Mkurugenzi mtendaji TPDC, Dkt. Mataragio asimamishwa kazi

Mkurugenzi mtendaji TPDC, Dkt. Mataragio asimamishwa kazi

Mimi simjui huyo mtu na hivyo sijui kama ana kosa au la. Hatahivyo hoja yako ya kutolewa Ulaya ni ya hafifu sana. Hivi mtu akitolewa Ulaya hawezi kufanya kosa??
Mara zote waliotolewa ulaya walitumika kama mipira baada ya lengo kukamilika unatupwa jalalani; yu wapi Dr. Balali? naye ciciyenu walimtoa USA wakamleta BoT; walipomtumia vizuri wakasema amefariki na nimarufuku mtu yoyote kuhuzuria mazishi yake ila serikali peke yake ndo inaruhusiwa😡😡🙁 hiyo ndo tabia ya maciciyenu.
 
Unaamini kwenye mizimu? Ndio maana hueleweki,jibu swali ni usalama upi kazini unaouzungumzia wewe?
Una cheti kikuuuubwa lakini maswali yaliyosababisa ufaulu ni kama:-
Siasa ni...........
Wewe ukajaza kilimo ukapata.

Asiyejua maana haambiwi maana.
 
Hapo bila kuharibu mengine, wawewaangalifu sana. Huyo inawezekana anafanya hivyo kwa manufa ya nchi pia. Huwezi kuona social capital kama moja ya asset kwenye natural resource economics. Efficiency yake inakuwa kubwa zaidi anapofanya kazi na watu ambao ame fellowship nao kwa muda mrefu pengine they can come at winwin scenario kiurahisi zaidi kuliko nchi zingine; kama ndivyo hiyo haiwezi kutafsiriwa kuwa ni conflict of interest unless kuna grounds zingine.

Tatizo letu ambalo tunalo nikushindwa kuweka context kwenye sheria zetu na rules zetu.

Mimi leo ukinipa kifanya kazi ili niwe efficient lazima niweze kitengeneza team itakayonipa back up na kufill in gaps za weakness zangu kwenye area of my experize, hilo ss huwa hatuangalii tunaendesha mno mambo bila kuweka context.

I was arguing the same jata kwenye UKUTA hiyo sheria mna ii inteprete kuvunjwa kwa perspective na ya upande fulani either of the side bila kiweka context ni sheeda!

Watanzania tubadilike tumesoma kuelimika siyo kila jambo kulichukulia juu juu tu. Mtakatisha watu tamaa hadi washindwe kuja kusaidia...

Lakini pia hao waliochukuliwa msitume advantage hiyo for your personal gains. Ebu tuwe honest na kujali uadilifu bila kusababisha hisia mbaya. Ingekuwa vizuri angetoa mawazo yake kwenye tendering ili yaweze kuwa one of the criteria. Ila pia utakuta pia kuna kuviziana kwingi kwenye ofisi zetu.
 
Una cheti kikuuuubwa lakini maswali yaliyosababisa ufaulu ni kama:-
Siasa ni...........
Wewe ukajaza kilimo ukapata.

Asiyejua maana haambiwi maana.
Viroba vinakusumbua unakwepa hoja
 
kasharudi kwa mkewe USA au bado yuko Bongo?
 
Hii ya kusimamishwa tu haitoshi, na ikiwa kweli wameamua kumsimamisha maana yake tayari wamejiridhisha kwa tuhuma husika.
Nasubiri kusikia mtuhumiwa anafikishwa mahakamani ili akajibu mashtaka ya wizi na ufujaji wa mali ya uma.

Ndugu yangu hata hiyo kesi haina haja....unaweza kushangaa mtuhumiwa kaisbabishia serikali hasara ya mabilioni....yeye anapigwa fine miezi jela au kutoa milioni kumi......

Rejea kesi ya wakina mramba.....
 
Aliacha kazi yake nzuri sana US kurudi nyumbani ili kuja kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo nchini sasa imekula kwake.

Imenikumbusha Daktari Masau daktari mzalendo ambaye alienda kusomea udaktari wa upasuaji moyo US. Baada ya kumaliza vizuri sana masomo yake pamoja na vishawishi chungu nzima alivyovipata vya kubaki US ikiwemo mshahara na marupurupu manono aliamua kurudi nyumbani ili aje asaidie Watanzania wenye matatizo ya moyo, lakini akaishia kupigwa vita kwa kila namna ikiwemo kuomba rushwa na maofisa mbali mbali wa Serikali (wizara ya afya na kwingineko) ili tu 'wamsaidie' kuanzisha hospitali yake. Matatizo makubwa aliyokutana nayo katika kuanzisha hospitali yake yakamsababishia msongo wa mawazo hadi alipokutana na kifo chake.

TANZIA: Dr. Ferdinand Masau wa Tanzania Heart Institue afariki dunia

Kufanya kazi Tanzania shida tupu. Arudi zake Ulaya akale bata kwa mrija.
 
We will be following his progress with great interest, and are sure that he will bring a breadth of skill and experience to this role that will ensure that TPDC has a significant impact on exploration and production in Tanzania”.
Duh...noma hii!
 
Kufanya kazi Tanzania shida tupu. Arudi zake Ulaya akale bata kwa mrija.

Bongo majungu. Enzi hizi za kukurupuka bila kufanya uchunguzi wa kina watafukuza kila brain wabaki na makarani!!
 
Tatizo kubwa katika uendeshaji wa mashirika ya umma nchini ni kuingiliwa kisiasa katika utendaji wake. Hili tatizo ni la kimfumo kwa sababu ma-CEO na bodi za wakurugenzi, kwa mujibu wa sheria, wanateuliwa na wanasiasa (rais, mawaziri). Na kikubwa kinachozingatiwa katika teuzi hizi ni utiifu wa kisiasa (political allegiance) na siyo uwezo, weledi na uadilifu. Kwa mfano ni kawaida kwa ma-CEO wa mashirika ya umma kutakiwa kuchangia mikutano na kampeni za 'chama' na kufanikisha hili kikamilifu kutachukuliwa kama kigezo cha uwezo wake wa kazi! (Atajua atakakopata pesa!). Sasa swali linakuja: kwa nini mashirika ya umma yasiendeshwe kwa uhuru (autonomously) kwanza kwa viongozi wake kupatikana kwa kupitia usaili unaoendeshwa na taasisi za kitaalamu na kupimwa kwa vigezo vya kisayansi vya utendaji? Why do we have to put too much trust in politicians?
 
Bongo majungu. Enzi hizi za kukurupuka bila kufanya uchunguzi wa kina watafukuza kila brain wabaki na makarani!!

Bongo unafanya kazi na wanasiasa vilaza, unawapa ushauri wa kitaalamu halafu wanakataa.
 
Aliacha kazi yake nzuri sana US kurudi nyumbani ili kuja kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo nchini sasa imekula kwake.

Imenikumbusha Daktari Masau daktari mzalendo ambaye alienda kusomea udaktari wa upasuaji moyo US. Baada ya kumaliza vizuri sana masomo yake pamoja na vishawishi chungu nzima alivyovipata vya kubaki US ikiwemo mshahara na marupurupu manono aliamua kurudi nyumbani ili aje asaidie Watanzania wenye matatizo ya moyo, lakini akaishia kupigwa vita kwa kila namna ikiwemo kuomba rushwa na maofisa mbali mbali wa Serikali (wizara ya afya na kwingineko) ili tu 'wamsaidie' kuanzisha hospitali yake. Matatizo makubwa aliyokutana nayo katika kuanzisha hospitali yake yakamsababishia msongo wa mawazo hadi alipokutana na kifo chake.

TANZIA: Dr. Ferdinand Masau wa Tanzania Heart Institue afariki dunia

Kuwa mtanzania ni shida sana. Uzalendo alikufa nao Nyerere.
 
Duuh hiyo ndiyo jamiii forum wengine tulikuwa hatumjua huyo mtu duh umetisha kaka hadi cv na work experience
 
Back
Top Bottom