Mkurugenzi Mpya TPA, Bw. Erick Benedict Hamis amewahi kufaulu katika lipi?

Mkurugenzi Mpya TPA, Bw. Erick Benedict Hamis amewahi kufaulu katika lipi?

Kama umetumia takwimu za awamu ya Tano nakukumbusha hata Bodi ya Mikopo ilitoa gawio japo kuna watu walikuwa wamekosa mikopo ,ATC walitoa hadi gawio kumbe imepigwa 'tanganyika jeki' ya Mabilion
Hahahaha noma sana
 
Mkuu unataka iwe kama Kenya, wao kumpata bosi wa Kenya Port Authority (KPA) inatangazwa nafasi watakao kuwa na vigezo wanaingia kwenye usahili.

Ukipata marks below 70% umedis qualify na unatangazwa public.

Sasa Bongo ikiletwa hii itakuwa vita, mtu ana vigezo anapewa interview Kisha anafeli magazeti kesho yapo na wewe. Bado wakijua mshahara na bonus utazopata kutoboa itakuwa ni ndoto.
Kwani Kenya walianzaje mkuu?
 
Tuondoe mambo ya kuteuana, nafasi zitangazwe watu wafanye interview na mwisho iwe ni nafasi za mikataba.
Hakuna sehemu mbaya ambayo rushwa na vimemo zinatembea kama kwenye interviews. Teuzi sio mbaya kama vetting committee inaletewa majina yawalio aminiwa na kupitia CV zao kwa ukamilifu.
 
Hakuna sehemu mbaya ambayo rushwa na vimemo zinatembea kama kwenye interviews. Teuzi sio mbaya kama vetting committee inaletewa majina yawalio aminiwa na kupitia CV zao kwa ukamilifu.
Hapo kwenye vetting ndiyo kuna rushwa kuliko wewe unavyodhani
 
Hapo kwenye vetting ndiyo kuna rushwa kuliko wewe unavyodhani
Kwa mfano commissioner wa KRA anashindwa kupitisha mtu wake kwenye nafasi kwa zile interview zetu za DUCE???
 
Popotebwatoke unawajua majina yao hao wafanya vettting?
Sijui hata kama unaelewa maana ya vetting nini? sijui kwa akili ako unafikiri wanafanya huku wamevaa hijabu? jambo ambalo hulijui ni vizuri kuuliza, akina Bashiru wakikudanganya kuwa nimeshitukizwa huu uteuzi sijui na ww hutumie hata akili kdg, mtu anateuliwa saa 12 jioni kwao ni Kigoma kesho saa 3 anatakiwa kuapishwa Dar sijui hata huelewi.
 
Kwani Kenya walianzaje mkuu?
Kule Raisi wao aliweka sheria ili uwe Director wa KPA apatikane kwa kuomba na kufanyiwa interview.Walivyo anza sijajua mkuu.
Pitia link uone mchuano wa kumpata boss unavyoenda.

Screenshot_20210406-092936.png
 
Kuongoza watanzania kazi sana, Mama angebaki na wateule wote walioteuliwa na hayati bado mngepiga milunzi sasa ameamua kubadilisha kidogo bado hamridhiki.
Ndiyo demokrasia mkuu usitegemee siku moja watu wakae kimya kwamba mama amefanya kazi nzuri ikawaridhisha watu wote haiwezi kutokea lakini muhimu ni kjitahidi kufanya vizuri kadiri inavyofaa
 
Alifufua shirika la Marine Services lilikuwa mbioni kubinafsishwa. Shirika lilikuwa linapewa ruzuku na Serikali lakini kwa sasa linajiendesha na lina Meli za kutosha ziwa ni.
Na hizo meli zilinunuliwa chini ya kamanda mwendazake,wakati wa enzi za mzee wa msonga na chinga kila kitu kilikuwa ICU, tumshukuru sana Jiwe kwa kutuweka sawa.Mungu azidi kumpa pumziko la milele,tutazidi kumkumbuka kwa mazuri aliyoyafanya.
 
Niombe mwenye CV ya Mkurugenzi Mpya wa TPA lakini pia tupate experience yake pamoja na Miradi au ofisi alizowahi kuhudumu na mafanikio au mabadiliko aliyosababisha katika ofisi hizo.

Tumekuwa na wateule wa Rais ambao hawajawahi kufanikiwa popote walipowahi kufanya kazi, lakini pia utamaduni wakutumia vyeti vya taaluma nao umetukwamisha kwenye mambo mengi, utaratibu mmoja wakutumia makada wa CCM pia nao umelididimiza Taifa.

Ningependa kujua huyu Bwana huko alikokuwa alifanya nini hadi tumkabidhi bandari zetu?

Ukitafuta taarifa zake mitandaoni haupati ile flavour ya kupata nafasi ya Mkurugenzi wa bandari. Tukumbuke ili ni lango kubwa la uchumi wetu.
Kitendio wanachokifanya walo nyuma za hizi teuzi ni usaliti dhidi ya watanzania.

TPA ni moja ya njia kuu za kuingiza mapato ya taifa hivyo kuna kila sababu zilizo juu ya uwezo wa hawa watu kuhakikisha mteule yoyote wa kuongoza TPA ana sifa zinazostahiki.

Wakti huohuo TPA ni sehemu ya kupitisha makontena bila kuyafanyia scanning, na kutolipa kodi na vitendo vyote vya uhujumu uchumi wa nchi.

Kwa bahati nzuri sisi sote hapa ni mashuhuda wa kinachoendelea na tunashuhudia mengi.
 
Back
Top Bottom