Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Watesi wetu wameamua kutufunga 'midomo" kabisa sasa sijui wanataka tutumie 'mikono' kuzungumza!
 
Hiyo ni kinadharia kwamba ninyi ndio wenye nchi lkn kiuhalisia hakuna kitu kama hicho Dunia hii!
Sasa naelewa haya yanayoendelea kama serikali inamawazo kama uliyo nayo. Naona giza tupu mbele.
 
Wakati viongozi wetu wakihangaika kupambana na watumishi hewa,ni vema pia wakaanza mchakato wa kuanzisha Taifa halisi la Tanzania,hii si nchi sahihi ni nchi hewa inayoongozwa na sheria hewa zenye double standard.

Kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita jeshi la polisi lilivamia na kuteka kompyuta za kituo cha sheria na haki za binadamu na zile za vijana wa ngome waliokuwa wanajumlisha kura za mgombea wa UKAWA kadiri walivyokuwa wakipokea matokeo kutoka kwa mawakala wa UKAWA nchi nzima.

Wakati polisi wakifanya utekaji wa kompyuta za vijana wa ngome na kutokomea nazo kusikojulikana,vijana wa Lumumba wao waliendelea na kazi kama hiyo katika vituo viwili tofauti huku kile cha Mlimani city kilichokuwa chini ya February marope,kikijipa jukumu la kutangaza matokeo ya mgombea wa CCM na bado hakikukaripiwa na yeyote achilia mbali kuvamiwa na kunyang'anywa kompyuta kama walivyofanyiwa vijana wa ngome wa UKAWA.

Kama lengo la jeshi la polisi ni kuzuia habari za uzushi,mbona hadi leo halijachukua hatua yoyote kwa yule aliyefoji tamko hewa la mahakama la kuzuia uchaguzi wa meya wa jiji la DSM?

Haiwezekani Taifa la watu milioni hamsini wote tuwe na mawazo na fikra zinazofanana,kama mnalazimisha watanzania wote wawe "wapiga push-ups",nani atamkosoa mwenzake pale push-ups zitakaposhindwa kukidhi mahitaji ya Taifa letu?

Basi kama ni hivyo tunaomba viongozi wetu watoe muongozo wa kitaifa wa namna ya kusema,kufikiri na kutenda ili Taifa letu liwe na maneno,fikra na matendo yanauofanana.Hapo ndipo vyombo vyetu vya dola vitakuwa na haki kumchukulia hatua yule atakayefikiri,kusema na kutenda kinyume na muongozo wa Taifa letu.

Tunaomba pia hata wimbo wa Taifa ubadilishwe,badala yake tuwe tunapiga push-ups kama kielelezo cha utii kwa viongozi wetu.
 
Hilo ni chaguo lake kama anataka kugeuka Mwanamapinduzi kwa ajili ya watu ambao wanasema watakuwa naye kiroho ni yeye tu ndo anapaswa kuamua, lkn maisha yamenifundisha mengi khs binadamu kwamba mwisho wa siku hakuna anayejali na utakuwa mwenyewe, lema ni mfano mzuri ukiondoa familia yake hakuna anayekosa usingizi kwa ajili yake hata Mbowe au Lowasa hawajakanyaga Arusha hata Tundu lisu ambaye ni Mwanasheria hajakanyaga Arusha kwa ajili ya Lema!
Unajua RAFIKI yangu hata Jammeh raisi wa Gambia walimwambia kuwa kuna siku utaondoka lkn yeye alikataa akasema ataitawala Gambia miaka bilioni 1 lkn zilipotimu unajua kilichotokea. Hivyo makaburi yatakuja kufukuliwa hata kizazi cha 4 kujibu tuhuma.
Naiambia serikali tends wema duniani tunapita.
 
Bado watanzania wengi hawajaelewa hii nchi inavyoenda, chagua kukaa kimya au familia na watoto watabaki wanalia
 
Mkuu kwenye kampeni maghufuli alisema hakuna mwanafunzi aliye na sifa atakosa mkopo na hilo alilitamka dodoma, lakini mbona kafanya kinyume? Je huoni kwa hata yeye Mwenyewe anakichanganya?
Mkuu jifanye kama hakumbuki ahadi zake inachotakiwa hapa useme wanafunzi wote walioomba mikopo ya elimu ya juu wamepata hakuna hata mmoja aliyekosa. Haya ndiyo maneno wanayotamka lizabon na wenzie hivyo wana uhakika na usalama wao
 
Afrika ikiendelea mimi nitachoma vyeti vyangu vyote kama bado nitakua hai. Tumerithi kila mbinu ya mkoloni katika kuendesha taasisi na Serikali dhidi ya koloni lake.

Serikali za kikoloni zilitumia mbinu za kukandamiza uhuru kwa makoloni yao na serikali zetu hivyo hivyo. Serikali za kikoloni zilijenga chuki, woga na hofu kwa makoloni yao, na hizi za sasa hivyohivyo. Serikali za kikoloni hazikuruhusu ubunifu na hizi hivyo hivyo. Serikali za kikoloni ziliweka ukuta kati yao na raia kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama, na hizi za sasa hivyohivyo. Kwa nchi zisizo na fikra za kikoloni, ubunifu kama wa JF ulipaswa kupata support zote kutoka Serikalini ikiwa pamoja na kutanua coverage yake. Kwani Facebook, Insta, Twitter zilianzaje hadi wahusika kuijengea sifa nchi yao?

Mtu kijijini huko anabuni kitu mfano wa bunduki, badala ya serikali kumpa sapoti, wanamkamata na kumuweka ndani. Yaani histotia haijabadilika na uhuru haujatusaidia.
 
duh kwani hii kitu si waliregister usa kama ni bongo hakuna namna ataacha kutoa majina hasa kwa sheria ya mtandao ni ovyo mno
 
Labda isiwe tz na africa ata ukimbilie kwenye ubalozi wa Vatican tutakufikia tu kwani izo balozi siziko ndani ya nchi zetu!
 
Mbona kukamatwa kitu cha kawaida kwa sisi wanaume...inshu ni kuto kujua kosa...bt kukamatwa kawaida...inawezekana ana kesi isiyo hisiana na JF
 
Mimi mwenyewe nilizisoma alama za nyakati nina wiki sijagusa siasa kabisa.
Thanks to my bae kwa kunikeep busy,saa hizi ningekuwa ktk hofu kubwa sana.
Siasa kwa sasa tuziache,hali ni mbaya.
Hahaaaa duuu mi nilifikiri una miaka mitatu miwili kumbe wiki daaa unanikumbusha mbaali hadithi ya tai aliyekuwa akifukuwa akifuzwa na adui kuona anakaribia kukamatwa akachimba kashimo kadogo kwenye mchanga na kuacha mwili woote nje huku akijua haonekani.
 
Back
Top Bottom