Mkurugenzi Udhibiti Uchumi LATRA: Madereva watakaogoma Aprili 12, kufutiwa Leseni

Mkurugenzi Udhibiti Uchumi LATRA: Madereva watakaogoma Aprili 12, kufutiwa Leseni

Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Abdallah Mhagama, amesema kuwa kanuni na sheria zinazosimamia utoaji wa huduma za usafiri ziko wazi, na zinaweka masharti kwa watoa huduma ikiwemo kutofanya migomo. Mhagama amebainisha kuwa mgomo wowote unaofanyika kinyume cha sheria unachukuliwa kuwa batili kwa mujibu wa masharti ya leseni zilizotolewa kwa watoa huduma hao.

Akizungumza Aprili 9, 2026 katika mahojiano na Radio One, Mhagama amesema kuwa endapo mtu atashiriki mgomo, mamlaka itashughulikia kila mmoja mmoja kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni. Amesema pia kuwa iwapo wahusika watarudi tena kuomba leseni, watatakiwa kuzingatia masharti mapya tofauti na ya awali.

"Mkurugenzi Mkuu aliongea kwamba kanuni zipo wazi sheria iko wazi mgomo ni batili umepewa leseni ina masharti yake mojawapo kutofanya mgomo, ikiwa mtu atagoma tutadili na mmoja mmoja maana yake ni kufutiwa leseni na atakuja kuomba siku atakayokuja kurudi na tutakuwa na masharti mengine tofauti."

Ndio dawa yao mbwa hao
 
Latra shikilieni hapo hapo,hatuwezi kuwa na watu ambao wanaweza kuamua kufanya chochote na wakati wowote, lazima mamlaka husika ziheshimiwe
Exactly...mwaka juzi tu hapa nauli imepanda,mfano Tegeta VS K/KOO ilikuwa 700 now ni TSH 900.... Bunju vs makumbusho ilikuwa TSH 800, sasaivi ni TSH 1100/=

Mbagala kawe pia ivyo,mwenge posta pia ivyo ivyo... karibia njia zote,
Na mikoani pia nauli zilipanda Dar vs Morogoro kutoka Elfu Kumi hadi 13000/= na mikoa mingine pia ivyo ivyo.....Kibaya Zaidi mafuta yakishuka nauli hazishuki.....kumbuka na hesabu pia za gari zinaongezeka , wanafaidika wamiliki wa magari

Mfano sasaivi Kosta ya makumbusho Bunju hesabu ni TSH 110,000/=
 
Latra ni wapumbavu sana, kujipendekeza huku kuwe na mipaka..

Hesabu ya bosi ni laki/110 hii itabaki costant, bosi anataka chake, sababu nae anataka kurudisha hela yake na faida..

Hapa inabaki balaa la hela ya mafuta na na posho yao..

Tufanye kabla ya mafuta kupanda, walikuwa wakitoa hesabu ya bosi, na mafuta, wao wanabaki na 40, kila mtu anazuia 20,20, ama siku nyingine 30,30..

Sasa tujiulize bei ilivyopanda hata hiyo 15,15 ya kugawana wataipata?
Mafuta yatashuka bei week hii kuweni na subira...mkigoma tunaweka gari za Jeshi barabarani zibebe abiria,na nyie gari zenu itakuwa marufuku Tena kuonekana barabarani
 
Mafuta yatashuka bei week hii kuweni na subira...mkigoma tunaweka gari za Jeshi barabarani zibebe abiria,na nyie gari zenu itakuwa marufuku Tena kuonekana barabarani
Yakishuka na sisi tutashusha..
Sawa wekeni hizo gari zenu za wajeda, haziwezi kusolve tatizo la usafiri hata robo tu.. usijiongopee, labda na vifaru na ndege vyote vibebe watu wa dsm na bado hawawezi solve tatizo la usafiri dsm
 
Gomeni muone! Hatutaki baadae muanze oooh! Mama tuhurumie wanao tuna mikopo! Tutadili nanyinyi perpendicular!
 
Latra wapuuzi na wamiliki nao ni wapuuzi tu,kuna kipindi mafuta yalipanda nauli nazo zikapanda baada mafuta yaliposhuka wamiliki wakagoma kushusha nauli.
Nauli zikipanda mafuta yakashuka watataka nauli zibaki hivyo hivyo.
Corona mafuta yalifika mpaka 1500 kwanini hawakushusha bei za nauli??
 
Latra ni wapumbavu sana, kujipendekeza huku kuwe na mipaka..

Hesabu ya bosi ni laki/110 hii itabaki costant, bosi anataka chake, sababu nae anataka kurudisha hela yake na faida..

Hapa inabaki balaa la hela ya mafuta na na posho yao..

Tufanye kabla ya mafuta kupanda, walikuwa wakitoa hesabu ya bosi, na mafuta, wao wanabaki na 40, kila mtu anazuia 20,20, ama siku nyingine 30,30..

Sasa tujiulize bei ilivyopanda hata hiyo 15,15 ya kugawana wataipata?
Mafuta yalipopanda kidogo waliongezewa nauli wakawa wanafurahia super profit na hata mafuta yalipoanza kushuka hawakushusha nauli.

Kwahiyo wewe hoja yako ni kwamba mzigo aangushiwe mwananchi masikini ambaye hata kula yake tu ni shida halafu bado tena umuangushie zigo la nauli?

Wavumilie kwa kipindi hiki cha mpito kwasababu kama ni faida walishatengeneza sana mafuta yaliposhuka na wao wakafurahia nauli kubaki pale pale.
 
Hivi ndivyo inavyotakiwa, madereva wa daladala waliingia makubaliano na LATRA wanajua kila kilichomo ndani ya makubaliano yao.

Kama wanaona biashara ya daladala kwa sasa haiwalipi, vyema waache mabasi yao waende kulima nyanya mashambani, hakuna atakayewalazimisha kurudi barabarani.
 
Back
Top Bottom