Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nawajua Wabongo ndio maana nikakuambia hivyoKichanja hakina gharama mkuu ukizingatia upatikanaji wa meterial ni mwepesi na bei nafuu,ni kazi ambayo unaweza kuifanya hata mwenyewe bila kumlipa mtu au kama utakosa muda wa kufanya cost yake still ni ndogo .
Labda kama hayuko interested lakini ni Njia nzuri sana ya kuongeza thaman yanya zako
WhyKuna mashine ya drier hiyo ukiwa nayo unaweza win, lakini ukisema utegemee mwangaza wa jua kufail no 100%
Wazo zuri sana mkuu hilo, tena siyo lazima tusubiri zinatzotaka kuharibila unaweza kufanya hivyo wakati wa mavuno mengi. Kwa kukuongezea tu wakulima wanaweza kuungana wakatengeneza solar drier kama hii hapa kwenye picha zikakauka kwa ubora wa juu kabisa bila kupoteza viinilishe vyake.Wakulima wengi wa nyanya wanapata hasara kutokana na kuzalisha nyanya ambazo zimezidi mahitaji ya soko au Sababu nyingine ni uhaba wa masoko ,Kiasi kikubwa cha nyanya zinaoza shambani au sokoni ni kwa sababu wakulima wengi hawana/hawajui jinsi ya kuhifadhi nyanya zao
Kwa utafiti wangu usio rasmi nimebaini Wakulima wengi wanapoteza zaidi ya nusu ya nyanya zinazozalishwa.
Hasara kubwa wanaipata Kipindi Cha msimu wa mavuno , nyanya nyingi zinaharibika kwa kusubiri wanunuzi na zingine zinaharibika tu kutokana asili ya zao lenyewe lilivyo(laini) hivyo inawalazimu wakulima wengi kuuza kwa bei ya hasara wengine wanazitupa kabisa kwa kukosa wateja.
Sasa Njia nzuri ya kuzihifadhi na kuongeza thamani nyanya zako zilizoharibika (sio kuoza) na ambazo zimekosa soko ni kuzifanya kuwa unga (tomato powder).
Njia hii ni nyepesi Wala haiitaji gharama kubwa , unachotakiwa kufanya unazikatakata nyanya zako kisha unazianiaka juani, baada ya kukauka utazisaga kwa blenda au kwa kutumia kifaa chochote ilimradi iwe unga
kutengeneza tomatoe powder inasaidia kupunguza upotevu wa nyanya baada ya mavuno lakini pia inasaidia kendelea kutumia nyanya nyakati za uhaba wa nyanya,
hivyo ni wazo Bora pia ukiamua kufanya kibiashara , na uzuri ni kwamba tomato powder ikihifadhiwa vizuri inakaa kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita kwahiyo kazi kwako mkulima ulifanye kuwa wazo kamili au ulitume pindi nyanya zikishindwa kutoka sokoni.
View attachment 2734709
![]()