Mkulima mbaroni kwa kumvunjia heshima Rais Samia na Dkt. Kikwete mtandaoni

MKAZI wa Kidete mkoani Morogoro anayejishughulisha na kilimo,Piniston Nzali (20) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu ya kuchapisha mtandaoni taarifa yenye kuharibu hadhi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Piniston pia antuhumiwa kwa kosa la kushindwa kusajili laini ya simu iliyokuwa ikimilikiwa na mtu mwingine.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Sylivia mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Luboroga imedaiwa, Oktoba 8, 2022 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mshtakiwa alichapisha taarifa yenye kuharibu heshima au hadhi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Aidha, katika taarifa hiyo inadaiwa, mshtakiwa kupitia mtandao wa Tiktok alichapisha video inayomuonesha Rais Samia akiimba jambo ambalo halikuwa la kweli.

Mshtakiwa pia anadaiwa kuchapisha taarifa inayofanana na hiyo ikimuonesha Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiimba kosa alilolitenda Oktoba 10, 2022 huku akijua kuwa jambo hilo halina ukweli.

Katika shtaka la mwisho, inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba Mosi, 2022 na Oktoba 20, 2022 mshtakiwa alitumia laini ya simu ambayo awali ilikuwa inamilikiwa na Benjamani Chaji bila kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki kwa mtoa huduma.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka hayo na amerudishwa mahabusu mpaka kesho kesi hiyo itakapotajwa kwa ajili ya kueleza hatua za upelelezi ulipofikia.

View attachment 2412715
Kama shahidi ni jamhuri AMEKWISHA
 
Nadhani ile ilikuwa kama kibonzo tu,kweli serikali inaacha kushughulika na mambo ya msingi kama mfumuko wa bei,ukosefu wa maji na umeme nk,haya mambo mengine ni kuzidi kupoteza rasilimali za serikali tu
 
Niliiogopa ile video kama ukoma.

Nilivooneshwa tu nikajua lazima kuna jitu laenda nyea debe.

Watu hawajifunzi tu aisee.

Ila kavideo kanachekesha sana aisee, mama anachezesha mpaka nyusi kusikilizia mdundo.
 
ACHAPWE VIBOKO 30 KILA WIKI DOZI YA MIEZI 3.
Itamtosha sana.
Viboko vya kiasikari 480 tosha kabisa.
 
MKAZI wa Kidete mkoani Morogoro anayejishughulisha na kilimo,Piniston Nzali (20) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu ya kuchapisha mtandaoni taarifa yenye kuharibu hadhi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Piniston pia antuhumiwa kwa kosa la kushindwa kusajili laini ya simu iliyokuwa ikimilikiwa na mtu mwingine.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Sylivia mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Luboroga imedaiwa, Oktoba 8, 2022 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mshtakiwa alichapisha taarifa yenye kuharibu heshima au hadhi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Aidha, katika taarifa hiyo inadaiwa, mshtakiwa kupitia mtandao wa Tiktok alichapisha video inayomuonesha Rais Samia akiimba jambo ambalo halikuwa la kweli.

Mshtakiwa pia anadaiwa kuchapisha taarifa inayofanana na hiyo ikimuonesha Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiimba kosa alilolitenda Oktoba 10, 2022 huku akijua kuwa jambo hilo halina ukweli.

Katika shtaka la mwisho, inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba Mosi, 2022 na Oktoba 20, 2022 mshtakiwa alitumia laini ya simu ambayo awali ilikuwa inamilikiwa na Benjamani Chaji bila kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki kwa mtoa huduma.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka hayo na amerudishwa mahabusu mpaka kesho kesi hiyo itakapotajwa kwa ajili ya kueleza hatua za upelelezi ulipofikia.

View attachment 2412715
Hawa vijana wahuni wanaotumika wakihukumiwa wapelekwe mashambani huko JKT mbona watanyooka badala ya kuwarundika magerezani wanakuka bure..

Binafsi sikubaliani na mtizamo wa Rais Samia wa kuwakataza magereza na JKT kujishughulisha na Mambo ya uzalishaji Mali kwa kisinhizio eti wanaacha jukumu lao la msingi.
 
Kutumia jina la MamaSamia2025 haimaanishi mimi ni mama. Namaanisha Mama Samia tena 2025. Hili ni jina ambalo liko mbele ya muda. Kuhusu kijana aliyedakwa ingekuwa vema CHADEMA na wale wanaharakati wakamtetea. Vilevile wengine watajifunza kati ya uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kutukana/kudhalilisha.
Angalia emoji Zina display hakuna userious kwenye andiko.
 
Huyu sijui atakuwa mtu wa ngapi kufikishwa mahakamani kwa tuhuma kama hizi!!!!

Hivi shida ni nini; ni sisi wananchi, mamlaka au sheria?
 
Ujue kofuri aliharibu uwezo wa watanzania wa kufikiri? Huyu kijana ana tofauti gani na wachora katuni? Mbona JK alitaniwa sana na haikuwa ishu? Ujing mtupu hawa viongozi wa awamu hizi na nyota mnaoungana nao!
 
Back
Top Bottom