KERO Mkurugenzi Manispaa ya Moshi awalazimisha watumishi kufyeka na kusafisha makaburi ya Karanga siku za mapumziko

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kodi zao zinafanya kazi gani?
 
Hiyo yote Kwa sababu Walimu hamna vitega uchumi vya kuingizia kipato mbali na mshahara ila mkiwanavyo hata ukiambiwa Leo kazi basi unaendelea na maisha Yako mtu pekee wa kumuogopa ni mungu mgawa riziki msiende kama kwel mnajielewa
 
Nyie ndiyo mnawaendekeza watu wa aina hiyo. Tatizo nako hamjuwi haki zenu na utaratibu za kazi. Kusafisha makaburi wapi na wapi na kazi yako. Mgomeeni asiwapelekeshe kama ni mwanamke wapeleke mke wake na watoto wake wakasafishe na kama ni mwanamke ampeleke muwe na watoto wake wakafanye hiyo kazi.
 
Na yeye huwa anashiriki au ni nyie walimu tu?
 
Watumishi wote.....sio waalimu Peke yao. Soma vizuri tangazo acha mihemko
 
Watanzania tunanyanyaswa sana hapo angerafuta hela yeyote atafute watu wakafanye huo usafi yeye kaamua kuvamia Walimu mbona watumishi wapo wengi si angevamia kada nyingine aone majibu yake...
 
daah amakweli tamisemi kuna miungu watu. unamwamrisha mbaba au mmama wa watu akakwae makaburi ya watu hata hawajui tena wikendi? na si ajabu yeye hajawahi hata kukwaa kaburi la mzazi wake.
 
Kwa mtumishi kugomea elekezo la anayepitisha barua zako ni changamoto kubwa sana.Huyo ni afisa nidhamu wako hivyo ataamuru usumbuliwe,usimamishwe,uundiwe kamati nk,mpaka uje kuonekana ulionewa umeshateseka sana na familia yako.Na ngazi za juu zina mambo mengi mpaka zije kutetea jambo lako miaka imeenda,umepigika na kudhalilika ipasavyo;na kwa ufinyu wa muda wanaweza kukutoa mhanga ili maisha yawe rahisi.Hivyo inabidi akili itulie na zaidi ujishushe na kupotezea ili mambo yaende.
 
Hivi Mkurugenzi mzima anashindwa kuomba Magereza wafungwa wafanye huo usafi?

Na kuna wenye vifungo vya nje hizo ndio kazi wanapaswa kuzifanya.

Majitu ya ccm bure kabisa.
 
Kiongozi hana mamlaka yoyote ya kumtuma mwananchi au mtumishi wa umma kazi zilizo nje ya wajibu wake professionally let alone legitimately. Inavyoonekana huko mliko ni kijijini na huyo kiongozi ni mshamba na uncivilized savage anayedhani uongozi wa democracy unampa nguvu za kifalme za kuamua chochote. Na kwa bahati nzuri amekutana na washamba, waoga, wasiotambua haki wala wajibu wao.

Huyo mpuuzi asiyekuwa na akili angekutana na mimi angeacha huo upuuzi mara na asingenifanya chochote. Damn, ningeinjoy hilo kesi!

Embu acheni uoga nyie walimu na mjikusanye mu-question hako ka-modern day savage barbarian kuhusu credibility na legitimacy ya hilo agizo lake la kimbavu na relation yake na kazi, haki na wajibu wenu.

Akileta ubishi na nyie leteni ubishi, sababu technically hana chochote cha kuwafanya zaidi ya kuwatisha tu sababu anajua nyie ni waoga msiojitambua.
 
Hii ndio maana ya uoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…