Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande asema pamoja na kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Nyerere, watanzania tutegemee migao zaidi!

Ndugu Mleta madam, kwanza isome vizuri hiyo Article ya nwananchi na sikiliza vizuri alichosema Chande.

Amesema utafiti umefanywa nankuandikwa kwenye majarida, ili kuwe na uchumi wa Viwanda lazima katika kila Jamii 1m wawe na umeme wa 1000MW kutosheleza watu na viwanda.

Sasa hivi tunazalisha 1600MW, Bwana likikamilika litazalisha 2100MW = Approx. MW 3700, haitoshi watu 60m na viwanda.

Tuwe makini sana kutafsiri maneno ya wenzetu .
 
Mbona wapiga Kura washafanya hivyo mara kadhaa.. Wanapiga chini ccm, halafu NEC inawatangaza ccm kuwa washindi.
Huwa hawategemei kura!
Absolutely true.

Ndiyo maana tunataka Katiba mpya, ambayo itaweka muundo mpya wa uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi nchini.
 
Ndugu Mleta madam, kwanza isome vizuri hiyo Article ya nwananchi na sikiliza vizuri alichosema Chande.

Amesema utafiti umefanywa nankuandikwa kwenye majarida, ili kuwe na uchumi wa Viwanda lazima katika kila Jamii 1m wawe na umeme wa 1000MW kutosheleza watu na viwanda.

Sasa hivi tunazalisha 1600MW, Bwana likikamilika litazalisha 2100MW = Approx. MW 3700, haitoshi watu 60m na viwanda.

Tuwe makini sana kutafsiri maneno ya wenzetu .

Swali kwako wewe unayemuelewa Maharage, kwa nini tumeishi miaka 5 kabla ya Maharage na Makamba bila mgao wa umeme wala maji? Huo umeme tuliokuwa tunatumia ulikuwa unatoka wapi? Na kwa nini ghafla tu baada ya Raisi huyu kuletwa mgao wa maji na umeme ukaanza?
 
Nilishangazwa Sana na kauli aliyoitoa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande, eti pamoja na mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere, kukaribia kukamilika, watanzania tutegemee mgao zaidi wa Umeme, Kwa kuwa mahitaji ya Umeme wa nchi hii ni Megawatt 60,000😎

Maneno hayo aliyatoa katika mjadala maalum, ulioandaliwa na Mwananchi Twitter Space.

Hivi Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, anatufanya watanzania wote hatuna akili, tusiokumbuka maneno yaliyotolewa na viongozi wetu wakuu wa nchi, kabla ya kukamilika Kwa mradi huo mkubwa kabisa wa nchi, ambao watanzania tumekamuliwa zaidi ya shilingi trillion 7 kuwa mradi huo ndiyo utakaokuwa mkombozi Kwa nchi yetu, Kwa kuwa mradi huo unategemea kuzalisha Umeme wa Megawatt 2,115 na tutazalisha Umeme wa "surplus" ambao kama nchi tunategemea kuwauzia Umeme nchi za jirani, na hivyo kutengeneza pesa nyingi za kigeni.

Hivi Hawa viongozi wetu wanatuonaje watanzania, kiasi cha kupenda kutuongopea watakavyo?

Inavyoelekea huyo Maharage Chande, anatuandaa watanzania kisaikolojia, Ili tutakapoona mgao unaendelea, basi tujue kuwa KAZI INAENDELEA, ya kuuza majenereta yao😞

Mimi naona muarobaini wa tatizo hili sugu la kuongopewa watanzania wakati wote na viongozi waandamizi wa serikali hii ya CCM, ni kuwapiga chini watawala Hawa wa CCM na kukiingoza chama kingine Ili kiingoze nchi.

Bila hivyo matatizo ya watanzania hayatakuja kutatuliwa na watawala hawa wa CCM Hadi mwisho wa Dunia hii😎

====

Chande: Bado kuna safari ndefu kufikia umeme wa viwanda

Muktasari:

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Maharage Chande amesema mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kuendesha uchumi wa viwanda.

Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema, licha ya juhudi za Serikali kuongeza vyanzo vya umeme likiwemo Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), bado kuna safari ndefu kufikia umeme wa uchumi wa viwanda.

Ameyasema hayo leo Desemba 21 katika mjadala wa Mwananchi- Twitter Space unaoendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited.

Amesema Mradi wa Bwawa wa Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) unaotarajiwa kukamilika mwaka 2024 ni sehemu ya hatua za kupunguza changamoto hizo.

“Mradi huu utaleta umeme mwingi kwenye gridi, lakini mradi huu ni moja kati ya hatua ya safari ndegu ambayo tunayo kama nchi ya kuzalishaji kusafirisha na kusambaza umeme,” amesema Chadema leo Desemba 21, 2022 wakati wa mjadala.

Katika ufafanuzi wake, Chande amesema utafiti uliofanyika katika majarida mbalimbali unaonyesha ili uwewe na umeme wa kutosha kwa ajili ya viwanda na kukuza uchumi kila watu milioni moja wanahutaji megawati 1,000.

“Kwa idadi ya watu milioni 60, utaona tunahitaji umeme megawati 60,000 lakini kwa sasa tuna megawati 1500, tukileta hii 2115 tutakua na takribani megawati 3,800. Tunakazi kubwa ya kuongeza uzalishaji wa umeme,” amesema Chande.

Katika hatua nyingine, Chande amesema kama hakutakuwa na changamoto, ratiba ya kukamilisha mradi huo inabaki kuwa mwaka 2024.

“Hakuna aliyetegema Covid19, utaona pia kama bwawa hilo ikitokea changamoto tutatoa taarifa lakini mambo yakienda vizuri Juni mwaka 2023 tutakuwa tumemaliza,” amesema

Kesho Desemba 22, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua hatua ya kuanza kujaza maji katika bwawa hilo lililokamilika asilimia 79 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji wa Sh6.5trilioni zitakazokata kero kabla ya 2025.

Bwawa hilo lenye uwezo wa kuhifadhi lita bilioni 33.2 za maji eneo la Mto Rufiji mkoani Pwani, lilianza kujengwa 2019.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Tumecoka kusema Rais Samia anahujumiwa, sasa tunamtwika udhaifu yeye mwenyewe. Rais Samia anadanganywa na wanamdharau watendaji wake aliowataua kwa sababu wote kawateua inawezekana kawateua kwa mashinikizo. Yaani mi hata kumuombea sasa nimeshachoka kabisa. Yaani Rais aseme bwawa likikamilika mgao basi ila agent wa economic hitmen aseme mgao utaendelea kuwepo. Yaani inaudhi sana tena sana. Lengo lao ni kuhakikisha Tanzania haivutii wawekezaji kwa kutokuwa na uhakika wa umeme. Kwa sababu kama unajiandaa kuwa na umeme wa uhakika laizma ujigambe ili dunia ijue haitakuwa na tatizo la umeme watu waje wawekeze ila hawa wateule wa rais wao kila siku wanaona sifa kusema eti mgao mgao. Hivi kwa nini kipindi cha Dkt Magufuli umeme ulikuwa haukatiki?? Yaani ingekuwa china walipaswa kuuawa kwa rushwa ila iko siku

1671866578403.png
 
Sitaki kukiongezea kichwa changu stress zaidi kwa haya matamko na mafafanuzi
 
View attachment 2456456
Tumecoka kusema Rais Samia anahujumiwa, sasa tunamtwika udhaifu yeye mwenyewe. Rais Samia anadanganywa na wanamdharau watendaji wake aliowataua kwa sababu wote kawateua kwa vimemo
Ni Upuuzi kuteketeza 7Trilioni kwenye umeme wa maji halafu ni 2115MW tu.

Kama kweli wana nia nzuri wawekeze kwenye umeme wa nuclear.
 
Tatizo la nchi yetu ni kukosa au kutokuwa na kamati ya maamuzi, tunategemea wanasiasa badala ya watalaamu. Halafu eti unamkuta professor anasifia maamuzi ya mtu ambaye uamuzi wake una shaka kabisa
 
Ni Upuuzi kuteketeza 7Trilioni kwenye umeme wa maji halafu ni 2115MW tu.

Kama kweli wana nia nzuri wawekeze kwenye umeme wa nuclear.

Umeme wa nuclear mpaka wapate ruhusa kwa bosi, uliza AK mpaka Zuma aliondolewa kisa alitaka umeme wa nuclear na mpaka leo bado AK wanahaha na kuhangaika isitoshe kama huu wa maji tu unatushinda kuutumia kwa 100% tutauweza wa nuclear?

Tanzania kuna mgao sababu ya uzembe na incompetence na siyo kukosekana kwa maji, hivyo hata hiyo gesi pia kwa incompetence hii hamna kitu!
 
Ni strategy tu. Tatizo la nchi yetu ni kukabidhi maamuzi ya kitalaamu kwa mtu mmoja anayeitwa Rais. Kipindi cha Mwl Nyerere ilikuwa sawa maana ndiye alikuwa msomi. Ila kwa sasa nchi imebadilika sana, rais anatakiwa awe kama Mkapa au Dkt Magufuli, yaani rais akubali kutumia watalaamu na yeye mwenyewe asome nyaraka na kusoma strategy za nchi au ahakikishe watalaamu wanamuweka wazi bila wogs
 
Umeme wa nuclear ndio wa uhakika ,sema initial cost ndio gharama na inachukua muda kuumaliza ila ukishaufunga ndio ntolee mkataba tosha miaka 100+
 
Alinukuliwa akisema kuwa Megawatts 60,000 ndizo zitakazotifanya watanzania tujitegemee Kwa mahitaji yetu ya Umeme!

Ndiyo utambue hapo kuwa huyu Rais wetu, sijui huwa anawaokota jalalani hao wateule wake?😎

Kuna umuhimi mkubwa Sana wa kupata Katiba mpya ya nchi, ambayo itampunguzia madaraka makubwa mno Rais ya kufanya uteizi mbalimbali na Wala hapaswi kuulizwa, vigezo gani alivyotumia vya teuzi zake!
Kasema kwa uchumi wa viwanda kimahesabu kila watu 1m watahitaji megawatt 1000,so Tanzania 60m tutahitaji 60,000megawatts..Sasa huo uchumi wa viwanda tz uko wapi!?..yeye aliongelea makadirio,muwe mnasoma na kuelewa
 
Ha ha ha ha kwahiyo anamaanisha tokea hii Nchi izaliwe imefanikiwa kuzalisha umeme kwa asilimia 2.5% tu ya mahitaji halisi na bwawa likikamilika itakuwa asilimia 6.3% ya mahitaji.
Jamaa lazima kuna mahali kajichanganya.

Na hizo MW 60k sio za mchezo mchezo.
Nchi za wenzetu zilizoendelea 1 MW inahudumia fully makazi approximately 1000 kwa mwaka sasa sisi hizo MW 60k ni za nini.
 
Ni strategy tu. Tatizo la nchi yetu ni kukabidhi maamuzi ya kitalaamu kwa mtu mmoja anayeitwa Rais. Kipindi cha Mwl Nyerere ilikuwa sawa maana ndiye alikuwa msomi. Ila kwa sasa nchi imebadilika sana, rais anatakiwa awe kama Mkapa au Dkt Magufuli, yaani rais akubali kutumia watalaamu na yeye mwenyewe asome nyaraka na kusoma strategy za nchi au ahakikishe watalaamu wanamuweka wazi bila wogs

Dunia inaongozwa na satanist, itoshe tu kusema hivyo, usifikiri kila mtu anapenda maendeleo ya watu wote, kuna watu wanapenda tunavyopata shida ndiyo furaha yao, matazizo mengi na umaskini uliopo ni wa kutengenezwa kwa makusudi kabisa, …
 
Nilishangazwa Sana na kauli aliyoitoa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande, eti pamoja na mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere, kukaribia kukamilika, watanzania tutegemee mgao zaidi wa Umeme, Kwa kuwa mahitaji ya Umeme wa nchi hii ni Megawatt 60,000😎

Maneno hayo aliyatoa katika mjadala maalum, ulioandaliwa na Mwananchi Twitter Space.

Hivi Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, anatufanya watanzania wote hatuna akili, tusiokumbuka maneno yaliyotolewa na viongozi wetu wakuu wa nchi, kabla ya kukamilika Kwa mradi huo mkubwa kabisa wa nchi, ambao watanzania tumekamuliwa zaidi ya shilingi trillion 7 kuwa mradi huo ndiyo utakaokuwa mkombozi Kwa nchi yetu, Kwa kuwa mradi huo unategemea kuzalisha Umeme wa Megawatt 2,115 na tutazalisha Umeme wa "surplus" ambao kama nchi tunategemea kuwauzia Umeme nchi za jirani, na hivyo kutengeneza pesa nyingi za kigeni.

Hivi Hawa viongozi wetu wanatuonaje watanzania, kiasi cha kupenda kutuongopea watakavyo?

Inavyoelekea huyo Maharage Chande, anatuandaa watanzania kisaikolojia, Ili tutakapoona mgao unaendelea, basi tujue kuwa KAZI INAENDELEA, ya kuuza majenereta yao😞

Mimi naona muarobaini wa tatizo hili sugu la kuongopewa watanzania wakati wote na viongozi waandamizi wa serikali hii ya CCM, ni kuwapiga chini watawala Hawa wa CCM na kukiingoza chama kingine Ili kiingoze nchi.

Bila hivyo matatizo ya watanzania hayatakuja kutatuliwa na watawala hawa wa CCM Hadi mwisho wa Dunia hii😎

====

Chande: Bado kuna safari ndefu kufikia umeme wa viwanda

Muktasari:

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Maharage Chande amesema mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kuendesha uchumi wa viwanda.

Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema, licha ya juhudi za Serikali kuongeza vyanzo vya umeme likiwemo Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), bado kuna safari ndefu kufikia umeme wa uchumi wa viwanda.

Ameyasema hayo leo Desemba 21 katika mjadala wa Mwananchi- Twitter Space unaoendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited.

Amesema Mradi wa Bwawa wa Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) unaotarajiwa kukamilika mwaka 2024 ni sehemu ya hatua za kupunguza changamoto hizo.

“Mradi huu utaleta umeme mwingi kwenye gridi, lakini mradi huu ni moja kati ya hatua ya safari ndegu ambayo tunayo kama nchi ya kuzalishaji kusafirisha na kusambaza umeme,” amesema Chadema leo Desemba 21, 2022 wakati wa mjadala.

Katika ufafanuzi wake, Chande amesema utafiti uliofanyika katika majarida mbalimbali unaonyesha ili uwewe na umeme wa kutosha kwa ajili ya viwanda na kukuza uchumi kila watu milioni moja wanahutaji megawati 1,000.

“Kwa idadi ya watu milioni 60, utaona tunahitaji umeme megawati 60,000 lakini kwa sasa tuna megawati 1500, tukileta hii 2115 tutakua na takribani megawati 3,800. Tunakazi kubwa ya kuongeza uzalishaji wa umeme,” amesema Chande.

Katika hatua nyingine, Chande amesema kama hakutakuwa na changamoto, ratiba ya kukamilisha mradi huo inabaki kuwa mwaka 2024.

“Hakuna aliyetegema Covid19, utaona pia kama bwawa hilo ikitokea changamoto tutatoa taarifa lakini mambo yakienda vizuri Juni mwaka 2023 tutakuwa tumemaliza,” amesema

Kesho Desemba 22, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua hatua ya kuanza kujaza maji katika bwawa hilo lililokamilika asilimia 79 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji wa Sh6.5trilioni zitakazokata kero kabla ya 2025.

Bwawa hilo lenye uwezo wa kuhifadhi lita bilioni 33.2 za maji eneo la Mto Rufiji mkoani Pwani, lilianza kujengwa 2019.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Kama vipi zalisha umeme uwauzie Tanesco au kuwa self-sufficient kwa kuwa na chanzo chako cha umeme.
 
Back
Top Bottom