Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.

Polisi wanaeleza muda huu kwamba leo atalala ndani hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.

Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. Maxence ameendelea kushikilia msimamo kuwa ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi kufanya hivyo.

Taarifa zaidi baadaye
.mbona sisi huku jf tunatumia majina feki tupu au ndio mtatukamata hivyohivyo.
 
Sasa utawalazimisha watu wanyamaze kweli? Mh mbona Tanzania ngumu sana hii
 
Vigezo na masharti inabidi kuzingatiwa ili twende na sheria mpya ya magazeti na ile ya mitandao
kusema ukweli humu JF mazombi tupo wengi mno inabidi uongozi ili ujichomoe na kadhia hii ni muhimu wote kuwa verify our names na adress kwa ujumla wake
kama kweli hatuna nia mbaya,
Kwa haya masharti wengi watajitoa wahamie huko Instagram.
Vita ya kupambana na social media ni ngumu.
 
Issue tunetakiwa kukamatwa sisi yeye akataaa kuwapa ubuyu wa mahali tuipo!!!! L000h.........Ngoja habari hizi nizifikishe kijijini kwao wahaya wote waandamane
 
Duhhh kweli uhuru wa habari ni Zero kabisa Tanzania .
Badala ya kuchunguza miili saba ya watu walio uawa na kutafuta wauwaji. Mko busy kukamata watu wasio na kosa.
Mapolice wa Tanzania kweli mmekosa kazi.

Shame on you .
 
Hivi atakubali kweli tumbadilishe mwingine baada ya miaka yake mitano? Naona kama sasa amezidi, hataki kukosolewa, kusemwa vibaya, mbona katika jamii zetu sijawahi kuona mtu anasemwa kwa mazuri tu, hata ufanye mazuri mwingine anaweza kuona ni mabaya kwa mtazamo wake, yani leo wote tuwe na mtazamo sawa inawezekana kweli? Mbona mke kila mtu anachagua anayempenda iweje kwa kiongozi kulazimishana kumpenda wote?!!!! anyway duniani kuna kuzaliwa na kufa, yote ni maisha, hakuna atakayeishi milele, Hitler alikua mbabe kweli lakini mwisho wa siku alikufa.
Magu hausiki hapa
Sheria ya mitandao imepitishwa ns bunge Magu si Rais
Hilo mlifahamu,
Watu wanapost habari za uzushi bila kuangalia athali zake kwa jamii.

Hii inaleta maana kuwa
Unapo leta uzushi ujue sheria IPO
Uwe tayali kukabiriana na sheria husika.
 
Melo yuko salama..wala hakuna jambo jipya kaitwa kuhojiwa tuu.
Lakini walio sababisha kuitwa kuhojiwa ni wale waleta habari za uzushi ambazo serikali inalazimika kuhangaika kuzikanusha kila leo...
sheria ile ya mitandao ina ipa mamlaka polisi kupata taarifa za mtu kutoka kwa mtu na inawezekana hata kuchukua vifaa husika...
Melo yuko salama salimini.



Pale mtu wa Lumumba unapojifanya unafahamu kila kitu kutoka kwa mkoloni mweusi.Badala ya kuhangaika na jf ni vema wakaanzisha forum yao ambayo watakuwa wanaimoderate wenyewe huko polisi nasi tutajiunga na kuendelea kutoa michango yetu kama tutoavyo hapa jf.

Kwa mwendo huu huko tuendako wengi sana tutafungiwa kwenye mifuko ya sandarusi na kutoswa baharini,maana kila fursa iliyopo tuwezayo kupeleka vilio vyetu juu ya serikali hii inalazimishwa kufungwa ili Taifa liendelee kuimba wimbo wa sifa hata katika mambo yanayohitaji ukosoaji.
 
Yote juu yako
Lakini hoja kubwa ni kuleta habari ya maana na sio kuzusha zusha habari za uongo ili kuchochea watu,
Kamwe haliwezi kubalika
Na ni nani atang'amua kua hii taarifa au habari ni uongo uongo!? Kama serikali ina nia njema kwanini isikamate mashoga wanao jiuza FB!? Lengo hapa ni kutoa Taarifa zitakazo msifia na kumtukuza mtukufu.
 
Malaika ameshashuka kuzima mitandao ya jamii.

Pole sana Maxence Melo, Lissu alisema ni wasaa wa kumpinga popote huyu mtu lakini nadhani watanzania hatukuelewa na bado hatujaelewa.
 
Magu hausiki hapa
Sheria ya mitandao imepitishwa ns bunge Magu si Rais
Hilo mlifahamu,
Watu wanapost habari za uzushi bila kuangalia athali zake kwa jamii.

Hii inaleta maana kuwa
Unapo leta uzushi ujue sheria IPO
Uwe tayali kukabiriana na sheria husika.
Magu ndo nani? wapi nimemtaja huyo Magu wako?
 
Hapa hatuko safe kabisa. Inshaalah atapata haki yake .ndo maana wanataka na whatsapp group zisajiliwe maana mtu akileta Umbea tu. kiongozii unakamatwa. kitukuzwe chama cha maendeleo.
 
Back
Top Bottom