Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Abdallah Mhagama, amesema kuwa kanuni na sheria zinazosimamia utoaji wa huduma za usafiri ziko wazi, na zinaweka masharti kwa watoa huduma ikiwemo kutofanya migomo. Mhagama amebainisha kuwa mgomo wowote unaofanyika kinyume cha sheria unachukuliwa kuwa batili kwa mujibu wa masharti ya leseni zilizotolewa kwa watoa huduma hao.
Akizungumza Aprili 9, 2026 katika mahojiano na Radio One, Mhagama amesema kuwa endapo mtu atashiriki mgomo, mamlaka itashughulikia kila mmoja mmoja kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni. Amesema pia kuwa iwapo wahusika watarudi tena kuomba leseni, watatakiwa kuzingatia masharti mapya tofauti na ya awali.
"Mkurugenzi Mkuu aliongea kwamba kanuni zipo wazi sheria iko wazi mgomo ni batili umepewa leseni ina masharti yake mojawapo kutofanya mgomo, ikiwa mtu atagoma tutadili na mmoja mmoja maana yake ni kufutiwa leseni na atakuja kuomba siku atakayokuja kurudi na tutakuwa na masharti mengine tofauti."