Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Jioni hii nilipata wasaa wa kuongea na rafiki yangu mmoja, yeye kazi zake ni zile "maalum" huko ukudani.
Kanidokeza kuwa "majamaa" wamepanga kuifungia JF.
Lets wait and see...!
Itabidi jamaa aondoke na serve yake akakae marekani
 
Hata mimi napenda sana Maxence Melo apate dhamana haraka.

Ninatumaini polisi na uongozi wa Jamiiforums watafikia muafaka nje ya mahakama.

Changamoto iliyopo kwa uongozi wa jamiiforums ni namna ya kufuatilia mijadala hapa JF hasa ikichukuliwa kuwa kwa sasa wanachama wamekuwa wengi lakini michango yao niya udaku, kifacebook au instagram.

Nimejaribu kufuatilia mnachoongea msemajiukweli na Richard kutokana na uwezo wenu wa kujenga hoja na uzeofu wenu hapa jukwaani. Ninachokiona kutoka kwenu ni kama upotoshaji wa aina fulani hivi aidha kwa kujua ama kwa kujua labda kwa kuwa na agenda nyuma ya pazia. Mnataka tuamini tatizo la Melo kutakiwa kutoa taarifa za watumiaji hapa ni michango ya kidaku, facebook na instagram. Napenda niwaambie hilo sio lengo bali lengo ni zaidi ya hilo. Kama ingekuwa hao polisi wanakereka na hizo tabia za kidaku basi kuna magazeti mengi tu ya udaku yangekuwa yameshafungiwa. Kama ni hizo tabia za facebook na instagram sio kweli maana sasa hivi tunaona vijana wakitembea wamevaa suruali chini ya makalio, wamesuka nywele, kuvaa hereni na mashoga wengi tu. Mabinti ndio usiseme wanatembea nusu uchi na hakuna polisi anayewakamata zaidi ya jamii kusema eti maadili siku hizi yamebadilika.

Lengo kabisa ni kupata ni akina nani wanaovujisha mambo ya kweli ambayo yanawakera watawala na wasingependa yaanikwe. Kumbuka kuna watu wanahoji mambo ambayo kwa serekali ni mwiba kuyatolea majibu hivyo hao ndio wanashida nao na wala sio hao wanaotukana, wala hoja za kifacebook. Kumbuka bunge lengu lina utaratibu wa kuhoji ila wanatumia kitu kinaitwa lugha ya kibunge, ni ukweli ulio dhahiri wabunge walio wengi wanahoji kiitikadi na kujiona ni sehemu ya serekali, hivyo serekali hujibu inavyotaka na mizengwe kibao. Wabunge walio wachache wanauwezo wa kuhoji bila hofu lakini uchache wao hauwapi nguvu ya kufurukuta. Kumbuka kwa bunge la sasa speaker ni kama anaongozwa kwa remote toka sehemu fulani. Katika mazingira hayo ni lazima atafuata huyo muongoza remote anachotaka. Eneo pekee watu wanapoweza kuhoji na kutapika nyongo zao bila hofu ni huku kwenye mitandao ya kijamii. Sasa hao wanaotapika nyongo na kuweka kila kitu hadharani haswa ndo wanaotakikana. Wengi tunajua sio lazima tuwe wote, lakini hiyo sheria ya mitandao ni kama ilipitishwa kiitikadi tena kwa lengo la kukomoa watu fulani, na haswa ni wale walio na mtazamo tofauti na serekali iliyoko madarakani. Kwa hiyo ndugu zangu nawaheshimu sana ila mnachofanya ni upotoshaji wa wazi na wala sio kwamba eti waliojiunga siku za karibuni au sijui waliojiunga zamani, japo kweli kuna mapungufu ya kufanyia kazi kwa mods na sio kutaka details za members.

Tuwe wakweli tu japo ni ngumu kukiri lakini utawala wa sasa hauna uvumilivu wa kusikia ukweli. Ila mjue ni hatari sana kama itafikia mahali watu hawamwagi nyongo zao kama huku jukwaani. Huko tuendako kila mtu atakuwa amekuwa muoga, na hapo ndio utashangaa watu wataanza mara kurekebisha katiba ili sijui mtu akae madarakani muda zaidi kwani anakubalika na watu. Huwa haya mambo yanaanzaga taratibu na watu wema wataingizwa mkenge wadhani wanachokiona ndio hicho, wakija kujua rangi halisi inakuwa hawana uwezo wa kuhoji kwani majukwaa yanayopiga kelele kama haya yatakuwa yalishabanwa. Dalili zote ziko wazi na kama hamuamini ngoja hili lifanikiwe, nakupa miaka miwili ijayo tutaongea mengine wengine wakiwa jela.

cc: Richard, Bethlehem, ngururuvi3, the boss, technically, pasco, joka kuu, gamba la nyoka, kimweri, mzee mwanakijiji
 
Hivi ushajiuliza ni matukio mangapi yanatokea nchi nzima kuingku na polisi inabidi wadili nayo. Mambo mazito ya forgery kama yapi? Hivi unajua kuwa mumewe yule kajala masanja muigizaji mpaka leo hii yupo jela kwa ajili ya gorgery. Hujiulizi kina shose sinare na sioi sumari wako rumande na moja ya kosa lao ni forgery.

Mnachotetea ni hawa wahalifu wanaharibu taswira ya JF wasichukuliwe hatua wao ni kina nani?

Inawezekana isiwe ni approach nzuri kumkamafa maxence mello na kumlaza ndani ila kesi ya msingi hapo ipo.

Information za wale wavunjifu wa amani wanapost matamko ya kufoji ya serikali lazima zitolewe na wachukuliwe hatua ili ku maintain Law and Order.
Ndio maana kuna wahariri na wakiona hakuna ukweli huwa wananondoa taarifa hiyo mapema,
Ni kazi ngumu sana kushindana na technology
 
Hivi ushajiuliza ni matukio mangapi yanatokea nchi nzima kwa siku na polisi inabidi wadili nayo. Mambo mazito ya forgery kama yapi? Hivi unajua kuwa mumewe yule kajala masanja muigizaji mpaka leo hii yupo jela kwa ajili ya gorgery. Hujiulizi kina shose sinare na sioi sumari wako rumande na moja ya kosa lao ni forgery.

Mnachotetea ni hawa wahalifu wanaharibu taswira ya JF wasichukuliwe hatua wao ni kina nani?

Inawezekana isiwe ni approach nzuri kumkamafa maxence mello na kumlaza ndani ila kesi ya msingi hapo ipo.

Information za wale wavunjifu wa amani wanapost matamko ya kufoji ya serikali lazima zitolewe na wachukuliwe hatua ili ku maintain Law and Order.
Faida za jamii forum ni kubwa ×1000 kuliko hayo machache ambayo yanawakera watu fulani fulani
 
Very bad. Haya yote yana mwisho. Hiki kizazi cha kisomi hatutakubali wahuni wachache wateke fikra za watu.........KM UCHUMI UNAPAA NA WATZ WANAPATA HUDUMA ZOTE MUHIMU KM CCM WANAVOSEMA HII HOFU YOTE YA NN?
 
Watanzania mara nyingi hatu fikirii madhara ya sheria zinazotungwa huwa tunagawanywa kwa misingi ya kichama au ya kidini ,hii ni moja ya sheria ambayo tunge simama pamoja isinge pita,lakini tutajuta siku ikifungiwa chombo kama hiki na serikali.
 
Hivi mfano tukibunia au kukisia, hawa Polisi walikua wakiomba taarifa za watu kama kina nani hasa??
Yaani taarifa za kina nani hasa zilitakiwa Polisi hadi kuamua kuwekana ndani??
Ni verified Members??
Ni [HASHTAG]#TeamLumumbaBk7[/HASHTAG]??
Ni Makamanda??
Ni kina nani hawa wanaotakiwa kwa udi na uvumba na hao Polisi??
Aisee hapa unaweza ukajikuta kwenye list umo?
Naona sasa hii imekuwa shule...
Naona majina ya wakarofi sugu wameolozeshwa.
 
Kimenuka! Sasa ni Mwendo wa comment za kupongeza tu!

Tunaunga Mkono Jitihada za Mh. Rais kwa kukuza Uchumi na kurejesha Uadilifu na nidhamu Serikalini!
ndugu yangu jamii media ndo inageuzwa kuwa kampuni tanzu ya uhuru media
 
Hivi atakubali kweli tumbadilishe mwingine baada ya miaka yake mitano? Naona kama sasa amezidi, hataki kukosolewa, kusemwa vibaya, mbona katika jamii zetu sijawahi kuona mtu anasemwa kwa mazuri tu, hata ufanye mazuri mwingine anaweza kuona ni mabaya kwa mtazamo wake, yani leo wote tuwe na mtazamo sawa inawezekana kweli? Mbona mke kila mtu anachagua anayempenda iweje kwa kiongozi kulazimishana kumpenda wote?!!!! anyway duniani kuna kuzaliwa na kufa, yote ni maisha, hakuna atakayeishi milele, Hitler alikua mbabe kweli lakini mwisho wa siku alikufa.
Mimi huwa naogopa sana watu wanaotaja taja sana jina la Mungu. Mara nyingi huwa ni wanafiki
 
Jamani endapo kama huyu jamaa watamtesa sana,
Ili awape ushirikiano na akawapa,
Tafadhali jamani watakao kamatwa watujulishe.

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
nikiangalia kwa mbali swala la mama kuhamisha fuso la mchanga ndilo lililozaa haya yote, sasa vinatafutwa vyanzo vya habari
 
Hii ni kuwatisha wavujishaji wa taarifa za serikali.

sisi mbele kwa mbele,hatunywi sumu x8
 
Hivi ushajiuliza ni matukio mangapi yanatokea nchi nzima kwa siku na polisi inabidi wadili nayo. Mambo mazito ya forgery kama yapi? Hivi unajua kuwa mumewe yule kajala masanja muigizaji mpaka leo hii yupo jela kwa ajili ya gorgery. Hujiulizi kina shose sinare na sioi sumari wako rumande na moja ya kosa lao ni forgery.

Mnachotetea ni hawa wahalifu wanaharibu taswira ya JF wasichukuliwe hatua wao ni kina nani?

Inawezekana isiwe ni approach nzuri kumkamafa maxence mello na kumlaza ndani ila kesi ya msingi hapo ipo.

Information za wale wavunjifu wa amani wanapost matamko ya kufoji ya serikali lazima zitolewe na wachukuliwe hatua ili ku maintain Law and Order.
Kwa mfano,tamko la kufoji la serikali ni lipi?
 
Back
Top Bottom