Uhuni mtupu, hii nchi hata wananchi hawajui wanataka kitu gani, huwezi amini, hawa wanaolalamika serikali kuzuia upandishwaji wa nauli kiholela ndio hawa hawa wanalalamika mafuta kupanda bei, na ndio hawa hawa nauli zikipanda serikali ikikaa kimya wanalalamika.
Ni kweli serikali hatuipendi lkn kuna muda tuache ushabiki wa kisiasa za kitoto, hawa wafanyabiashara za usafirishaji wamekuwa wahuni sana, mafuta yakipanda kidogo wanalilia upandishwaji bei nauli wakati huo ongezeko wanalodai huwa halina maana kwao zaidi ya kumuumiza abiria wa kawaida.
Uhalisia uko hivi, kwa lita moja ya mafuta kwa 4,000Tsh, daladala inauwezo wa kutembea 10km, ktk hizo 10km daladala inabeba abiria si chini ya 30, kwa nauli ya 700Tsh kila kituo ndani ya 10km kwa abiria si chini ya 30 ni sawa na konda amepokea 21,000 Tsh hapo kwa root moja tu ya kwenda, haya tufanye 4,000Tsh ya mafuta, 700Tsh(nauli)×30(idadi ya abiria within 10km) = 700*30= 21,000Tsh-4,000Tsh(ya mafuta within 10km) = 17,000Tsh hiyo ni faida anayoipata konda wa hii daladala kwa root moja tu ya kwenda, ktk zile lita 1 za mafuta, hapo anakuwa na faida kubwa hata bila kumuongezea abiria nauli ambayo Kama wafanyavyo sasa
10km za root moja, 700 nauli iliyokuwa+ 300Tsh ongezeko= 1000× 30(idadi ya abiria kwa 10km) = 30,000Tsh- 4,000Tsh(mafuta per litre), = 26,000Tsh sawa na ongezeko la 9,000Tsh kwa kila root, yaani wanaililia 9,000 kwa root moja ambayo haiaffect gharama za usafirishaji, ni ongezeko dogo sana kwa aina hii ya biashara yenye mzunguko mkubwa wa pesa.
Uhalisia ni kwamba hawa wapumbavu wafanyabiashara wa usafirishaji ni wezi wanaopenda kufaidika kwa kumnyonya mwananchi wakati huo wakisingizia ongezeko dogo ambalo haliaffect hali ya usafirishaji zaidi ya ubinafsi.
Ningependelea serikali iwapige ongezeko kubwa la kodi ili iwe 50 to 50 waone uchungu wa kuwanyonya wengine.
Biashara ambayo ina uhuni mwingi ni pamoja na hii, nauli hazina uhalisia kuanzia pikipiki(boda boda), bajaji, daladala, mabus , yaani ni uhuni mtupu haikidhi vigezo vya uhalisia wa milinganyo ya kiusawa, ktk biashara lazima iwepo win to win, kitu unachokinunua kwa bei ndogo unapokigeuza huduma kwa wananchi lazima kikidhi uhalisia wa gharama zake na sio kujipangia kihuni
Serikali piga pin mbwa hizo.
Mbona wakulima miaka nenda rudi bei za mazao ni ndogo tofauti na uhalisia lkn hatuoni wakiwapandishia bei kiholela kama haya majizi ya usafirishaji?, hii nchi bila sheria kali tutaoneana