TANZIA Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda afariki Dunia nchini Afrika Kusini

TANZIA Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda afariki Dunia nchini Afrika Kusini

Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Apson Mwang’onda (75), amefariki dunia leo Oktoba 7, nchini Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa, familia yake imethibitisha.

View attachment 1226052
Rais Magufuli akimjulia hali Apson Mwang'onda hospitalini enzi za uhai wake
Pia soma
Asiyejulikana kakutana na asiyejulikana mkuu ibilisi shetani, mungu (SIO Mungu) amlaze anapostahili
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda amefariki dunia leo Oktoba 7, 2019 nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu


Kwa miaka kadhaa Idar ya Usalama wa Taifa iliongozwa na vigogo kadhaa waliobobea katika masuala la Ulinzi na Usalama wakiwamo; Emir Mzena, Lawrance Gama, Hans Kitine ambapo alipoondoka nafasi hiyo ilikamatwa na Dk. Augustine Mahiga.

Mbali na hao nafasi hiyo ilishikiliwa pia na Amrani Kombe, Apson Mwang’onda, Rashid Othman, Dkt Kipilimba na Bwana Diwani Athumani

Hivi Kifo cha Imran Kombe hadi leo Watanzania tuliambiwa kilitokana na nini hasa au nini kilitokea hadi Umauti kumkuta vile?
 
Mtu ameshafariki halafu nawe tena ' Unamsimanga ' hapa je, umeambiwa kuwa ' Maiti ' huwa inasikia? Miswahili bhana!
Hata ukumtakia mema mtu mwovu ataenda motoi tu , ndio maana tunamtakia alazwe anapostahili, Mungu ndio anajua
 
Ndiyo alikuwa mkurugenzi enzi zile Dr. Ulimboka alipotekwa na kuokotwa msitu wa Mabwepande akiwa yuko hoi bin taaban?

Tunamtakia kila la heri huko aendako.
hapana hakuwa yeye alikuwa aliefuatana na kipilimba
 
Afrika Kusini alipelekwa Na familia? Kwanini familia ithibitishe kifo cha Mtendaji Mkuu wa idara ya serikali? Taarifa hiyo Ina ukweli gani?

Iko hivi, sikiliza ukiwa mstaafu mipango yote ya matibabu na hata mazishi huongozwa na familia. Serikali inasaidia na kushiriki kwa maelekezo na muongozo wa familia.
 
Mkuu nipo sana tu sema siku hizi nimehamia kule jukwaa la intelijensia, elimu na jukwaa la biashara!! kwenye siasa napita pita japo si kiivo!!
sawa pia mimi napitia humo, jaribu kupitia hata hapa, unaweza pitwa na jambo muhimu sana mkuu.kumbe wewe ni fellow bussisnessman like me, hongera sana,kuwa na siku jema
 
Back
Top Bottom