Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Mkuu mimi sijaleta ujuaji.
Naandika kwa msisitizo tukubali tukatae Tanzania raia tunapenda sana kulalamika tena saaanaaaa.
Kama huwezi kupanda SGR panda mgr diesel deluxe locomotive.
Katika hivyo vitu kuna jambo la kulalamika mkuu!??
Zote ni trivial complains.
Mambo madogo kulalamika aisee watanzania tuna safari ndefu sana.
Punguzeni kulalamika.
Halafu pia sisi sio watunzaji wa miundombinu hata uchembe.
Kama isipowekwa sheria za udhibiti miundombinu itachakaa mapema hutoamini.
Nilisafiri juzi tu hapa kurudi Dar kutoka Morogoro,sehemu ya kuwekea vitu kile kimeza cha mbele ya kiti mtu anafosi aweke pale mtoto ambadilishe pampers!!
Ushaambiwa pale kisikae kitu kizito na hadi kutangaza wanatangaza.
Mtu ana tissue kamaliza kula haitoshi anapangusa kwa kiti.
Punguzeni kulalamika kwa mambo yasiyo na tija mkuu.
Mkuu kwa hilo la utunzaji nakubaliana nawe 100%. Ila vitu kama maji si vya kuzuia kabisa, na hata wakizuia waviuze kwa bei ya soko, hao abiria wengi wao ni akina sisi pangu pakavu.
 
Kinachoendelea kwenye makatazo kwa abiria wanaopanda treni ya SGR ni kuonesha ushamba na ulimbukeni.

Hili la kukataza mifuko yenye zipu maarufu kama shangazikaja na maji ya kunywa chupa moja! Na vitu vingine visivyokuwa na athari kwa abiria wengine.

Tanzania Railways Corp
Shangazi kaja halitoshi ile sehemu ya kuwekea mizigo unaweka hatarini maisha ya abiria aliyechini...
 
Kinachoendelea kwenye makatazo kwa abiria wanaopanda treni ya SGR ni kuonesha ushamba na ulimbukeni.

Hili la kukataza mifuko yenye zipu maarufu kama shangazikaja na maji ya kunywa chupa moja! Na vitu vingine visivyokuwa na athari kwa abiria wengine.

Tanzania Railways Corp
Taasisi Ona wasemaji

Tusipoteze muda kusumbua viongozi
 
Kinachoendelea kwenye makatazo kwa abiria wanaopanda treni ya SGR ni kuonesha ushamba na ulimbukeni.

Hili la kukataza mifuko yenye zipu maarufu kama shangazikaja na maji ya kunywa chupa moja! Na vitu vingine visivyokuwa na athari kwa abiria wengine.

Tanzania Railways Corp

Nina mashaka sana baada ya muda tutasikia yale yale ya mwendokasi. Kufilisika kwa kuwa na biashara iliyozidi.

Bora kukosa mali kuliko kukosa maarifa. Watanzania wenzangu, uongozi ni dhamana. Tusije kusahau hilo maana asilani abadani, ipo siku kama tulichezea hizi nafasi, tutawajibishwa. kama sio duniani, basi mbele ya Mwenyezi Mungu anayeipenda na kuibariki nchi yetu.
 
Punguza ujuaji, sisi watu weusi tuna matatizo. Hizi treni hata huko kwa wenzetu wamachinga wanaingia kuuzia abiria vitu.
Baadae muanze kulalamika wizi 👀👂
 
Baadae muanze kulalamika wizi 👀👂
Nilikuwa napinga hoja ya kuingia na naji ya kunywa na hiyo mibegi mikubwa. Naamini hayo mabehewa yana kamera za kutosha na mwizi akibainika lazima adhabu yake iwe kubwa.
 
Kinachoendelea kwenye makatazo kwa abiria wanaopanda treni ya SGR ni kuonesha ushamba na ulimbukeni.

Hili la kukataza mifuko yenye zipu maarufu kama shangazikaja na maji ya kunywa chupa moja! Na vitu vingine visivyokuwa na athari kwa abiria wengine.

Tanzania Railways Corp
TRC ni mojawapo wa wadau wa JF natumai watakuja na majibu haraka
 
Nilikuwa napinga hoja ya kuingia na naji ya kunywa na hiyo mibegi mikubwa. Naamini hayo mabehewa yana kamera za kutosha na mwizi akibainika lazima adhabu yake iwe kubwa.
Nani kakuambia mabegi ya shangazikaja ni makubwa tu! Mbona treni yao ya reli ya kati hakuna vizuizi vya vitu hivyo na hakujawahi kutokea milipuko ya kigaidi, watanzania tukatae kufugwa kama kondoo.
 
Nani kakuambia mabegi ya shangazikaja ni makubwa tu! Mbona treni yao ya reli ya kati hakuna vizuizi vya vitu hivyo na hakujawahi kutokea milipuko ya kigaidi, watanzania tukatae kufugwa kama kondoo.
Ninapinga SGR kuzuia watu kuingia na mabegi ya shangazi kaja na maji ya kunywa, pengine hujanielewa tu. Hata likiwa kubwa kuzuia ni ulimbukeni tu. Yaani hizo treni tumezichukulia kama kitu cha kipekee sana na kuweka masharti kibao. Abiria wenyewe kwa asilimia kubwa ni sisi hawa hawa tunaotumia mabasi kila siku.
 
Ananunua maji anakunywa nusu then anajaza konyagi ndogo, TRC wapo sahihi kwa hilo hata mimi shahidi
Mtu akinywa pombe Kwa starehe zake kuna shida gani?
Mbona treni zingine zina mpaka Bar ndani kabisa watu wanakunywa tu??
 
SGR ISHIKILIE HAPO HAPO MASAA MAWILI MATATU SHANGAZI KAJA WA NINI ?
 
Mtu akinywa pombe Kwa starehe zake kuna shida gani?
Mbona treni zingine zina mpaka Bar ndani kabisa watu wanakunywa tu??
Si zingine tu, hizohizo za TRC na hata hiyo inazo bia. Achana na hao abiria wa daladala.
 
Back
Top Bottom