Hata mimi napenda sana Maxence Melo apate dhamana haraka.
Ninatumaini polisi na uongozi wa Jamiiforums watafikia muafaka nje ya mahakama.
Changamoto iliyopo kwa uongozi wa jamiiforums ni namna ya kufuatilia mijadala hapa JF hasa ikichukuliwa kuwa kwa sasa wanachama wamekuwa wengi lakini michango yao niya udaku, kifacebook au instagram.
Nimejaribu kufuatilia mnachoongea msemajiukweli na Richard kutokana na uwezo wenu wa kujenga hoja na uzeofu wenu hapa jukwaani. Ninachokiona kutoka kwenu ni kama upotoshaji wa aina fulani hivi aidha kwa kujua ama kwa kujua labda kwa kuwa na agenda nyuma ya pazia. Mnataka tuamini tatizo la Melo kutakiwa kutoa taarifa za watumiaji hapa ni michango ya kidaku, facebook na instagram. Napenda niwaambie hilo sio lengo bali lengo ni zaidi ya hilo. Kama ingekuwa hao polisi wanakereka na hizo tabia za kidaku basi kuna magazeti mengi tu ya udaku yangekuwa yameshafungiwa. Kama ni hizo tabia za facebook na instagram sio kweli maana sasa hivi tunaona vijana wakitembea wamevaa suruali chini ya makalio, wamesuka nywele, kuvaa hereni na mashoga wengi tu. Mabinti ndio usiseme wanatembea nusu uchi na hakuna polisi anayewakamata zaidi ya jamii kusema eti maadili siku hizi yamebadilika.
Lengo kabisa ni kupata ni akina nani wanaovujisha mambo ya kweli ambayo yanawakera watawala na wasingependa yaanikwe. Kumbuka kuna watu wanahoji mambo ambayo kwa serekali ni mwiba kuyatolea majibu hivyo hao ndio wanashida nao na wala sio hao wanaotukana, wala hoja za kifacebook. Kumbuka bunge lengu lina utaratibu wa kuhoji ila wanatumia kitu kinaitwa lugha ya kibunge, ni ukweli ulio dhahiri wabunge walio wengi wanahoji kiitikadi na kujiona ni sehemu ya serekali, hivyo serekali hujibu inavyotaka na mizengwe kibao. Wabunge walio wachache wanauwezo wa kuhoji bila hofu lakini uchache wao hauwapi nguvu ya kufurukuta. Kumbuka kwa bunge la sasa speaker ni kama anaongozwa kwa remote toka sehemu fulani. Katika mazingira hayo ni lazima atafuata huyo muongoza remote anachotaka. Eneo pekee watu wanapoweza kuhoji na kutapika nyongo zao bila hofu ni huku kwenye mitandao ya kijamii. Sasa hao wanaotapika nyongo na kuweka kila kitu hadharani haswa ndo wanaotakikana. Wengi tunajua sio lazima tuwe wote, lakini hiyo sheria ya mitandao ni kama ilipitishwa kiitikadi tena kwa lengo la kukomoa watu fulani, na haswa ni wale walio na mtazamo tofauti na serekali iliyoko madarakani. Kwa hiyo ndugu zangu nawaheshimu sana ila mnachofanya ni upotoshaji wa wazi na wala sio kwamba eti waliojiunga siku za karibuni au sijui waliojiunga zamani, japo kweli kuna mapungufu ya kufanyia kazi kwa mods na sio kutaka details za members.
Tuwe wakweli tu japo ni ngumu kukiri lakini utawala wa sasa hauna uvumilivu wa kusikia ukweli. Ila mjue ni hatari sana kama itafikia mahali watu hawamwagi nyongo zao kama huku jukwaani. Huko tuendako kila mtu atakuwa amekuwa muoga, na hapo ndio utashangaa watu wataanza mara kurekebisha katiba ili sijui mtu akae madarakani muda zaidi kwani anakubalika na watu. Huwa haya mambo yanaanzaga taratibu na watu wema wataingizwa mkenge wadhani wanachokiona ndio hicho, wakija kujua rangi halisi inakuwa hawana uwezo wa kuhoji kwani majukwaa yanayopiga kelele kama haya yatakuwa yalishabanwa. Dalili zote ziko wazi na kama hamuamini ngoja hili lifanikiwe, nakupa miaka miwili ijayo tutaongea mengine wengine wakiwa jela.
cc: Richard, Bethlehem, ngururuvi3, the boss, technically, pasco, joka kuu, gamba la nyoka, kimweri, mzee mwanakijiji