Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Wewe unaonekana exposure ni zero minus,hujui hata mwelekeo wa dunia
Usidhani wewe ndio mwenye uelewa na ufahamu mkubwa kuliko wote unapata nafasi ya kujadiliana nao, ukijifunza kuwa na hekima itakusaidia.
 
inaumiza sana ukiiwazia, na kuisikia, lakini wamekuja watu wengi kuijaza hii thread na sumu mbaya. naogopa nchi yangu inakoelekea
 
Zamani kulikuwa hakuna udikteta uchwara,zmani hakuna alietamani malaika waje wazime mitandao,zamani tulikuwa tuna bunge live,zamani mikutano ya siasa haikufutwa.......kwa hyo usituletee hadithi zenu za lumumba wanafki wakubwa nyie mnataka msifiwe tu.
Walidhani hapa ni bunge live
 
Unataka tumweshimu yy tu kwan yy amemheshimu nani. TOKA ZAKO HAPA
 
- Tunajenga Taifa so wananchi mchana mzima wanatakiwa kuwa kazini sio kuangalia Bunge live, hayo mengine ya kwako na ni nonsense!

le Mutuz
Mkuu,

Kwa nini matangazo ya bunge yalikuwa mubashara "in the first place"? Je, ni kweli kwamba matangazo hayo kuwa mubashara yalichangia kushuka uchumi wetu au watu kuacha kutimiza wajibu wao makazini na maeneo mengine?

Kaka ...
 

Sina haja ya kubishania ujinga.
 
Hakuna shida - MELO hatulazimishi jeshi la polisi kusoma JF
 
Tunaamini haki itapatikana kwa Max Melo, MUNGU mwenye HAKI atamsimamia.
Tunaelezwa JamiiForums.com haina uwezo wa kumtambua kila mtumiaji wa mtandao huo kwasababu ya mfumo wanaotumia ama mtumiaji mhusika aamue mwenyewe kutoa utambulisho unaofahamika kwa wengine kama kutumia jina halisi. Tumeona wengi wanatumia majina ambayo si halisi ukiwa wewe Jick na wengine wengi. Kwa mfumo huo, mtu anayejisajili halazimiki kutoa particulars ambazo zinaweza kum-link mhusika (by using real names, phone numbers etc.) ndiyo maana wengi wanaamua kutumia majina ambayo si halisi. Lakini tukumbuke kuwa watumiaji wengu wa mtandao huu ni watu tofauti wakiwepo viongozi nyeti katika serikali ambao pengine anadhani hana sehemu ya kusemea, analazimika kuja JF. Hata wale ambao wanatumia majina halisi inaaminika kuwa nao wana accounts zisizo na utambulisho unaofahamika pia.
Haya yanatokea kwakuwa watu wanakosa uhuru wa kuongea, kwani hata kama kinachozungumzwa si cha kweli kwani shida iko wapi..?? Toka mbele kanusha with facts! Ndivyo mataifa yote yanavyofanya kazi, hii inatufanya tuzidi kurudi nyuma zaidi. Serikali kuhangaika na JF na kutumia nguvu nyingi ni kukosa maarifa ya kufanya kazi. JamiiForums iko miaka mingi mno, why leo yanatokea haya?? Non-sense kabisa!
 
Wakuu,

Taarifa mpya ni kwamba, Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo mpaka muda huu bado anashikiliwa na polisi na hajafikishwa Mahakamani kama sheria inavyotaka.

Alifanyiwa mahojiano jana usiku kwa muda mrefu na faili lake limechukuliwa linapelekwa kwa DPP mchana huu.

Bado mashtaka halisi yanayomkabili hayajawekwa wazi.

Taarifa zaidi kukujia...
 
Eeeh, Mola wetu, kila ajae kwa shari, waijua yake siri, ivunje yake dhamiri asiweze kusimama! wote natuseme amin!
 
Aluta Continua!

Kaka ...
 
Mpaka leo bado anahojiwa?
 
Melo ushauri wangu ukishatoka hamishia kazi zako Kenya, nenda kafungue ofisi na kazi zifanyike pale, ili tuwe tunafunguka sawasawa, hapo utapigwa zengwe mpaka basi,
 
Kama taifa, tunayumba na kupotea mwelekeo sana. Mungu wa rehema kawajaze viongozi wetu hekima na busara katika haya yanayotukumba kama taifa. Kazuie ombwe la uongozi ktk taifa letu ili hatimaye maoni na tuhuma ziibuliwazo na wananchi zikasaidie serikali kuchunguza watuhumiwa na kuwashughulikia badala ya mtoa/ mwibua taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…