mafundi, Ata Kipa Aishi Manula alikua akipiga mipira mirefu kitu ambacho si utamaduni wa Simba.

Simba walipotaka kucheza kupitia kati ya Uwanja Yanga wali win mipira mingi Sema Tusiila aliipoteza. Kama Kisinda angekua na Utulivu Angetengeneza nafasi za kutosha.
 
Wewe kama muda wote akiwa amelewa Pombe (Bia na Konyagi ) kuchanganya na Mpepe ( Bange ) anaypipenda hakuna mfano katika Machimbo yake ya Kawe, Juliana Pub na Kiarano Pub Goba husema kwa Sauti kuwa iwe isiwe ni lazima tu kabla hajatundika Daluga ( hajastaafu ) kucheza Soka ni lazima akaichezee Yanga SC ili Kumfurahisha Mama yake Mzazi ambaye ni mwana Yanga SC lia lia leo ulikuwa unategema jipya lolote labda kutoka Kwake?
 
Wewe kama muda wote akiwa amelewa Pombe ( Bia na Konyagi ) kuchanganya na Mpepe ( Bange ) anaypipenda hakuna mfano katika Machimbo yake ya Kawe, Juliana Pub na Kiarano Pub Goba husema kwa Sauti kuwa iwe isiwe ni lazima tu kabla hajatundika Daluga ( hajastaafu ) kucheza Soka ni lazima akaichezee Yanga SC ili Kumfurahisha Mama yake Mzazi ambaye ni mwana Yanga SC lia lia leo ulikuwa unategema jipya lolote labda kutoka Kwake?
Una ushahidi au unajilopokea tu
 
Sawa mkude mda umemtupa mkono ila mzamiru kwa mkude bado sana mzamiru kupiga pasi shida kukimbia shida sio ajabu mzamiru kupokonya mpira halafu akapoteza mda huo huo kwa kupiga pasi fyongo hyo hali ni tofauti na mkude ndo maana mzamiru anaitwa kuingo punda mkude anamapungufu yake ila sio kwa mzamiru maana wapo tofauti sana kiuchezaji
Wewe sio mfuatiliaji wa mechi za simba toka Mgunda akabidhiwe timu
 
Mkude anachoweza ni passing tena square pass,hajui kukaba hana mbio na hajui awe wapi kwa wakati gani.Mzamiru work rate yake ni nzuri sana ila passing yake ndio tatizo

Back
Top Bottom