Wakati viongozi wetu wakihangaika kupambana na watumishi hewa,ni vema pia wakaanza mchakato wa kuanzisha Taifa halisi la Tanzania,hii si nchi sahihi ni nchi hewa inayoongozwa na sheria hewa zenye double standard.
Kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita jeshi la polisi lilivamia na kuteka kompyuta za kituo cha sheria na haki za binadamu na zile za vijana wa ngome waliokuwa wanajumlisha kura za mgombea wa UKAWA kadiri walivyokuwa wakipokea matokeo kutoka kwa mawakala wa UKAWA nchi nzima.
Wakati polisi wakifanya utekaji wa kompyuta za vijana wa ngome na kutokomea nazo kusikojulikana,vijana wa Lumumba wao waliendelea na kazi kama hiyo katika vituo viwili tofauti huku kile cha Mlimani city kilichokuwa chini ya February marope,kikijipa jukumu la kutangaza matokeo ya mgombea wa CCM na bado hakikukaripiwa na yeyote achilia mbali kuvamiwa na kunyang'anywa kompyuta kama walivyofanyiwa vijana wa ngome wa UKAWA.
Kama lengo la jeshi la polisi ni kuzuia habari za uzushi,mbona hadi leo halijachukua hatua yoyote kwa yule aliyefoji tamko hewa la mahakama la kuzuia uchaguzi wa meya wa jiji la DSM?
Haiwezekani Taifa la watu milioni hamsini wote tuwe na mawazo na fikra zinazofanana,kama mnalazimisha watanzania wote wawe "wapiga push-ups",nani atamkosoa mwenzake pale push-ups zitakaposhindwa kukidhi mahitaji ya Taifa letu?
Basi kama ni hivyo tunaomba viongozi wetu watoe muongozo wa kitaifa wa namna ya kusema,kufikiri na kutenda ili Taifa letu liwe na maneno,fikra na matendo yanauofanana.Hapo ndipo vyombo vyetu vya dola vitakuwa na haki kumchukulia hatua yule atakayefikiri,kusema na kutenda kinyume na muongozo wa Taifa letu.
Tunaomba pia hata wimbo wa Taifa ubadilishwe,badala yake tuwe tunapiga push-ups kama kielelezo cha utii kwa viongozi wetu.