Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Wako watu kwa maksudi na kwa dhati kabisa hawalitakii taifa hili hali iliyo nzuri kwa 100%,na wachonganishi kwa rais na umma wa watanzania.Nilishangazwa Sana na kauli aliyoitoa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande, eti pamoja na mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere, kukaribia kukamilika, watanzania tutegemee mgao zaidi wa Umeme, Kwa kuwa mahitaji ya Umeme wa nchi hii ni Megawatt 60,000😎
Maneno hayo aliyatoa katika mjadala maalum, ulioandaliwa na Mwananchi Twitter Space.
Hivi Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, anatufanya watanzania wote hatuna akili, tusiokumbuka maneno yaliyotolewa na viongozi wetu wakuu wa nchi, kabla ya kukamilika Kwa mradi huo mkubwa kabisa wa nchi, ambao watanzania tumekamuliwa zaidi ya shilingi trillion 7 kuwa mradi huo ndiyo utakaokuwa mkombozi Kwa nchi yetu, Kwa kuwa mradi huo unategemea kuzalisha Umeme wa Megawatt 2,115 na tutazalisha Umeme wa "surplus" ambao kama nchi tynategemea kuwauzia Umeme nchi za jirani, na hivyo kutengeneza pesa nyingi za kigeni.
Hivi Hawa viongozi wetu wanatuonaje watanzania, kiasi Cha kupenda kutuongopea watakavyo?
Inavyoelekea huyo Maharage Chande, anatuandaa watanzania kisaikolojia, Ili tutakapoona mgao unaendelea, basi tujue kuwa KAZI INAENDELEA, ya kuuza majenereta yao😞
Mimi naona muarobaini wa tatizo hili sugu la kuongopewa watanzania wakati wote na viongozi waandamizi wa serikali hii ya CCM, ni kuwapiga chini watawala Hawa wa CCM na kukiingoza chama kingine Ili kiingoze nchi
Bila hivyo matatizo ya watanzania hayatakuja kutatuliwa na watawala hawa wa CCM Hadi mwisho wa Dunia hii😎
STABLE ELECTRIFICATION REFLECTS TO STABLE COUNTRY. NCHI HAIWEZI KUWA IMARA KIUCHUMI KAMA HAKUNA UMEME WA UHAKIKA NA NAFUU.
UMEME NAFUU MAANA YAKE NI VIWANDA VINGI NA PRODUCE NYINGI NDANI YA NCHI.
#INAUDHI SANA.