NAKEMBETWA
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 3,517
- 3,135
Wakuu naomba nijuzwe namna ya kupata hifadhi ubalozini ili usishtakiwe na nchi yako kama alivyofanya Julian Asange wa wikileaks?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanaweweseka na taarifa za ukweli zinazorushwa humu,humu ni zaidi ya kuongea jukwaani sasa mkubwa namba 1 hataki kukosolewa,hii ni aibu lakini wanatakiwa wajue huu mtandao no tofauti na wanavyofikiriaTuliwaambia... Akimaliza wanasiasa ataamia kwenu.
Mbona hata facebook yaliandikwa hayo au kwakua hawawez kulipata server la fbKuna uzi humu ulisema wazi na ushahidi kuwa Makamu wa rais amejiuzulu.
Kuna uzi humu ulipost barua ya ikulu ikionyesha nembo ya ikulu na sahihi ya msemaji wa ikulu ikielezea kutenguliwa kwa mrisho gambo. Huo sio uchochezi ? Au uchochezi kwako ni mpaka watu washike bunduki
acha uongo taarifa za makamu wa raisi kujiuzulu hazikuanzia humu zilikuwepo instagram kabla ya jf tena zilipostiwa na mange kimambiTofautisha kukosoa na kuleta habari za uchochezi.
Ingekuwa ni kukosoa JF ingekuwa imeshafungiwa muda mrefu sana. Lakini kwa kuwa kuna haki ya mtu kujieleza au freedom of speech ndio maana ipo mpaka leo.
Wanaotafutwa hapa ni wale wachochezi ambao ndio wamemponza maxence mello watu ambao ni chadema na kosa kubwa ni kuitumia JF kama Propaganda tool yao kueneza uchochezi.
Kama utakumbuka vizuri taarifa za kujiuzulu
Makamu wa rais zililetwa humu na pia ni humu humu JF ilitolewa taarifa ikiw na nembo ya ikulu
Pamoja na Sahihi ya msemaji wa ikulu
Ikielezea juu ya kutenguliwa kwa mrisho Gambo.
Hakuna nchi yoyote itakayovumilia uchochezi kama huo na hao ndio haswa wanaotafutwa na serikali Kwasababu aliyefoji amefanya kosa la jinai na anatakiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria na hao waovu ndio mello
Anawalinda.
Ndugu yangu hivyo ni vitisho. Hakuna vita iliyoletwa na vyombo vya habari, Rwanda chanzo cha vita ni Kutungua na kumuua Rais wa wakati huo Habyarimana; Kenya chanzo cha mapigano ni wizi wa kura na siyo vyombo vya habari kama unavyotaka kuaminisha umma. Angalia Burundi..... kwa nini Nkurunzinza kang'ang'ania madaraka?? Si ndo mwanzo wa kuleta vita na vurugu??? hapo utalaumu vyombo vya habari??? Popote penye haki huwezi kuona vita.JF ina rensponsibility kubwa sana, kama vivlivyo vyombo vingine vya Habari, kuna mambo mengi ya uongo na uzushi huletwa humu na kuachwa, ikumbukwe kwamba nchi nyingi kama Kenya, Rwanda, Burundi n.k Vita ililetwa na Vyombo vya Habari kama redio na TV, hivyo JF ina jukumu la kulinda amani ya nchi, kama ni kweli amekamatwa, na kama siyo kweli basi wajifunze na wabadilike, watambue jukumu lao kwenye Jamii!
CEO wa JF asipumbazwe na watu wanaosapoti kwenda kinyume na Serikali hapa, wengi wao wana maisha yao na wala hawaishi TZ, na JF ikifa kesho, au ofisi ya JF kunyimwa kibali cha kufanya kazi TZ hawana cha kupoteza, zaidi ya kuhamia kwenye mtandao mwingine na kuendeleza wanayoyafanya, hivyo angalia maisha yako na familia yako, fanya lililo sahihi na jinsi Serikali inavyokutaka kwani mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye nchi, watakushauri wanachama wa JF wanavyotaka lkn Serikali ndiyo wasimamizi wa hii nchi!
Labda Huyo ni MAJI marefu!Jitihada hizo wazielekeze kwa Mange Kimambi...
JF ina rensponsibility kubwa sana, kama vivlivyo vyombo vingine vya Habari, kuna mambo mengi ya uongo na uzushi huletwa humu na kuachwa, ikumbukwe kwamba nchi nyingi kama Kenya, Rwanda, Burundi n.k Vita ililetwa na Vyombo vya Habari kama redio na TV, hivyo JF ina jukumu la kulinda amani ya nchi, kama ni kweli amekamatwa, na kama siyo kweli basi wajifunze na wabadilike, watambue jukumu lao kwenye Jamii!
CEO wa JF asipumbazwe na watu wanaosapoti kwenda kinyume na Serikali hapa, wengi wao wana maisha yao na wala hawaishi TZ, na JF ikifa kesho, au ofisi ya JF kunyimwa kibali cha kufanya kazi TZ hawana cha kupoteza, zaidi ya kuhamia kwenye mtandao mwingine na kuendeleza wanayoyafanya, hivyo angalia maisha yako na familia yako, fanya lililo sahihi na jinsi Serikali inavyokutaka kwani mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye nchi, watakushauri wanachama wa JF wanavyotaka lkn Serikali ndiyo wasimamizi wa hii nchi!