Wagome au kusitisha huduma wote, tuone watafungia leseni ya nani na kuacha ya nani!. Atakayeingiza gari barabarani gari itiwe moto tu.
UTARATIBU WA KUWASILISHA MAOMBI YA KUPANDISHA NAULI ZA MABASI YA ABIRIA
Ndugu Msomaji
Utaratibu wa kupandisha au kushusha nauli za mabasi ya abiria unaongozwa na sheria ya LATRA Sura ya 413 pamoja na Kanuni yake inaiyoitwa
The Land Transport Regulatory Authority(Tariff) Regulations,2020 yaani Kanuni ya LATRA ya Tozo ya Mwaka 2020. Kanuni hii imetungwa chini ya kifungu cha 45 cha sheria. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA hawezi kukurupuka tu au kuamka tu asubuhi na kutangaza kushusha nauli au kuongeza nauli, bila kufuata masharti na maelekezo ya sheria.
MAOMBI YA MAPITIO YA NAULI
Maombi ya mapitio ya nauli yanaweza kuwasilishwa na mtoa huduma (Msafirishaji) kwa mujibu wa Kanuni ya 9(1) ya Kanuni za Tozo, kupitia fomu maalumu iliyopo kwenye jedwali la pili la Kanuni hizo. Maombi hayo ni lazima yaambatanishwe na nyaraka zifuatazo:
1.
Leseni hai ya usafirishaji. Kwa maana ya kwamba kama leseni yako sio hai hutakuwa na sifa za kuwasilisha maombi.
2.
Nauli Pendekezwa, yaani unapendekeza nauli iwe kiasi gani kwa kilometa au kwa daraja fulani.
3.
Sababu na uhalalisho (justifications) wa maombi ya mapitio ya nauli, ikiwemo kueleza Mteja atafaidika vipi na mapitio hayo, kwa maana ya kwamba unapoomba nauli iongezeka lazima utoa sababu, kama ni hasara uoneshe hiyo hasara unaipata wapi na kwa nini?
4.
Mkeka unaoonesha namna ulivyokokotoa au kupiga hesabu au kufikia nauli unayopendekeza, yaani huweza kuamka tu na kusema nataka nauli ya dalala iwe shilimgi 1000 kitoka 600 iliyopo sasa. Lazima uoneshe umefikiaje hilo hitimisho kwamba 1000 ndio itafaa.
5.
Hesabu zilizokaguliwa za biashara yako kwa kipindi cha miaka 3 nyuma, yaani kwa mfano, unaomba nauli zipande mwaka 2026 lazima ulete hesabu zako za mwaka 2025; 2024; na 2023 au chini yake. Hesabu hizo ziwe zimekaguliwa na Mkaguzi wa Mahesabu Aliyeidhinishwa (Certified Auditor)
6.
Taarifa ya Ufanisi wa Biashara yako (Performance Report) ikiwemo mchanganuo wa uendeshaji (technical operations) na uchambuzi wa kifedha (financial analysis) kwa miaka 5 iliyopita au chini yake kulingana na umri wa biashara.
7.
Nyaraka nyingine yoyote inayosapoti maombi yako kama itakavyoelekezwa na mamlaka.
Kwa ujumla, mtoa huduma anaweza kupeleka maombi ya mapitio ya nauli baada ya kipindi cha
miaka 3 tangu yalipofanyika mapitio ya mwisho. Yaani tangu zilipotangazwa nauli mara ya mwisho. Ndio kusema kwamba
Nauli ikitangazwa na LATRA hudumu kwa kipindi cha miaka 3
Hata hivyo, Mtoa huduma wakati wowote ule, anaweza kupeleka maombi ya mapitio ya nauli iwapo marejeo ya mtaji wake (return on investment) ni chini ya 10%. Lakini pia maombi ya mapitio ya nauli yanaweza kufanywa iwapo marejeo ya mtaji ni zaidi ya 25% yaani mtoa huduma anapata zaidi ya kile anachostahili. Mara nyingi maombi haya hufanywa na abiria au vyama vinavyowakilisha maslahi ya abiria.
Na pia mtoa huduma anaweza kuwasilisha maombi ya mapitio ya nauli kwa niaba ya watoa huduma wengine.
Aidha, Maombi ya mapitio ya nauli yanaweza pia kufanywa na watumiaji huduma (abiria). Hili tutaeleza kwenyw somo linalofuata.
Ni imani yangu umeongeza ufahamu kuhusu jambo hili
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.