Mkude Simba SC imetosha, tafuta changamoto sehemu nyingine

Mkude Simba SC imetosha, tafuta changamoto sehemu nyingine

Ninacho sisitiza ni Kamati ya saa sabininambili ichukue hatua za kinidhamu dhidi ya Chama Kwa tukio la (unsports man faul) dhidi ya Aucho. Kama alivyo fanyiwa Morrison hatutegemei tukio kama Lile lisichukuliwe hatua Kwa muda husika.
 
Wewe sio mfuatiliaji wa mechi za simba toka Mgunda akabidhiwe timu
Mzamiru ni kiungo asiye na faida ni vile tu Tanzania hatuna match analyst mechi ya kigoma ya ngao ya jamii ile ya kigoma alikaba akapata mpira halafu akapiga pasi fyongo akampa feisal na ndo lilikuwa goli pekee kwenye mechi ile kama kiungo anapokonya mipira halafu anapiga pasi fyongo sasa ana faida gani kwenye team mkude na mzamiru ni mbingu na ardhi ndo maana wanamwita kiungo punda.
 
Unamuongelea mzamiru wa zamani...the guy toka mgunda achukue timu amebadilika sana labda kama hufuatilii mechi za simba
 
Amani iwe kwenu.

Nimekuwa nikifuatilia sana mwenendo wa viungo wakabaji wa timu ya Simba SC kwa muda mrefu sasa. Nimeona mabadiliko makubwa kwa Mzamiru Yasin na Sadio Kanoute, viwango vyao vinakua siku baada ya siku ila inapokuja kwa mchezaji Jonas Gerald Mkude suala hili limekuwa ni tofauti. Mkude habadiliki kiuchezaji hata kidogo.

Ni mvivu kukaba na hupendelea kukaba kwa macho tu, kitendo ambacho kinampa mzigo wa ziada Mzamiru Yasin kwenda kusahihisha makosa ya Mkude.

Hakimbii uwanjani, ikumbukwe hakuna sehemu inahitaji mchezaji akimbie sana kama sehemu ya kiungo mkabaji. Kwa Mkude hali ni tofauti, sehemu ya kukimbia yeye ana jog (kimbia taratibu).

Mkude hana msaada katika timu linapokuja suala la kushambulia. Timu inasogea mbele kushambulia ila Mkude utamuona ametulia kwenye dimba kati kati ya kiwanja na hata akipewa pasi wakati timu inafanya shambulizi la kushtukiza, utamkuta anapiga pasi za upande au pasi za nyuma.

Mchezo huu wa derby dhidi ya Yanga amempa tabu sana Mzamiru katika kukaba tofauti na pale ambapo Mzamiru anapocheza na Putin Sadio Kanoute.

Mkude ni wakati sasa wa kuivua jezi ya Simba na kwenda kutafuta changamoto kwa timu za madaraja ya chini ambazo hazina uhitaji kubwa katika suala la uchezaji kama ilivyo kwa timu ya Simba.

Tunakushukuru kwa mchango wako katika kuitumikia timu na tunakutakia safari njema katika maisha yako mapya ya soka.
mkude hawezi kuishi na kufanya akzi nje ya simba
IVI WALISHAMPIMA AKILI?
 
Back
Top Bottom