Mkurugenzi mtendaji TPDC, Dkt. Mataragio asimamishwa kazi

Mkurugenzi mtendaji TPDC, Dkt. Mataragio asimamishwa kazi

Hii ni ajabu, nimesoma gazeti la daily news wanasema amesimamishwa (iwapo itathibitika) kutokana na mikataba iliyosainiwa na TPDC mwaka 2010,2013 ambapo yeye kaanza kazi TPDC disemba 2014 au mapema januari 2015.

Hapa naona kuna chuki binafsi au maslahi binafsi kwenye huo ukurugenzi wa tpdc, vinginevyo hata gawana wa bot anatakiwa asimamishwe kutokana na makosa ya kina liyumba na kina mramba.

hii hapa sehemu ya habari ya daily news.

the audit centred on reviewing how oil and gas exploration contracts were awarded between 2010/11 and 2013/14 revealing serious inefficient management of the contracting and licensing process.

Dr Mataragio is among the few experts in minerals, oil and natural gas in the Diaspora who volunteered to offer free advice to the government on development of the sector. He holds a PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), from Missouri - Rolla University, Missouri, US (2005); Masters in Business Development (MBA), from Charlotte University, North Caroline, US (2008); MSc (Geochemistry and Petrology), from Okinawa University, Japan (1997); and BSc (Hons) (Geology), University of Dar es Salaam (1994). Prior to the post, Dr Mataragio was Senior Geoscientist with Bell Geospace Inc, Houston, Texas, US where he started working with the firm in 2004. Among major international Gas and Oil firms he worked with while employed by Bell Geospace include Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas (Malaysia) and Vale Rio Doce.
 
Afu hawa jamaa wanaongoza kwa kilipana mishara MINONO hapa Tz.
 
Kama taarifa za CAG zinatosha kusimamisha watu, basi kuna watu humu nchini wanapaswa wajisimamishe wenyewe kama hakuna watu wa kuwasimamisha.
 
Usalama umepungua makazini.

Especially kwa wale waliozoea kufanya kazi kwa ujanja ujanja na kufanya maamuzi kwa maslahi binafsi. Sisi tulijua Hawa wanaoletwa kutoka nje kwa exposure na weledi walionao wangefanya kazi tofauti na Hawa tuliowazoea humu.
 
Una point nzuri, sipingani nayo moja kwa moja wala kwa taathira yake, tena usinitafsiri vibaya,
Nasema hiviiii,
Mishahara haitoshiiiiiiiiiiii
 
Una point nzuri, sipingani nayo moja kwa moja wala kwa taathira yake, tena usinitafsiri vibaya,
Nasema hiviiii,
Mishahara haitoshiiiiiiiiiiii

Hakuna mshahara unaotosha. Sasa ukiniambia mshahara WA CEO WA TPDC hautoshi....ngachoka kabisa.....
 
Nadhani ni muda muafaka hizi report za CAG ziwekwe hadharani nasi tuwe tunazisoma. Wapost hata kwenye website zao, au serikali ianzishe special portal tuwe tunazipakua huko
Hizo report zipo kwenye website ya CAG nafikiri wabunge wetu wangekuwa wanaziprint kupeleka kwenye majimbo yao wananchi wasio na access ya Internet wajionee
 
TPDC ni ngumu kuiongoza sawa na TPA na TRA yapo mapungufu ya kweli,lakini yapo majungu na fitina za kimaslahi.Ila kama wakubwa wanejirudhisha hakuna jinsi.Yawezekana wanao taka kuondolewa ni hayo makampuni ya makubwa ya mafuta ya nchi za nje anawazibia riziki.
 
Kama taarifa za CAG zinatosha kusimamisha watu, basi kuna watu humu nchini wanapaswa wajisimamishe wenyewe kama hakuna watu wa kuwasimamisha.
wajisimamishe wenyewe kwani wamekuwa gegedeo!?
 
Hivi kama alikiuka sheria ya manunuzi ya umma si ilipaswa PPRA kua imetoa ripoti yake kuhusu hilo suala? Na ni kipengele kipi hasa amekiuka huyu bwana? Lazima tujiulize maswali ya muhimu sana kabla ya ku conclude... Nachelea kusema kwamba ukisoma taarifa zilizotoka katika magazeti leo inaonesha mkanganyiko wa habari wa hali ya juu, hili Shirika kwann lisitoe taarifa kwa wananchi juu ya yaliyotokea? Wanatupa tabu tu kuwaza na kujipa majibu wenyewe
 
Nadhani ni muda muafaka hizi report za CAG ziwekwe hadharani nasi tuwe tunazisoma. Wapost hata kwenye website zao, au serikali ianzishe special portal tuwe tunazipakua huko

Mkuu tusiwe watu wa kulalama kama leyland kwenye vilima, ulishwahi kupekua National Audit Office of Tanzania ukakosa hizo report? kwa taarifa tu ni kwamba hawa jamaa dakika chache baada ya kuziwasilisha hizi report yaa tarehe 31 March Kila mwaka kama sheria inavyowataka huwa wanazipandisha kwenye site yao na yeyeto huweza kuzipata huko.
 
Hivi kwa mtizamo wako umeona miye nimelalama? Hebu jifunze kusoma post za wenzio ukatulia na kutafakari. Unacho jua wewe sio wote wanajua sio uanze kujitia ujuaji. Mbona wenzio wametoa link tuu kistaaarabu. Akili nyiiiiiiingiiiii mbele kiza.
 
Wenye kunielewa wamenielewa, wewe subiri vasheni yako utaelewa tu!!!
Usalama wa vipi unaozungumzia wewe? Kuvamiwa na vibaka kuingiliwa na wanyama wakali?
 
Msishangae mme wa naibu spika akapewa hicho cheo
 
hoja za cag zinaonyesha utendaji usiofuata taratibu na sheria... pia ufujaji na wizi uwekwa wazi.

tatizo ni nadra sn watu kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya hoja kuibuliwa.

mara nyingi taasisi upewa hati chafu na kupunguziwa ruzuku.
 
Back
Top Bottom