Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Kumbe michango yetu inasomwa mpaka sentlo na ikulu,haya ngoja nitume salam kwa wakulu woote mlio sentlo na pale ikulu vipi familia zenu zinaendeleaje,?.Hebu tuelezeni lengo lenu hasa nini,whats your end game?,hivi roho zenu haziwasuti mnavyo watenda wenzenu ndivyo sivyo?au mnadhani mtaishi milele,haya nyie endeleeni tu.ila kumbukeni walikuwapo ma bwanawakubwa kibao enzi hizo na wakawahenyesga watu vya kutosha,leo wako wapiii.yuko wapi hitler,franco,musolini,savimbi na wengineo.endeleeni tu
 
Naona sasa malaika kashaanza kushushwa kuifungia mitandao ya kijamii.

Iwa hao malaika na aliewatuma afahamu kuwa ni ngumu sana kuzuia mafuriko kwa mkono.

Nao hao malaika wanahitaji pia social media kusemea mema yao.

Yanamwisho.. ila huwezi zuia mafuriko kwa kutumia kiganja cha mkono.

Malaika anaongea kisukuma teh teh teh vituko vya hawamu ya vituko
 
Jamani tupeni updates

Mod jitahidin kutupa taarifa rasmi kwa wakati sahihi

JF ni kimbilio la wengi wasio na sauti (at least ilikuwa hivyo)
 
Huu ujumbe utafutwa muda si mrefu!

Tukisema kuna watu elimu zao hazitoshi mtatuambia sisi ni wachochezi au tunajidai! Nilishasema na nasema tena kuwa kati ya idara zinazotakiwa kuwa na watu wa kila aina hasa katika dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia, wakiwemo wataalamu waliobobea katika fani za kijasusi ukiwemo ujasusi wa kiteknolojia ni Idara ya Polisi/Usalama wa Taifa. Ujasusi huu sio tu kuvizia na kukamata data za watu wanaopingana na serikali au kufanya makosa mbalimbali kwa njia ya mtandao bali ni pamoja na kuiba teknolojia (hasa soft technology), siri, mbinu na maarifa mbalimbali kutoka watu au mataifa mengine ulimwenguni. Usitegemee kuendelea kwa kujifunza tu na kwamba ipo siku utawakamata wenzako ambao wako mbali kutoka kwako mamilioni ya kilometers bila kutafuta mbinu za kuiba maarifa yao.

Je, ni kweli polisi wameshindwa kabisa kuhack servers za JF kiasi cha kuamua kumkamata jamaa "red-handed" ili awape data za watumiajia wa jf wanaowatafuta kwa mkono wake, au awape logins waingie na kupekua?

Je, kama hamuwezi kuhack server kwa nini msikodishe wataalamu, "hackers" waliojaa kila kona ya dunia? Hao jamaa ukiwaahidi hela hawafanyi makosa, ni asubuhi wanakupakulia database za jf: majina, ip addresses, user log files, geographical locations na info zingine muhimu.

Nendeni deep web, watu wanashindana kuhack sites kama vile kubet au kushangilia soccer la ligi za England! Au kodisheni makampuni kama vile Cellebrite - mamafia ya Kiisrael ambayo yamebobea kuhack, kuanzia simu mpaka kitu chochote ambacho ni connected na web.

See more: 10 Best Hackers The World Has Ever Known.

Hakuna profession tamu kama hacking!
 
Kinachonishangaza ni pale matusi kashifa dharau kejeli zinapofanywa na viongozi kuanzia Ikulu mpaka kwa wakuu wa wilaya na mikoa na mawaziri kwa wananchi lakini wao hawapendi kuambiwa kitu
 
Kwa nchi ambayo hata rais ni kituko ni lazima mambo meng yashangaze
Halafu bado mnadhani mtaendelea kujificha kwa anuani bandia, kwa upuuzi kama huu,! Unaposhindwa kumheshimu rais wa Nchi yako unayeweza kumpa heshima ni nani ? Katika maisha yako??
Biblia inasema tiini mamlaka iliyo kuu sabbu hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu. !!! Halafu kwa kebehi na dharau zenu mnataka Nchii iendelee kuwaangalia tu,! Kwa kisingizio cha uhuru wa maoni na kukosoa.!
Haiwezekani na halitawezekana.
 
Halafu bado mnadhani mtaendelea kujificha kwa anuani bandia, kwa upuuzi kama huu,! Unaposhindwa kumheshimu rais wa Nchi yako unayeweza kumpa heshima ni nani ? Katika maisha yako??
Biblia inasema tiini mamlaka iliyo kuu sabbu hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu. !!! Halafu kwa kebehi na dharau zenu mnataka Nchii iendelee kuwaangalia tu,! Kwa kisingizio cha uhuru wa maoni na kukosoa.!
Haiwezekani na halitawezekana.
Wewe unaonekana exposure ni zero minus,hujui hata mwelekeo wa dunia
 
- Ok tatizo ni kwamba Wanasiasa wetu nao wanatuvuruga sana kwa mfano USA hivi karibuni Uchaguzi umeisha Mama Clinton kampigia simu Trump kumpongeza kwa ushindi, na siku tatu baadaye Mama Clinton kakubali mbele ya umma kwamba kashindwa na kuwataka wananchi wajiunge nyuma ya Trump kwa masilahi ya Taifa case closed.

- Sisi unajua sihitaji hata kurudia ni huzuni tupu, mgombea aliyeshindwa eti anataka kufanya ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kushindwa haijawahi kutokea Duniani, sasa for that unataka Mtawala mpya afanye nini? WATanzania wote tufike mahali tubadilike kwa manufaa ya Taifa,

le Mutuz
Hawawezi kukuelewa sabbu wanalipwa kwa propaganda zao za kipuuzi na wanajifanya kama sio raia wa Nchi hii.
 
QUOTE]

Sasa kwanini unamtisha binadamu mwenzako hivyo?! Alichosema Nyaluhusa87 kwani hiyo wish ya kwamba malaika waje wafungie mitandao mpaka maendeleo yatakapofanywa haijawahi kusemwa in public?!
Tena unamtishia mwenzako na familia yake kabisa! Muogopeni Mungu jamani!!!!
Sio rahisi sana kuki kimbia kivuli chako,! Hakuna anayemtisha kama alichokidhamilia ni sahihi.
 
Back
Top Bottom