Mkurugenzi Udhibiti Uchumi LATRA: Madereva watakaogoma Aprili 12, kufutiwa Leseni

Mkurugenzi Udhibiti Uchumi LATRA: Madereva watakaogoma Aprili 12, kufutiwa Leseni

Serikali kuchujua hatamu ina maana nyingi.

Inaweza kuwa ni kupunguza kodi au kutoa ruzuku.

Kwa namna hiyo serikali inapunguza gharama na ku influence nguvu ya soko.

Kulazimisha biashara ifanyike kwa amri tu

Huko serikalini wamejaa watu wasio na uwezo
bila kujali nguvu ya soko ni kutengeneza matatizo katika uchumi.
Kuna kauli aliitoa professor Asad huwa ina ukweli asilimia mia
Na watawala waone hivyo sasa sio kwa wafanyabiashara pekee kama ni nyeti wanatakiwa kulinda biashara na huduma pia nini wao wamefanya kwa upande wao? Ongeza income kwa walaji au punguza cost za uendeshaji kwa watoa huduma sio kutishia tu kufuta leseni
 
Mafuta yalipopanda kidogo waliongezewa nauli wakawa wanafurahia super profit na hata mafuta yalipoanza kushuka hawakushusha nauli.

Kwahiyo wewe hoja yako ni kwamba mzigo aangushiwe mwananchi masikini ambaye hata kula yake tu ni shida halafu bado tena umuangushie zigo la nauli?

Wavumilie kwa kipindi hiki cha mpito kwasababu kama ni faida walishatengeneza sana mafuta yaliposhuka na wao wakafurahia nauli kubaki pale pale.
Hakuna asiependa super profit, kosa lilikuwa la latra, kwanini hawakupiga kelele za kupunguza nauli, wanakaa vikao wanakula posho za bure..
Wao walipandisha na wao ndio walipaswa kushusha.
 
Akili za mafunzo mbalimbali.

Uliwahi kuona wapi duniani driving licence inakuwa revoked kwa mtu kugoma kuendesha chombo??

Wanaokota wapi hawa vilaza?
 
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Abdallah Mhagama, amesema kuwa kanuni na sheria zinazosimamia utoaji wa huduma za usafiri ziko wazi, na zinaweka masharti kwa watoa huduma ikiwemo kutofanya migomo. Mhagama amebainisha kuwa mgomo wowote unaofanyika kinyume cha sheria unachukuliwa kuwa batili kwa mujibu wa masharti ya leseni zilizotolewa kwa watoa huduma hao.

Akizungumza Aprili 9, 2026 katika mahojiano na Radio One, Mhagama amesema kuwa endapo mtu atashiriki mgomo, mamlaka itashughulikia kila mmoja mmoja kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni. Amesema pia kuwa iwapo wahusika watarudi tena kuomba leseni, watatakiwa kuzingatia masharti mapya tofauti na ya awali.

"Mkurugenzi Mkuu aliongea kwamba kanuni zipo wazi sheria iko wazi mgomo ni batili umepewa leseni ina masharti yake mojawapo kutofanya mgomo, ikiwa mtu atagoma tutadili na mmoja mmoja maana yake ni kufutiwa leseni na atakuja kuomba siku atakayokuja kurudi na tutakuwa na masharti mengine tofauti."

Anayeongoza huo mgomo kama sio mtu wa mfumo litamkuta jambo.
 
Hawa si nilisikia wana kikao cha kujadili nauli mpya , imekuwaje wanachimbiana mikwara🤣
Nimemsikia mwenyekiti wao anasema sehemu ya 600 iwe 750,nk kutoka chanika mpaka Machinga Complex iwe 3000/= huu wizi wa waziwazi.

LATRA kamatia hapo hapo kipindi Fulani mafuta yalipanda na nauli ikapanda yalipo shuka nauli zilibaki vile vile sasa ni mwendo wa serikali kutocheka na hawa majizi
 
Serikali ambayo shirika lake la ndege linajiendesha kwa hasara,shirika la reli nalo hasara tupu halafu inataka na sekta binafsi ijiendeshe kwa hasara!!!šŸ˜€

NB:TABOA ndiyo wameazimia kusitisha kutoa huduma,huyo dereva anahusikaje sasa?
 
Serikali kuchukua hatamu ina maana nyingi.

Inaweza kuwa ni kupunguza kodi au kutoa ruzuku.

Kwa namna hiyo serikali inapunguza gharama na ku influence nguvu ya soko.

Kulazimisha biashara ifanyike kwa amri tu bila kujali nguvu ya soko ni kutengeneza matatizo katika uchumi.
Swadakta ,kiujumla bado serikali inatuona wajinga kupitiliza so far kuna wajinga bado wanaendekeza uchawa ,how come kiongozi unakuja tu kutishia kusiwe na mgomo na haji na mikakati ya serikali juu ya kuongezeka kwa bei ya mafuta
 
Exactly...mwaka juzi tu hapa nauli imepanda,mfano Tegeta VS K/KOO ilikuwa 700 now ni TSH 900.... Bunju vs makumbusho ilikuwa TSH 800, sasaivi ni TSH 1100/=

Mbagala kawe pia ivyo,mwenge posta pia ivyo ivyo... karibia njia zote,
Na mikoani pia nauli zilipanda Dar vs Morogoro kutoka Elfu Kumi hadi 13000/= na mikoa mingine pia ivyo ivyo.....Kibaya Zaidi mafuta yakishuka nauli hazishuki.....kumbuka na hesabu pia za gari zinaongezeka , wanafaidika wamiliki wa magari

Mfano sasaivi Kosta ya makumbusho Bunju hesabu ni TSH 110,000/=
So far wamiliki wa mabasi nao wapo kwenye unyonyaji kama serikali inavyofanya hivi ni vitu ambavyo wanatakiwa kuzifanyia kazi sio kuzuia mgomo
 
Exactly...mwaka juzi tu hapa nauli imepanda,mfano Tegeta VS K/KOO ilikuwa 700 now ni TSH 900.... Bunju vs makumbusho ilikuwa TSH 800, sasaivi ni TSH 1100/=

Mbagala kawe pia ivyo,mwenge posta pia ivyo ivyo... karibia njia zote,
Na mikoani pia nauli zilipanda Dar vs Morogoro kutoka Elfu Kumi hadi 13000/= na mikoa mingine pia ivyo ivyo.....Kibaya Zaidi mafuta yakishuka nauli hazishuki.....kumbuka na hesabu pia za gari zinaongezeka , wanafaidika wamiliki wa magari

Mfano sasaivi Kosta ya makumbusho Bunju hesabu ni TSH 110,000/=
Ni sahihi kabisa ulivyosema,hawa sio wa kuwaendekeza kabisa,ukitaka kujua bado wanapata faida,ikitokea Serikali ikakaza utawaona wanaoperate kama kawaida
 
Shida ni nchi isiyo na mifumo. Watengeneze mifumo, bei ya mafuta ikipanda kwa a certain percentage na nauli inapanda kwa kiwango Fulani. Mafuta yakishuka kwa percentage Fulani na nauli inashuka hivo hivo. Mbona ni simple tuuu!
Pili waweke mfumo wa kutangaza bei za nauli kila mwezi Kama wanavotangaza bei za mafuta.
Kinyume na hapo hakuna atakayekubali kufanya kazi ya hasara. Serikali mpira ulikuwa mikononi mwake imeshindwa kuucheza kwa akili sasa na wenye ma-bus na malori nao waache huru kucheza mpira wao.

Hao Latra walikuwa wapi wakati bei ya mafuta inapanda? Latra ni Chombo cha upigaji hakina hata maana. Wana-regulate usafiri lakini wanashindwa ku-play fair game .
Mafuta yalipopanda kidogo waliongezewa nauli wakawa wanafurahia super profit na hata mafuta yalipoanza kushuka hawakushusha nauli.

Kwahiyo wewe hoja yako ni kwamba mzigo aangushiwe mwananchi masikini ambaye hata kula yake tu ni shida halafu bado tena umuangushie zigo la nauli?

Wavumilie kwa kipindi hiki cha mpito kwasababu kama ni faida walishatengeneza sana mafuta yaliposhuka na wao wakafurahia nauli kubaki pale p
 
Back
Top Bottom