TANZIA Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda afariki Dunia nchini Afrika Kusini

TANZIA Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda afariki Dunia nchini Afrika Kusini

Moderator imefika wakati sasa huo uzi hapo chini kutoka kwa Mzee Mwanakijiji unaozungumzia uchafu wa Mwang'onda Ufunguliwe ili ajadiliwe kwa haki kutokana na matendo yake ili Mungu achukue hatua zinazostahili dhidi yake .

Natanguliza shukrani

Ajadiliwe kwa Kosa gani labda ambalo una uhakika nalo kuwa alilifanya chini ya Uongozi wake kama TISS DG enzi zake?
 
Dah nakumbuka enzi hizo kitaa kwenye daraja la Apson kabla ya kwa Zenna Kawawa, kuna jamaa alimuibia mbwa wake

Yule jamaa akipita nje ya ukuta wako kama mbwa wako ndani watavunja banda wamfuate sijui alikuwa anatumia nini

R. I. P Mzee Apson

Ulichokiandika kama si Kukitapika hapa kina ' connection ' gani na ' logic ' ipi hasa kulingana na taarifa ya huu Msiba wake? Miswahili bhana!
 
alafu eti mijitu inakuja hapa inasema RIP, pumbav, muacheni Mungu aweke mavuno yake panapostahili, na kama damu ya ulimboka ipo kwake basi italia mpaka kizazi chake cha nne
Mabalaa ya damu za watu yanaanza saaa kuwatafuta kizazi cha kwanza hadi cha nne, Mungu sio mwongo ni mwaminifu. Sasa kaenda na mali alizotumikia??
 
Rambirambi kwa mwalimu Mrs. Apson Mwang'onda, Thomas Mwang'onda na familia.

Mwambie ' Brazameni ' Jimmy asisahau Kupitisha Kitabu cha Maombolezo cha Msiba wa Baba yake kwa wana Darasa la Saba Wenzake wa ' Obey ' wa mwaka 1992 chini ya Mwalimu Mkuu Marehemu Mama Ng'ambi. Na kwa Kuanzia tu aanze upesi sana na Dada Brenda Msangi Boss Mkuu pale CCBRT Msasani kisha amuwahi na aliyekuwa Jirani yake wakati wakiishi Jirani na Maogesheo ya Mbwa pale ' roundabout ' mita chache tu kutoka Shule ya Msingi ya Obey Dada Mwasu Lubuva ( Binti wa Mzee Jaji Mstaafu Damian Lubuva ) Mimi mchango wangu pekee ambao nitautoa kwakuwa ni ' apeche alolo ' ni wa kupokea tu hiyo Michango, Kuihesabu Kiukamilifu kisha anaihakiki halafu namkabidhi Tom.

Poleni sana Familia ya Mzee Colonel Apson Mwang'onda, Bwana ametoa na Bwana ametwaa pia. Tupo pamoja hasa katika Kipindi hiki Kigumu mno na cha Majonzi ambacho mnakipitia na kikubwa tu nawaomba muwe Wavumilivu na tumuombee Mzee ili basi Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake kama Binadamu wengine, ampokee na amlaze mahala pema peponi Amen / Amina.

Sijajua kwa sasa Msiba upo wapi ila mkitusadia kutupa Maelekezo tutashukuru ili na Sisi wengine tuweze Kujumuika nanyi.
 
Damu ya IMRAN KOMBE inawalilia watu, sijui nani ila zile risasi alizomiiniwa, mpaka kizazi cha 4

Kama kuna DG aliyeanza Kuiharibu Idara huku ' Watendaji ' wake wengi wakianza ' Kujitajirisha ' hovyo huku Idara nayo ikiwa na matumizi mabaya ya Fedha, Majungu huku Fitna nazo pamoja na Visasi baina ya Wafanyakazi vikiongezeka ni huyu uliyemtaja hapa IK. Na ana mengi mno ila Kimaadili na hasa kwa Mila za Kiafrika huwa haturuhusiwi sana ' Kumnanga ' Marehemu. Udhaifu mkubwa wa Watendaji wa Idara ulianzia Kuota Mizizi katika Uongozi wake.
 
Je Ben Mwang'onda wa Azam Tv ana undugu na huyu mzee?

Kwa utaratibu usio rasmi wa Kitanzania ( Kiswahili ) hata kama Mtu fulani hamna Undugu wowote lakini Majina yenu ya Ukoo yamefanana halafu akawa pia ni Kiongozi basi ni lazima tu huyo Mtu ' atajirasimisha ' nae kwa namna moja au nyingine kuwa ni Nduguye na hata kusema ni Baba yake Mzazi.
 
Kwani ' Spymasters ' ndiyo huwa wanawaweka Madarakani Marais wa Tanzania? Watanzania tunapenda mno Uzushi na Uwongo.

Wewe poyoyo huwezi kujua jinsi spymaster anavyoweza kuinfluence matokea katika hatua mbalimbali za uchaguzi!! Marehemu alikuwa karibu sana na wana mtandao mwaka 2005 na ndio maana waliweza kukwapua fedha za EPA zilizofanikisha kuchaguliwa kwa mkwere!!!
 
Hahahaha, Oysterbay Primary school hii nini

Pamoja na kwamba alikuwa akifundisha hiyo Shule na Mwanae wa ' Kudekadeka ' Jimmy alikuwepo lakini alikuwa akimkuta amefanya Kosa anampa ' Bakora ' ambazo hata Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Chalamila za hivi majuzi zilikuwa ni za cha Mtoto tu. Na usiombe Siku awepo zamu na Mwalimu Mmoja wa Kiume Mkurya aliyekuwa ametokea JKT Nyagabona halafu uwe na Makosa hicho Kipigo chao cha ' Kolabo ' lazima tu ukitoka hapo utaenda Kuhadithia Kwenu. Walimu walikuwepo zamani siyo hawa wa Miaka hii waliolegea sana kiasi kwamba hata Wanafunzi wao tu huwa wanawatisha na wanawaogopa vile vile.
 
Back
Top Bottom