Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mbona hata facebook yaliandikwa hayo au kwakua hawawez kulipata server la fb
 
kwani hizo taarifa si wanazipata tu hadi wakamsumbue huyo CEO wa Jf? wangetakiwa kujiunga na Jf kisha wakaanza kusoma thread tu ingewasaidia ,mbona mimi napata taarifa zote ,alafu kingine sidhani kama kukamatwa kwa mkuu Maxence kuna husiana na kuminya uhuru wa maoni na kutoa taarifa kama watu wanavyoanza kujishuku humu ndani
 
Mbona commenti chache maana wanaopinga Uhuru wa Habari jukwaa lao kubwa ni hili hili, njooni na hapa mseme huyu anajisikia sana kuliko kukaa kimya. Ni vyema watu wakapewa Uhuru wa Habari kulingana na katiba ya nchi inavyotaka na si vingine.
 
acha uongo taarifa za makamu wa raisi kujiuzulu hazikuanzia humu zilikuwepo instagram kabla ya jf tena zilipostiwa na mange kimambi
 
Je,wanaweza kukufahamu vipi ili hali tunatumia ID fake? Naomba kujuzwa
 
Ndugu yangu hivyo ni vitisho. Hakuna vita iliyoletwa na vyombo vya habari, Rwanda chanzo cha vita ni Kutungua na kumuua Rais wa wakati huo Habyarimana; Kenya chanzo cha mapigano ni wizi wa kura na siyo vyombo vya habari kama unavyotaka kuaminisha umma. Angalia Burundi..... kwa nini Nkurunzinza kang'ang'ania madaraka?? Si ndo mwanzo wa kuleta vita na vurugu??? hapo utalaumu vyombo vya habari??? Popote penye haki huwezi kuona vita.
 
Weep not,child
Weep not,my darling
With these kisses let me remove your tears,
The ravening clouds shall no long be victorious,
They shall not long posses the sky,they devour the stars only on apparition.
By Walt Whitman.
Ngugi wa Thiongo alinukuu ubeti mmoja nakukipa jina kitabu chake cha
*WEEP NOT CHILD*
Ujumbe kuntu.
 
It is ok kwamba kwasasa jf inatikisa sii tz tuu bali dunia nzima, watawala matumbo joto! Kumbuka dogo hana kosa bali anatetea uhuru wangu na wako! Je sisi tunaotetewa tukae mimya? Nooo.
 
Siku hizi taarifa za wateja mtu analazimisha kuzipata, inanikumbusha kesi Kampuni Apple na Polisi wa Marekani.
 

ccm siku zote
 
Humu sio pakujiachia siku hizi zama zimebadilika..! pole Max kwa magumu unayopitia..
 
Kwa hyo tubakie jukwaa la mapenzi tu siasa na habari, hoja mchanganyiko bye bye babangu alisema watz hawapendi kuambiwa ukweli
 
Nje ya tz tunachekwa sana! Unajua wanasemaje? Ni kazi kwelikweli kumtetea mtz. Kwani hajui hata wanaomtetea na wanaomtafuna!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…