Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Mkuu kwa hilo la utunzaji nakubaliana nawe 100%. Ila vitu kama maji si vya kuzuia kabisa, na hata wakizuia waviuze kwa bei ya soko, hao abiria wengi wao ni akina sisi pangu pakavu.
 
Shangazi kaja halitoshi ile sehemu ya kuwekea mizigo unaweka hatarini maisha ya abiria aliyechini...
 
Taasisi Ona wasemaji

Tusipoteze muda kusumbua viongozi
 
Nina mashaka sana baada ya muda tutasikia yale yale ya mwendokasi. Kufilisika kwa kuwa na biashara iliyozidi.

Bora kukosa mali kuliko kukosa maarifa. Watanzania wenzangu, uongozi ni dhamana. Tusije kusahau hilo maana asilani abadani, ipo siku kama tulichezea hizi nafasi, tutawajibishwa. kama sio duniani, basi mbele ya Mwenyezi Mungu anayeipenda na kuibariki nchi yetu.
 
Punguza ujuaji, sisi watu weusi tuna matatizo. Hizi treni hata huko kwa wenzetu wamachinga wanaingia kuuzia abiria vitu.
Baadae muanze kulalamika wizi 👀👂
 
Baadae muanze kulalamika wizi 👀👂
Nilikuwa napinga hoja ya kuingia na naji ya kunywa na hiyo mibegi mikubwa. Naamini hayo mabehewa yana kamera za kutosha na mwizi akibainika lazima adhabu yake iwe kubwa.
 
TRC ni mojawapo wa wadau wa JF natumai watakuja na majibu haraka
 
Nilikuwa napinga hoja ya kuingia na naji ya kunywa na hiyo mibegi mikubwa. Naamini hayo mabehewa yana kamera za kutosha na mwizi akibainika lazima adhabu yake iwe kubwa.
Nani kakuambia mabegi ya shangazikaja ni makubwa tu! Mbona treni yao ya reli ya kati hakuna vizuizi vya vitu hivyo na hakujawahi kutokea milipuko ya kigaidi, watanzania tukatae kufugwa kama kondoo.
 
Nani kakuambia mabegi ya shangazikaja ni makubwa tu! Mbona treni yao ya reli ya kati hakuna vizuizi vya vitu hivyo na hakujawahi kutokea milipuko ya kigaidi, watanzania tukatae kufugwa kama kondoo.
Ninapinga SGR kuzuia watu kuingia na mabegi ya shangazi kaja na maji ya kunywa, pengine hujanielewa tu. Hata likiwa kubwa kuzuia ni ulimbukeni tu. Yaani hizo treni tumezichukulia kama kitu cha kipekee sana na kuweka masharti kibao. Abiria wenyewe kwa asilimia kubwa ni sisi hawa hawa tunaotumia mabasi kila siku.
 
Ananunua maji anakunywa nusu then anajaza konyagi ndogo, TRC wapo sahihi kwa hilo hata mimi shahidi
Mtu akinywa pombe Kwa starehe zake kuna shida gani?
Mbona treni zingine zina mpaka Bar ndani kabisa watu wanakunywa tu??
 
SGR ISHIKILIE HAPO HAPO MASAA MAWILI MATATU SHANGAZI KAJA WA NINI ?
 
Mtu akinywa pombe Kwa starehe zake kuna shida gani?
Mbona treni zingine zina mpaka Bar ndani kabisa watu wanakunywa tu??
Si zingine tu, hizohizo za TRC na hata hiyo inazo bia. Achana na hao abiria wa daladala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…