Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa jamii forums amekamatwa na jeshi la polisi, kituo cha kati Dar.

Polisi wanaeleza kuwa kesho atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka.

Ni kuhusu makosa ya mtandao. Polisi wamekuwa wakishinikiza awape majina ya watu wanaowahitaji kutoka mtandao wa jamii forums.

Kesho atapanda kizimbani.

Taarifa zaidi baadaye.

Niko polisi kati bado.
Copy and paste
Copy and paste from wapi?
 
Vigezo na masharti inabidi kuzingatiwa ili twende na sheria mpya ya magazeti na ile ya mitandao
kusema ukweli humu JF mazombi tupo wengi mno inabidi uongozi ili ujichomoe na kadhia hii ni muhimu wote kuwa verify our names na adress kwa ujumla wake
kama kweli hatuna nia mbaya,
 
Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.

Polisi wanaeleza muda huu kwamba leo atalala ndani hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.

Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. Maxence ameendelea kushikilia msimamo kuwa ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi kufanya hivyo.

Taarifa zaidi baadaye
mama weee ,,,, walikuwa wananitafuta mimi hivyoo
 
Back
Top Bottom