Mkulima mbaroni kwa kumvunjia heshima Rais Samia na Dkt. Kikwete mtandaoni

Mkulima mbaroni kwa kumvunjia heshima Rais Samia na Dkt. Kikwete mtandaoni

MKAZI wa Kidete mkoani Morogoro anayejishughulisha na kilimo,Piniston Nzali (20) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu ya kuchapisha mtandaoni taarifa yenye kuharibu hadhi ya Rais wa sha Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiimba kosa alilolitenda Oktoba 10, 2022 huku akijua kuwa jambo hilo halina ukweli.

Katika shtaka la mwisho, inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba Mosi, 2022 na Oktoba 20, 2022 mshtakiwa alitumia laini ya simu ambayo awali ilikuwa inamilikiwa na Benjamani Chaji bila kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki kwa mtoa huduma.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka hayo na amerudishwa mahabusu mpaka kesho kesi hiyo itakapotajwa kwa ajili ya kueleza hatua za upelelezi ulipofikia.

View attachment 2412715
Daaa, sasa faida ya hayo aliyofanya ni nini?
 
Ni ujinga tu.

Watu wanakwapua mabilioni, ripoti za cag zimejaa madudu wanakenuliana meno.
 
Tupo busy kukamata watu mitandaoni badala ya kukaa kama kwa pamoja tujadili jinsi ya kukabiliana na majanga maana yapo...hizi drama za kitoto zikiendelea hatutaacha kutumia kamba za kufungia mbuzi kuzitumia kwenye majanga badala ya kuwa na Wazamiaji kwenye kina kirefu...
 
Hizo pesa za kuhangaika na watu hawa minor wangezipeleka VETA au kule wanakopeleka TOZO zetu hence kutupunguzia TOZO huenda badala ya kutumia nguvu kuziba midomo kwa wanaomuona Mtawala kwa jicho la ku-criticise wangemuona vinginevyo..., hence wasingehangaika kuziba watu midomo...

Hivi wale kila siku wanaojaza humu nyuzi kwamba anaupiga mwingi sio wapotoshaji pia hence wafunguliwe mashitaka !!!

Huenda huyo Mkulima alishikwa na msongo wa mawazo hence kuchanganyikiwa kutokana na bei ya mbolea kuwa juu... Na sisi walaji sijui tumekosa mazao kilo ngapi kwa kupoteza hii nguvu kazi...
sawa mzee wa "hence"
 
Back
Top Bottom