Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Watakuwa wanataka IP. Address za watu lakini wanasahau kuna kitu kinaitwa VPN na wengine wanatumia shared WiFi

Unless kuna jambo lingine
 
Naona na wewe unajiongeza kwenye list ya wanao tafutwa teh teh!
 
vijana wenzangu tunaopenda/mnaopebda ku-comment kimuhemuko kuhusu masuala yanayohusu watawala,sasa muanze/tuanze kujitafakari upya.

yaonekana mamlaka inatutafuta sana watukamate ili tufunguliwe mashtaka.

tumshukuru sana maxence melo kwa kushikiria msimamo na tumuombee asibadilike maana na yeye ni binadamu.

vinginevyo saa hii wengine mngekuwa/tungekuwa lupango tunanyea debe.
 
Hii serikali ya mtukufu aliye tukuka Raisi wa maraisi haijashindwa. infact imeimarisha uchumi na kujenga viwanda, na sasa inanunja ndege kibao ili wananchi muanze kutumia ndege na sio mabasi tena.
hahahaha
 
tatizo ni kubwa kuliko nlivofikiri...
Hapana ni kwamba Tatizo linakua siku baada ya siku. Na mbaya zaidi ni kua Wasema ukweli ndio wanao tafutwa na sio watukanaji au wanao weka picha za uchi.
 
Hakika kwa sasa hatupo Salama... Taa nyekundu hiyo....
 
Nahisi walikuwa wanataka taarifa za Mange Kimambi.. Si wamfyate huko huko USA? Kwan lazima wamkamate Water Mellon?
 
Ila kuna kesi jf ilishinda kuhusu hii kutoa taarifa sijui nini kiliendeleaga Retired
 
Mbona kulikua na kesi mahakaman na JF walishinda kwa hizo ishu za polisi kutaka axcess ya database ya jamii forums.
 
Hawa Chadema wamesababisha hayo yote maana wao ni wazee wa kuongea kila neno wanalojisikia na wala bila heshima wala adabu kwa dola inayotuongoza. Kwa mtindo huu JF itafungwa kwa Sababu ya hilo.
Sio kila anayetoa mawazo ya tofauti na kupinga ni CHADEMA wewe,wengine ni watu wasio na itikadi yoyote ile.Ns wengi ni CCM.
Na bado tutakoma
2020 amka mtanzania,mbona Gambia wameweza!

Lissu alisema, sasa yanatokea na kuna mdau humu alishasema kuwa ipo siku watu wote watamkumbuka Lissu kwa kile anachopigania.
 
Kwa hyo police wanataka information za members WA jamii F au nn ? Cjui akitoka hapo ataenda wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…