Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Asilimia 95 ya watumiaji wa JF wana ID fake. Serikali imeshatangaza kuwa kumiliki ID fake kwenye mitandao ya kijamii ni kosa la jinai. Sasa nyie wenye ID fake kiama kinakuja jiandaeni.

Mimi nipo clean.
Nitakuwa wa kwanza kuamini kuwa wewe ni mwongo
 
JF imetumika kumpigia kampeni Magufuli na kwa hakika ina mchango mkubwa kwenye kwenye sera ya CCM ya "kupinga ufisadi". Nadhani waliomkamata hawata sahau mchango mkubwa wa Max katika kukuza demokrasia na uhuru wa habari ambao bila kuwapo hata Lowassa asingejiuzulu Uwaziri Mkuu.

Free Max.
 
I'D zetu zinawahusu nini serikali badala ya kupambana kuwaletea wananchi maendeleo wanapambana kumnyima uhuru wa watumiaji wa mitandao kutoa maoni yao huu upuuzi kiwango cha lami.
 
Kumbe tanganyika inahitajika kupiganiwa uhuru wake mpya, kwa maana wananchi hawako huru kabisa. ..
 
MAWAZO YA KIPAYUMBU KABISA HAYA...KINYAA HADI KUSOMA...SIJUI KWANN UNAISHI DUNIANI MPAKA SASA
 
Lawama yooote iwaendee waliotuletea hii serikali. Wana CCM kwa haya yanayotokea Mungu anawaona.

Hongera kwa Mimi Mwanakijiji, Dr. Slaa, Lipumba, nk kwa kampeni zenu ili CCM ishinde ituletee haya yanayoendelea kwa sasa.

[HASHTAG]#BringBackBenSaananeAlive[/HASHTAG]
 
Wasije wakamfungia sandarusi na kumtupa baharini
 
Pole Max hivi ana kosa gani na atawajuwa wangapi mtandao ambao una member's toka Dar nzima ni maajabu kweli hivi watawala wanajuwa maana ya kunya maisha watu
 
Maxence Melo awe huru then mengine yafate ...very simple ...
 
Asilimia 95 ya watumiaji wa JF wana ID fake. Serikali imeshatangaza kuwa kumiliki ID fake kwenye mitandao ya kijamii ni kosa la jinai. Sasa nyie wenye ID fake kiama kinakuja jiandaeni.
Mimi nipo clean.

Kama sababu ndo hiyooo wakamkamate na Mack zu....
Maana fb id fake ni mingi.
 
Kuna watu mpaka Leo hawajui kwamba hawana akili .. na ukishapita umri flani basi akili ndo hupati tena hata ufanyeje
 
[emoji116]
 

Attachments

  • IMG_20161213_210921_383.JPG
    73.1 KB · Views: 41
Ikifungwa itabidi muhamie huko Facebook na Instagram.
 
sikusema kaitwa kwa tukio hilo,ila nilijiuliza mbona polisi kuna mambo mazito ya forgery hawayafanyii kazi kama hilo tukio la zuio feki la mahakama maana ile ilkuwa ni mockery of democracy na hilo suala limeisha kijuu juu tu as if nothing happened.
 
Watuache, JF ni sehemu pekee ya kutoa nyongo zoote. We ngoja Max akiachia majina lazima kuna watu watapozea ajira zao
 
Lumumba kwa dharau .... eti unauliza Melo ni nani wakati unamwaga upupu kwenye forum yake.
 
Sasa nimeamini kuwa tumeingia katika kipindi kingine cha ajabu sana katika demokrasia ya nchi hii. Tunaapa kwa katiba lakini tunaishi kwa hisia zetu. Hawa Polisi wanataka taarifa gani kutoka kwa Mello? Wanataka watufahamu? Kifungu cha katiba kinachoruhusu uhuru wa kujieleza kunalindwaje na serikali hii?

Tutafika tu ingawa hatujui tuendako!!!
 
Mh!! Serikali hujui kama inauwezo wa kuifungia facebook isiwe hewani Tanzania?
Hawana uwezo wa kuifunga facebook isiwe Tanzania kwa sababu kwa kufanya hivyo ni kukiuka uhuru wa habari wa kimataifa na adhabu yake ni kutengwa kimataifa ambapo kwa nchi masikini kama Tanzania ambayo haina uwezo wa kutengeneza chochote hata dawa ya malaria ni adhabu mbaya sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…