KERO Mkurugenzi Garda World jitafakari, wafanyakazi tumekuchoka

KERO Mkurugenzi Garda World jitafakari, wafanyakazi tumekuchoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ndio kajirekodi kachomeka flash yeye kaenda kuendelea kula Hela zao za mafao hana muda wa kukaa kuwasikiliza wanampotezea muda wa kuzitumbua Hela zao
Mtanzania akipewa nafasi ya kusimamia sehemu fulani huwa anataka wale waliochini yake waishi kama wako motoni furaha ni kuona wakiteseka na kunyenyekea na siyo kuwapa stahiki zao
 
Mtanzania akipewa nafasi ya kusimamia sehemu fulani huwa anataka wale waliochini yake waishi kama wako motoni furaha ni kuona wakiteseka na kunyenyekea na siyo kuwapa stahiki zao
Mzungu anakuja anasema Hawa nitawalipa kimataifa km wanavyolipwa walinzi wa Canada mbongo aliepewa rungu anawakandamiza anamwambia Mzungu hapa sio Canada Hawa usiwalipe km watu wa Canada walipe km Watu wasio na umuhimu wowote Mzungu anasema ebu tuone mbinu yake sasa mbinu anayoitumia mbongo ndio hio kuwakimbia Wafanyakazi hawasikilizi Wafanyakazi sababu anajua anawaibia haki zao na stahiki zao
 
Ulipotaja neno KELO nikasikitisha kusoma hapo hapo.
images (17).jpeg
 
Mkuu kwa hayo mawenge utatoboa kweli? Alafu ule mkopo ulichukua ni kama umejifunga mpaka umalize.
na sikushauli mkuu unadhalilika sana haifai ww unang'atwa na mbu usiku kucha ila ukienda kw mwajiri wako hata kubadili nguo tu unasimangwa sana Yani unajiona sio binadamu inafika kipindi hata ule uanamme inapotea Kwa hofu .
 
Mzee kampuni imeuzwa mnataka kulipwa mlikua shareholders? Yani ni kama unauza duka halafu Boss wako kafilisika kauza utamdai muuzaji au mnunuaji akulipe share ya mauzo ? Kama hukua shareholder endelea kulinda mzee na ushkuru mnunuaji kaendelea nawewe hajataka kuingiza watu wake anaowaamini.
 
Mzee kampuni imeuzwa mnataka kulipwa mlikua shareholders? Kama hukua shareholder endelea kulinda mzee siku akili ikifunguka kuwa ulinzi si kazi utaenda kushona hata viatu na mkeo atakuheshimu kuliko ulinzi.
lala tu mzee Kwa uandishi huu🌈 maana umejaa zarau nyingi na huna point zaidi ya kejeli
 
Hawa Gardaworld walianza kwa mbwembwe sana. Sasa hivi biashara yao imeshuka. Wamepoteza malindo mengi sana, kwa Sumajkt Guard, G4S, SGA. Hii chengachenga ya kukutana na wafanyakazi inaonyesha jinsi gani wanapitia wakati magumu kimapato. Walinzi wa kawaida wabeba virungu na kupigwa na baridi hawawezi kujua hili. Sisi tulioko kwenye mfumo ndio tunajua🤔
 
Back
Top Bottom