Mkulima wa nyanya usitupe nyanya zako zilizo kosa soko fanya hivi kuziongezea thamani

Huwezi kupata soko la unga wa tomato,bora tomato paste
Mtoa mada ana idea za vitabuni. Hamna mtu atanunua unga wakati fresh tomatoes zipo na kwa bei affordable

Hata hao jamaa nilioeleza hapo kwenye post yangu iliyotangulia walifeli sababu demand ya hiyo powder ni almost nothing

Labda kama unahifadhi kwa matumizi yako tu
 
Nimekuelewa vizuri Mkuu
 
Shida ni market promo hakuna,soko always lipo.
Soko haliwezi ishinda idea.
Mimi nataka nianze kuzalisha viazi vya kupikwa then vinakaushwa kwa dar ni ngeni lakini shinyanga,Mwanza tabora ni kitu Cha kawaida
 
Hili ni wazo zuri,swali ni kuwa je ukiuza hiyo Tomatoe powder itanunulika...?
Ni bidhaa mpya kwa wengi, unaweza ukalazimisha soko anza na kwa mama lishe,mahotelini,nk.
Mbona Bakhresa anauza Nazi ya paketi
 
Biashara ni pamoja na kuangalia wenzio wameshindwa wapi ,hao walifeli pengine labda kwenye masoko nadhan ukiwekwa mkakati mzuri unaweza kuvuka mbele zaidi ya waliko inshia wao.
Mtanzania anaangalia Bei nafuu na Sio ubora thus mchina kaijua Siri hii anavuna utajiri Africa
 
kula tano mjomba!!!
 
Mtanzania anaangalia quantity na low price hizo factors zingine ni za masaki huko.
Na market kubwa yenye pesa ipo uswahilini.
 
Ni idea nzuri sana hii.
Matunda yote yanakaushwa hata ikiwemo embe muhimu usafi tu na vikinga nzi tu wakati unaanika.
Tumia solar dry yaani vichanja vyenye ngazi kisha Hilo banda lifunike na wavu wa mbu kuzuia nzi kwa maeneo yasiyo na vumbi.
Zipo mashine za kukaushia matunda kwa sehemu za baridi.
 
Kama ndimu,chungwa,papai,embe nanasi yanakaushwa na unauza powder yake sembuse nyanya.
Ukichukua unga wa embe,papai,nanasi,chungwa nk ukitaka kutumia unauloweka kwenye maji unapata ladha halisi ya tunda husika
 
Shida ni market promo hakuna,soko always lipo.
Soko haliwezi ishinda idea.
Mimi nataka nianze kuzalisha viazi vya kupikwa then vinakaushwa kwa dar ni ngeni lakini shinyanga,Mwanza tabora ni kitu Cha kawaida
Swali ni kua bei yako baada ya kufanya hiyo process yote je inaweza kua chini ya bei ya fresh tomatoes [emoji534]
 
Biashara asili yake ni idea za vitabuni (mawazo ya watu) huwezi kusema hakuna mtu atakaye nunua tomato powder kwasababu tomatoes fresh zipo na hujawai ku practice Wala kufanya research zaidi kuwaona watu fulani wanefeli tena bila kujua Sababu nini.

Tomato inategeneza products nyingi na zote zina soko lake kwa namna yake kama ingalikuwa kama usemavyo basi hizo bidhaa zisingefanya vizuri sokoni kwasababu tomato fresh zipo kwa wingi.
 
Swali ni kua bei yako baada ya kufanya hiyo process yote je inaweza kua chini ya bei ya fresh tomatoes [emoji534]
Siku zote gharama ya bidhaa inapangwa kulingana na upatikanaji wake, operation cost yake na packaging.

Upatikanaji wa nyanya hasa kwa msimu wa mavuno ni mwepesi na kwa bei rahis, pia package na utengenezaji wake rahis.so sidhani kama bei inaweza kuwa juu sana

Ila kumbuka mkuu hii ni value addition of tomato sasa kitu kikishaongezewa thamani hakiwezi kuwa sawa kama kilivyo awali, hata hizi tomato paste &chill bei zake zipo juu kulinganisha fresh.
 
Kama ndimu,chungwa,papai,embe nanasi yanakaushwa na unauza powder yake sembuse nyanya.
Ukichukua unga wa embe,papai,nanasi,chungwa nk ukitaka kutumia unauloweka kwenye maji unapata ladha halisi ya tunda husika
Kila kitu kilianza kigeni promotion ndio inayotambulisha bidhaa ,yani mtu kwasababu hajawai kutumia au kuona bidhaa fulani basi anaamini hakiwezekani huku kukutatisha watu tamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…